Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

Mapilot mbona wengi tu [emoji1]
Anawapata,kuna tajiri yangu mmoja
Alikuwa myahudi anaitwa malapa
Ah tulikuwa tunapuyanga sana na kadege kake tanzania hii
Parking fee kwa 12hrs ilikuwa 2000 kwa ndege za ndani
Ila za nje $5 kwa 12hrs,service na bima kdg ndy ilikuwa imechangamka
Hapo ujipqnge kdg...ila kama mtu uko na mipango ndege mbn unaimiliki kama ist tu [emoji1]

Ova
😆 tatizo kakianguka halafu ndio safari ya 2 tu
Acha nindelee na malori tu
 
Tanzania ndio nchi pekee watu wanapinga hadi ndoto za watu.

Mtu kaulizia bei tu raia zinampiga spana na kumwambia hana pesa ya kununua ndege😃
Sina uhakika kama ni Tanzania pekee ndiyo kuna watu wa aina hiyo, ila nakubali kuwa baadhi ya Watanzania wana mitazamo hasi sana inapotokea mtu anataka kufanya kitu ambacho wao hawajakifanya. Ni tofauti na kwa baadhi ya Mataifa. Huwa naingia mara chache baadhi ya mitandao ya Kimataifa, kama Reddit na Quora (japo nimejiunga hivi karibuni tu). Mijadala yao ni mizuri sana . Wako very serious. Kwa nyuzi chache nilizozifuatilia, ni nadra sana watu kujibu kwa kukejeli. Anajitahidi kujibu mpaka unaona kabisa huyo mtu kajibu kwa uwezo wake wote.

Hata hivyo, hata huku Tanzania, na hasa Jamii Forum, tunao watu wakarimu kama hao. Hata kwenye huu uzi, kuna watu wamejibu vizuri sana, kwa ukarimu wa hali ya juu. Nakiri hata mimi nimejifunza mengi kupitia huu uzi, kutokana na ukarimu wa wachangiaji.

Kwa hiyo pamoja na kuwa kuna watu wachache walio na mzaha, kuna watu, tena wengi tu ambao wapo serious kwenye mambo serious.

Muhimu ni mtu kujua kuchuja kwa kuachana na yaliyo hasi na kuchukua yanayokufaa.
 
Mapilot mbona wengi tu [emoji1]
Anawapata,kuna tajiri yangu mmoja
Alikuwa myahudi anaitwa malapa
Ah tulikuwa tunapuyanga sana na kadege kake tanzania hii
Parking fee kwa 12hrs ilikuwa 2000 kwa ndege za ndani
Ila za nje $5 kwa 12hrs,service na bima kdg ndy ilikuwa imechangamka
Hapo ujipqnge kdg...ila kama mtu uko na mipango ndege mbn unaimiliki kama ist tu [emoji1]

Ova
Au anaweza kupiga course yeye mwenyewe akaendesha kupunguza gharama , ndege ndogo na chopper hazina ugumu wowote ni kupiga course Tu,kupata leseni then unarusha chuma
 
Au anaweza kupiga course yeye mwenyewe akaendesha kupunguza gharama , ndege ndogo na chopper hazina ugumu wowote ni kupiga course Tu,kupata leseni then unarusha chuma
Tuliambiwa Sekondari kuwa mtu anayeweza kusoma "udereva" wa ndege lazima awe "mkali" wa Hesabu na Geography. Kwa hilo unasemaje?
 
Hongera sana kwa kuwaza hilo.

Zipo used ambazo utapata kuanzia 200m.

Ikiwa nje sasa mengine piga hesabu zako.

Au kusanya ununue mpya tu na ukihitaji pilot naweza kuchukua license nikawa naendesha 😄
Na Mimi natamani sana kujua "kuendesha" ndege.

Mafunzo ya kurusha ndege ndogo huchukua muda gani?
 
Na Mimi natamani sana kujua "kuendesha" ndege.

Mafunzo ya kurusha ndege ndogo huchukua muda gani?
Kuna LAPL ambayo ni light aircraft zile ndogo zisizozidi tani 2 uzito na kupata license lazima ukamilishe masaa 30 ya kuendesha na mafunzo pia
Inakuchukua mwaka au chini ya mwaka inategemea na mda wako
Kwa 🇬🇧 unalipa £6000 kama 18m
Na PPL Private pilot license hiyo ni kuanzia £7000-12,000
Sio mbaya kama unapata makampuni au hata kwenye mbuga za wanyama
Wapo watu wanachukua for fun 😁
 
Back
Top Bottom