Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Hasa sisi tunaoishi mijini, kumekuwa na changamoto katika utunzaji wa familia zetu. Kwa walio wengi, hupenda kila siku kuacha hela za matumizi kwa familia zao; wapo wanaoacha elfu kumi kwa siku, ishirini, laki n.k
Na waachapo hiyo fedha, ndio inayofanya manunuzi ya chakula kwa siku husika. Ndio maana wengine wakaamua kuibatiza na kuiita kodi ya meza, au wengine wanaiita kodi ya kitanda n.k
Kwangu binafsi nilishawahi kutumia hiyo fomula, lakini nikaona nakuwa mtumwa wa kila siku. Usipokuwa na fedha kwa siku husika au pungufu, mambo yanakuwa hayaeleweki eleweki.
Baada ya kujitafakari kwa kina, nikagundua hii njia sio sahihi kwa sababu unakuwa unahangaikia tumbo tu, na mambo ya msingi ya kimaendeleo yanakuwa hayaendi.
Kwa mtazamo wangu, pale upatapo hela, weka 'stock' ya chakula hata miezi sita kutokana na uwezo wako. Fedha ndogo ndogo za kubadilishia mboga kwa siku, mkabizi mke au mtu anayesimamia mambo ya ulaji wa familia.
Hata kama kipato chako ni kidogo, jaribu kujikusanya na uweke 'stock'. Baada ya hapo, hela utakayokuwa unaipata kutokana na jitihada zako, wekeza kwenye mambo yako ya msingi ya kimaendeleo.
Hii itapunguza msongo wa mawazo, hasa pale uchumi wako utakapokuwa unatetereka; kwa sababu familia yako haitalala njaa, lakini pia mambo yako ya msingi yanakuwa yamepiga hatua.
Kwa hali hiyo, huu utaratibu wa kutoa hela ya matumizi kwa kila siku husika, naona sio mzuri.
Njooni kwenye mjadala....