Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu anatunga listor.........Ugumu wa maisha unasababisha watu wafanye vitu vya aibu sana.
Watu wataprefer bure kuliko kazi ,mm hutoa mtaji sio matumizi ,mtaji ni one time hatujuani ,matumizi ni maisha ,mungu ndo atakupa matumizi au wewe mwenyewe ,wengine ni tukijaaliwa ni mtaji tuuDuniani huwezi ukamfurahisha kila mtu mtu anakuja kukaa tu nyumbani hana kazi anatafta nini?sijawahi fuga mtu kwangu et aamke anakula na kuangalia tv kwangu ni big no?mtu wa hivyo humsaidii bali unamlemaza
Kaa nao waambie kesho ondokeni tunaishi kwa bajeti hapa mjini period.Habari za siku nyingi watu wa Mungu.
Hivi ni utaratibu gani unafaa kufuatwa katika kuchagua ndugu wa kuishi nao baada ya ndoa. Nakumbuka mwanzo kabisa kipindi namuoa mke wangu nilimjulisha kuwa napenda sana ndugu ila kuishi na ndugu ni mtihani kama mtu ana uhitaji na tuna uwezo wa kumsaidia bora tumsaidie huko huko aliko kukiwa na ulazima sana ndipo ataishi kwetu.
Bahati mbaya huyu mwenzangu na ndugu zake wamefanya nyumba yangu kijiwe ndugu zake wote wapo hapa hapa mjini sasa imekuwa anakuja huyu anakaa wiki anaondoka wanapokezana , likizo watoto zao wanawaleta kwangu na wana vurugu kweli ile likizo ya mwaka mpya walinivunjia side mirror ya gari ikabidi niwafukuze manake walikuwa wakiaanza kukimbizana wanapita mpaka juu ya makochi ilibaki kidogo wakanyage kompyuta niliwafukuza siku hiyo hiyo.
Tatizo la pili kuna ndugu zake hawa watu wazima wakike ambao ni dadazake ni wakubwa kiasi mmoja binti yake ndiyo mwenye watoto niliowafukuza, hawa wanakaa tu nyumbani hawafanyi chochote ni kuangalia tu tamthiliya mpaka kurudi nyumbani sasa naona kero mimi na wife hatujajaliwa watoto sasa hapo nyumbani kuna familia ya watu 4 na wote wanatokea hapo mabibo yaani mimi ndio nimekuwa kama mgeni kwenye familia.
Nikimuambia hawa watu kwanini wasirudi kwenu kwenye nyumba ya familia wakae sisi tutakaa nao mpaka lini anasema soon wataondoka toka mwezi wa pili anasema hivyo soon wataondoka, karibuni mama anataka kuja kwenye matibabu MOI ila kagoma kufikia kwangu hawezi lala kitanda kimoja na mtu mwingine anashida na mifupa.
hapo bado kuna ndugu zake wanakuja tu wikend wakijisikia na wakiondoka hawana nauli wanakuomba tena shemeji nauli hasa namuuliza hawa nao wanakuja kila wikend kufanya nini, anasema kama sitaki ndugu zake waje atawaambia ila tatizo sio kuja tatizo hata nauli hawana ukiwapa ndogo wanakuimbia kuna sehemu ya kupanda bodaboda.
Ajabu wao wenyewe kwa wenyewe hawatembeleani ni kama vile wanaamua kunimalizia pesa hivi. Nipeni busara kudeal na hawa watu nahisi kuanza kukata mahitaji.
Wewe dada mwenye HIV.Tukiwaambie mje kuoa huku kwetu usukumani mmatuona wakuja kweli, ona sasa mswahili wa uzaramoni anavyokupeleka. Pole lakni mwaya