Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KAMA NDOA YENU ILIKUWA YENYE BARAKA ZA MUNGU BASI NA KUACHANA KWENU NI MACHUKIZO KWA MUNGU.Upo tiyari kukaa bila kuoa tena mpendwa? Kumbuka kuachana ni machukizo kwa Mungu!
Malaki 2:16
Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
Hili la wake washirikina ni tatizo kubwa hasa kwa wanawake waliotoka kwenye familia zenye kuamini ushirikina. Kuna sababu nyingi za wanawake kuendea waume zao kwa waganga na moja ambayo inaniacha hoi ni yua kutaka eti mume awe chini ya masharti ya mwanamke, yaani mwanamke awe ndiye msemaji wa mwisho hasa kwenye mambo ya fedha. Pia awe na uhuru wa kutoka atakavyo na pia kuchepuka. Mimi huwa siamini kwenye ushirikina hata kidogo na nina uhakika hakuna dawa inayoweza kumpumbaza mwanaume. Nachoogopa ni kulishwa uchafu au sumu kwa sababu waganga wanatoaga maagizo ya tata sana. Mke anaweza kuambiwa aingize kipande cha nyama kwenye sehemu ya haja kubwa kilale ndani halafu kesho yake akiunge vizuri na mboga, ampe mume.Kama una mchepuko basi huenda ndio aloleta mfaraka wa nyie kutaka kuachana.
Anataka muachane umuoe yeye.
Tafakari.
Michepuko wengi ni wachawi na washirikina.
Ni wachache sana ambao hawarogi wanaume.
Off course hata wake wa ndoa nao wapo wengi tu wachawi na washirikina sana tu.
Hasa wale ambao ni tegemezi kiuchumi.
Awe hafanyikazi rasmi kabisa au anafanya lakini kipato kidogo kama rafiki zake Mr. Mpwayungu Village.
Maana anajua ukimuacha hataweza kuishi maisha yenye hadhi mnayoishi akiwa na wewe.
Au la alenge kugawana Mali.
Je, kama mume na mke akienda kwa pamoja na kusema wameamua kuachana kwa amani kwani wameona ndoa yao ina misukosuko sana?Habari Mkuu
Kuna vitu muhimu vya kufahamu hasa linapokuja swala la talaka kwani watu wengi hudhani talaka ni jambo la wanandoa pekee, si kweli.
1. Talaka hutolewa na Mahakama, hivyo ili kupata talaka ni lazima ukafanye maombi Mahakamani na si kila Mahakama bali itakupasa kuzingatia maelekezo ya sheria kulingana na aina ya ndoa yenu
2. Talaka hutolewa kwa kuionesha Mahakama sababu za msingi za kuifanya iamini kuwa ndoa yenu hioyo hairekebishiki tena. Fahamu kuwa Mahakama yenyewe haipendi kutoa talaka/kuvunja ndoa za wapendanao.
3. Talaka itakupa uwezo wa kutambulika kama mtu asiye ndani ya ndoa, hii ina maana kuwa kwa wakristu wataweza kuoa/kuolewa tena na kwa waislamu itahesabu ongezeko la idadi ya nafasi ya kuoa mke mwingine, kwa watamaduni vivyo hivyo pia.
4. Talaka hutolewa kwa ndoa inayotambulika kisheria na ili kuthibitisha uwepo wa hiyo ndoa ni sharti pawepo cheti cha ndoa hiyo. Hii ni kwa ndoa za aina zote, kidini, kiserikali na kimila, ni sharti ndoa iwe imesajiliwa kwa msajili wa ndoa.
5. Kabla ya kufanya maombi ya talaka Mahakamani ni sharti muwe mmeshapita kwenye usuluhishi wa ndoa, na ikashindikana kusuluhishwa hivyo mkapatiwa hati ya kushindwa kwa usuluhishi. Usuluhishi unaweza kufanywa na Baraza la kata au mabaraza ya kidini ya usuluhishi wa ndoa, ila sharti Baraza hilo liwe linatambulika kisheria.
6. Baada ya talaka kinachofuata ni mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja, hapa ni lazima ijulikane kuwa huu mgawanyo una wahusu watalaka pekee na wala hauwahusu watoto wao. Kumekuwa na mazoea na dhana kwamba mali tutawapa watoto, hii ni kinyume na sheria. Zipo kesi za Mahakama Kuu zilizopinga hili swala/mtazamo.
Mwisho kabisa, pole kwa maswahibu Mkuu, pima uzani wa unayopitia kisha tafakari vizuri kama kweli talaka ndjo suluhisho la hayo maswahibu. Ukiona ndio basi fuata utaratibu, ukikwama unaweza niuliza siku yoyote nitakupa mwanga pindi nitakapoona swali lako.
Kila la kheri.
Kwako wewe kipimo cha akili ni uwezo wa kuishi na mke, wakati vichaa tunaona wanazaa.Habari hizo ni nadra sana kuzisikia na ni matokeo ya wanaume wasio na akili kuoa
Mwanaume asiye na akili hatakiwi kuoa.
Kuoa kunahitaji mwanaume mwenye akili sio jinga jinga.Hayo majinga jinga ndio huua
Kwenye bibilia mahali inatakiwa ya garama gani, ili Mungu aibariki ndoa.Yaan ni muislam ndo uanzishe mpaka uzi? Wewe chana kikaratasi hata kama ni cha kufungia maandazi, andika hivi" kuanzia keo mimi na wewe basi" mpelekee
Yaan waislam mbaoana kwa ndoo moja ya maandazi, na chai ya rangi, kuachana ndo uangaike?
Nasikia hata sms moja tu mnaachana unasubiri nini?
