Gambino
Hapa naona mnalishana matango pori! Hakuna horizontal transfer katika mashirika ya umma. Horizontal transfers zinawezekana katika idara za serikali, yaani mtu unaweza kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa. Au kuhama kutoka serikali kuu kwenda shirika linalifanya kazi moja kwa moja na wizara inayohusika kwa mfano kutoka DAWASA kwenda wizara ya maji au Chuo cha maji.
Mashirika mengi ya umma ni autonomous yanajitegemea kwa kwa kila kitu. Mtu hawezi kuhama kutoka UDSM kwenda TANESCO isipokuwa kama nafasi ya kazi itatangazwa na wewe kuiomba na kuchaguliwa. Mashirika ya umma yana salary scheme zinazotofautiana, kwa hiyo ukiajiriwa katika shirika lingine unaanza ajira upya na hakuna muendelezo wa ajira ya shirika lako la mwanzo.