Rafiki yangu ana kampuni Ina miezi kama 8 tangu ianzishwe, imeshafanya tenda kadhaa za serikali. Kutokana na kupata tenda zinazohitaji mtaji mkubwa na yeye hana mtaji ameamua kutaka kuniunganisha Mimi na mwenzangu mwingine tuwe wakurugenzi pia.
Je inawezekana kuzivuruga HISA za kampuni zake ili tuanzie kuzigawa upya au taratibu zikoje?
Kama una swali lolote linalohusiana na kampuni katika upande wa usajili wake, kufanya mabadiliko, kodi za TRA na chochote kile kinachohusu kampuni kwa BRELA na TRA uliza hapa nitakujibu. Karibu