Kabla ya kuleta vitu humu uwe na utaratibu wa kuomba ushauri si kila linalo kukwaza unaleta humu. Sasa subiri upewe unacho hitaji.Kwema humu,
Nisiwachoshe nimeishi na mke wangu kwenye ndoa mpaka sasa ni miaka mitano ila kutokana na changamoto za ndoa nilikuwa nahitaji tuachane kwa amani na mke wangu pasi kugombana, kwahiyo nilikuwa nahitaji kumpa talaka.
Msaada wenu taratibu za kuandika talaka upoje?
Tatizo lako umeshindwa kuelewa hiyo sheria inasimamia ndoa za kiserekali zinazo fungwa bomani.[emoji777] Kwa Sheria ya ndoa ya Tanzania , hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuandika Wala kutoa talaka tofauti na Mahakama baada ya kupitia taratibu zote na kubaini kuwa ndoa imevunjika vipande vipanda Haina spea na Wala haitawezekana tena kwa wanandoa hao kuishi pamoja.
[emoji736] Utaratibu, unasnzia kwa Baraza la usuluishi la Kata, pale ambapo mmoja wa wandoa ataoeleka malalamiko, basi Baraza litawaita na kuwasikiliza kwa lengo sii la kuvunja ndoa Bali kuwasuluisha maana kwa mujibu wa kifungu Cha 9 Cha Sheria ya ndoa na kesi ya Hyde vs Hyde lengo la ndoa ni wanandoa waishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe. Baraza likishindwa kusuluisha litaandika certificate kwa mahakama kuwa usuluishi umeshindikana. Hivyo hakuna kesi yoyote ya maombi ya talaka yatapikelewa mahakamani kabla ya kupitia kwenye Baraza la usuluishi linambulika kisheria. Mtu mwenye dini Fulani ambapo ndoa imefungwa kwa misingi hiyo na wanayo mabaraza ya usuluishi, mabaraza hayo yanaweza kutbulika kama mbadala wa mabaraza ya Kata.
[emoji736] Kesi ikifika mahakamani, baada ya kuwasikiliza itsona kama kweli haiwezekani wanandoa Hawa kuendelea kuishi pamoja na kabla haijatoa talaka lazima itoe muda wa kisheria wa wanandoa kujitafakari hii order ni separation ambayo ni decree nisi.
[emoji736] Baada ya muda wa separation kuisha mahakama itawasikilizs tena kama bado mambo ni magumu basi itatoa talaka na amri za matunzo ya watoto ( kama wapo) na mgawanjo wa Mali walizochuma pamoja .
[emoji777] Hivyo, kwa Sheria zetu, makatatasi wanaojiandikia watu kwa kusema mara ni talaka tatu, mara talaka rejea kimsingi Yale sii talaka na hayana effect ya kuvunja ndoa, mmoja wao akienda mahakamani kesi inasikilizwa upya kwa mujibu wa Sheria na haki inatolewa. CHOMBO CHENYE MAMLAKA YA KUVUNJA NDOA KISHERIA TANZANIA NI MAHAKAMA TUU
Ila mila,bomani,dini hati hutoka serikalini kama kuhalalisha uwepo wenu kama mume na mke. Ili mmoja akizingua haswa upande wa mali serikalini husimamia mgawanyo wa mali. Tanzania haina dini ila raia wake wanaruhusiwa kuwa na imani zao tofauti tofauti.Tatizo lako umeshindwa kuelewa hiyo sheria inasimamia ndoa za kiserekali zinazo fungwa bomani.
Nifunge ndoa ya kidini, au kimila, hata bila kuarifu derikali leo, tunataka kuachana idhini mpaka waitoa wao. ndoa za kidini na kimila taratibu za kuacha zipo ndani ya dini na mila husika. Ndiyo maana hakuna alieshitskiwa kuachana na mkewe bila kupitia mahakamani.
Talaka ukitamka tu tayari hiyo,kuandika ni kumpa ushahidi kwamba kaachika,we andika tarehe na dhumuni,Ila utaratibu eda inabidi akae kwako na umuhudumie bila kummmttombba,isipokua Kama ulimkamata akifanya uchafuKwema humu,
Nisiwachoshe nimeishi na mke wangu kwenye ndoa mpaka sasa ni miaka mitano ila kutokana na changamoto za ndoa nilikuwa nahitaji tuachane kwa amani na mke wangu pasi kugombana, kwahiyo nilikuwa nahitaji kumpa talaka.
Msaada wenu taratibu za kuandika talaka upoje?
Akili ni nini!?Humu ndani watu wamedakia na kuanza kutoa ushauri wa aanzie wapi kutoa talaka? Wanamjua huyo wanayemshauri aanzie wapi process za talaka kama ana akili timamu?
Swali la kwanza alitakiwa kuulizwa ninje una akili timamu mleta mada?
Mimi nimeanzia kumchambua huyo mtaka kutoa talaka kuwa akili hana
Ageuke kungwi siyo!!?Inaonekana kama unataka kususa ndoa kutokana na maudhi flani. Vaa uanaume mdogo wangu mnyooshe huyo kiumbe we ndio kichwa
Madogo wengi huwa wanadhani haya mambo ni mepesi kama waoAgeuke kungwi siyo!!?
Ndoa hufika pahala haiwezekani Tena kuendeleaMadogo wengi huwa wanadhani haya mambo ni mepesi kama wao
Hadi hapa mimi binafsi nimekuelewa. Mungu akusaidie sana ndugu yangu.Mimi ndo mwenye shida katika ndoa, sitaki kumtesa mtoto wa watu
NDUGU WEWE OA KWA MKEKA MAHALI ELFU 20 NDOO YA MAANDAZI NDOO YA CHAI.Kwenye bibilia mahali inatakiwa ya garama gani, ili Mungu aibariki ndoa.