Utaratibu wa kutoa talaka upoje?

Kiislam .
Andika barua kwa mkono wako.

Mimi fulani bin fulani , nikiwa na akili zangu timamu , na bila ya kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yoyote , nimeamua kukutaliki fulani binti fulani , hivyo kuanzia leo hii tareh...... wewe sio mke wangu wa ndoa.
Nakutakia maisha mema.

Jina na saini yako.

Mashahidi wawili ,
Majina yao na saini zao.

Halafu piga photocopy , original mmkabidhi yeye, copy moja mkabidhi babamkwe au walii wake ( sio lazima lakini ), copy moja ibaki kwako.
Kazi imekwisha.

Kama anaishi nyumbani kwako , akae hapo mpaka kipindi cha eda ya talaka iishe ndio anaondoka.
Ukimuingilia kwa tendo la ndoa kabla kipindi cha eda kuisha , talaka inakufa , ila itahesabika talaka moja tayari.
 
Kwenye hii sekta ya ndoa mko vizuri sana kuliko sisi Wagalatia. Na kwenye mazishi. Mambo simple kabisa. I admire you guys!
 
Mimi ndo mwenye shida katika ndoa, sitaki kumtesa mtoto wa watu
Kama shida ni wewe je yuko tayari kukuvumilia ? Kama yuko tayari kuvumilia shida zako , usimtaliki maana hapo utakuwa umemuonea sana, ila kama yuko tayari kuachwa basi sawa.
 
Umempa ushauri wa pumba wewe na watu bado wanakupa (like) ama kweli kwnye miti hakuna wajenzi. umeanza vizuri umekuja kumaliza maneno ya pumba lohh majangaa kweli.
 
Nafikiri umeongea kama mwana dini uliyelishwa daawa madrasa na hajaongea kama mtu aliyesoma Sheria ya ndoa ya Tanzania ambayo imejumuishwa na kufanya mjumuisho wa Sheria za kimila katika ndoa, dini zote na wale wasiofuata misingi yoyote katika hayo.

Kwa Taarifa yako, ndoa zote zinazofungwa ziwe za kiserikali, za dini zote nk ni ndoa za kiserikali na sio Kila kiongozi wa dini anaruhusiwa kufungisha ndoa nazima wawe na kibali na kusajiliwa serikalini. Hivyo Kuna watu wanafungishwa ndoa na watu wasio na kibali, zinakuwa batili mwanzo mwisho.
Hivyo, ndoa nyingi zinavunjika kienyeji kwa hivyo mnavyoviita talaka 3 , na watu kwa ujinga wao wa kutokujia Sheria wanaishiwa kugandamizwa kwa woga wa dini. Ila akienda mahakamani ile ndoa inakuwa bado hai na Mahakama ndio Ina mamlaka ya kuvunja au kuto kuvunja na kugawa upya Mali bila ubaguzi na kutoa amri ya matunzo ya watoto kwa mujibu wa Sheria.Mifano ni mingi ya kesi za namna hiyo na haki zimetolewa.
 
Umempa ushauri wa pumba wewe na watu bado wanakupa (like) ama kweli kwnye miti hakuna wajenzi. umeanza vizuri umekuja kumaliza maneno ya pumba lohh majangaa kweli.
Pumba iko wapi hapo.
Niko sahihi talaka hawndiki yeye
Naongea kama mwanasheria sio mganga wa kienyeji
 
hapana mkuu
ndoa za kiislamu siyo lazima BAKWATA wilaya hata ukitamka tu kwamba kuanzia leo wewe siyo mke wangu ni talaka tayar,
ukiandika zinaanzia moja mpaka 3 ila ukimpa tatu hutamrejea kirahisi
Note: ndoa zinachangamoto ila talaka siyo jambo zuri kaeni muyazungumze mkiwashirikisha wakubwa
 
siyo vizuri kuongea mambo usiyoyajua wala kuwa na ushahidi nayo. Hapa uliandika kwa hisia tu na wala huna ukweli wowote
 
Unaongea kulingana na uwelewa wako.Inategemea walifunga ndoa ya aina gani
 
Unaongea kulingana na uwelewa wako.Inategemea walifunga ndoa ya aina gani
Sio uelewa wangu ni sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 wewe ndio umejaza kichwani propaganda ambazo sio za kisheria na yawezekana Kuna sehemu umekaririshwa ukayameza kama yalivyo, na umeendelea kuamini yapo hivyo.
 
Labda muowane kwa kutamkiana hivyo hivyo. lakini mkisaini vyeti vya serekali hamuchani kienyeji namna hiyo
 

Inanisikitisha sana; Kwani imeshindikana kabisa kumaliza mgogoro wenu kwa amani mkaendelea kufurahia maisha yenu.Mbona maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana.Kwa nini kugombana gombana
 
VIP akienda mahakamani unadhani mahakama itapokea icho kikaratasi Chako unachoita talaka.jamani mue na uwelewa ndoa Ni Mali ya serikali mahakama peke yake ndio imepewa mamlaka ya kuvunja ndoa
 
Siku hizi mahakama nasikia hazicheleweshi kesi za talaka .

Kwa jinsi wanandoa wanavyoumizana na kuuana naona wamehamasika
Ku-facilitate kesi kuisha haraka.
 
Kama nafsi imekataa usilazimishe kuishi nae maijepata matatizo bure!
 
VIP akienda mahakamani unadhani mahakama itapokea icho kikaratasi Chako unachoita talaka.jamani mue na uwelewa ndoa Ni Mali ya serikali mahakama peke yake ndio imepewa mamlaka ya kuvunja ndoa
Hiyo ni kwenu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…