Utaratibu wa kutoa talaka upoje?

Utaratibu wa kutoa talaka upoje?

Upo tiyari kukaa bila kuoa tena mpendwa? Kumbuka kuachana ni machukizo kwa Mungu!

Malaki 2:16
Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
KAMA NDOA YENU ILIKUWA YENYE BARAKA ZA MUNGU BASI NA KUACHANA KWENU NI MACHUKIZO KWA MUNGU.
NDOA ZA MKE ANAYEWAJUA WANAUME WENGI, MUME ANAYEWAJUA WANAWAKE WENGI, HIZO SIO ZA KIMUNGU.HAZINA BARAKA WALA UTUKUFU KIASI HATA KUACHANA KWENU WALA SIO CHUKIZO KWANI HAZITAMBULIKI.HIVI KWANI HAO WANAOFUNGISHA NDOA, WANA UTAKATIFU GANI?

KUNA WATU WANAISHI PAMOJA LAKINI WALIISHA ACHANA MIAKA MINGI.
SHERIA ZA NDOA LAZIMA ZIBADIRIKE KWENDANA NA MABADIRIKO YA DUNIA.
 
Kah! Jamani!!

Huko kwa Mungu tutafika tukiwa tumechoka sana!

Naendelea kujifunza Kwamba sio VIZURI kufunga ndoa na kama unafunga ndoa funga uzeeni kabisaaa huna cha kupoteza!
 
Niwashauri wote waislam kwa wakristo kabla hatujaoa kwa uchache tujifunze habari za ndoa na hukmu zake kulingana na dini zetu inasaidia kidogo


Nirudi kwa mleta mada, swala la talaka hilo ni swala la kisharia(elimu) sio rahisi kama unavyozani kupata mafuhumu yake jamiiforums...sio kwamba na underrate nguvu ya social media! Hapana naelewa nafasi ya mtandao katika dunia ya sasa ila kuna baadhi ya mambo hutoyapata kihakika yake kupitia huko

Jambo likishakaa kisharia tena za dini basi huwa ni vizuri kuwaona wajuzi mkaliongea

Kwa elimu yangu nijuavyo Mimi talaka za kiislam hayo mambo ya bakwata sjui wapi hayo yamekaa kiserikali zaidi na kugawana mali labda ili vipatikane vithibitisho vitakavyotumika huko mbele ila talaka ya kiislam ukimshamtakia mkeo kuwa umemuacha iwe ni masikhara utani au serious hiyo talaka mbele ya mwenyezi imepita maadam usiwe umetokwa na akili

Msipende kuuliza maswala muhimu kienyeji jamani viongozi na wa dini na wasomi wa dini wapo kwaajili yetu humu ukiuliza masiala ya dini kumbuka hujui hata unaeamiliana nae ana elimu gani

Ila talaka pia hakikisha iwe sababu inajuzu ihofie nafsi yako isije ukawa una mdhulumu mwenzio..talaka ni halali inayomchukiza mwenyezi mungu (though this is claimed to be maudhui)

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kama una mchepuko basi huenda ndio aloleta mfaraka wa nyie kutaka kuachana.

Anataka muachane umuoe yeye.

Tafakari.

Michepuko wengi ni wachawi na washirikina.

Ni wachache sana ambao hawarogi wanaume.

Off course hata wake wa ndoa nao wapo wengi tu wachawi na washirikina sana tu.

Hasa wale ambao ni tegemezi kiuchumi.

Awe hafanyikazi rasmi kabisa au anafanya lakini kipato kidogo kama rafiki zake Mr. Mpwayungu Village.

Maana anajua ukimuacha hataweza kuishi maisha yenye hadhi mnayoishi akiwa na wewe.

Au la alenge kugawana Mali.
Hili la wake washirikina ni tatizo kubwa hasa kwa wanawake waliotoka kwenye familia zenye kuamini ushirikina. Kuna sababu nyingi za wanawake kuendea waume zao kwa waganga na moja ambayo inaniacha hoi ni yua kutaka eti mume awe chini ya masharti ya mwanamke, yaani mwanamke awe ndiye msemaji wa mwisho hasa kwenye mambo ya fedha. Pia awe na uhuru wa kutoka atakavyo na pia kuchepuka. Mimi huwa siamini kwenye ushirikina hata kidogo na nina uhakika hakuna dawa inayoweza kumpumbaza mwanaume. Nachoogopa ni kulishwa uchafu au sumu kwa sababu waganga wanatoaga maagizo ya tata sana. Mke anaweza kuambiwa aingize kipande cha nyama kwenye sehemu ya haja kubwa kilale ndani halafu kesho yake akiunge vizuri na mboga, ampe mume.
 
Habari Mkuu
Kuna vitu muhimu vya kufahamu hasa linapokuja swala la talaka kwani watu wengi hudhani talaka ni jambo la wanandoa pekee, si kweli.

1. Talaka hutolewa na Mahakama, hivyo ili kupata talaka ni lazima ukafanye maombi Mahakamani na si kila Mahakama bali itakupasa kuzingatia maelekezo ya sheria kulingana na aina ya ndoa yenu

2. Talaka hutolewa kwa kuionesha Mahakama sababu za msingi za kuifanya iamini kuwa ndoa yenu hioyo hairekebishiki tena. Fahamu kuwa Mahakama yenyewe haipendi kutoa talaka/kuvunja ndoa za wapendanao.

3. Talaka itakupa uwezo wa kutambulika kama mtu asiye ndani ya ndoa, hii ina maana kuwa kwa wakristu wataweza kuoa/kuolewa tena na kwa waislamu itahesabu ongezeko la idadi ya nafasi ya kuoa mke mwingine, kwa watamaduni vivyo hivyo pia.

4. Talaka hutolewa kwa ndoa inayotambulika kisheria na ili kuthibitisha uwepo wa hiyo ndoa ni sharti pawepo cheti cha ndoa hiyo. Hii ni kwa ndoa za aina zote, kidini, kiserikali na kimila, ni sharti ndoa iwe imesajiliwa kwa msajili wa ndoa.

5. Kabla ya kufanya maombi ya talaka Mahakamani ni sharti muwe mmeshapita kwenye usuluhishi wa ndoa, na ikashindikana kusuluhishwa hivyo mkapatiwa hati ya kushindwa kwa usuluhishi. Usuluhishi unaweza kufanywa na Baraza la kata au mabaraza ya kidini ya usuluhishi wa ndoa, ila sharti Baraza hilo liwe linatambulika kisheria.

6. Baada ya talaka kinachofuata ni mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja, hapa ni lazima ijulikane kuwa huu mgawanyo una wahusu watalaka pekee na wala hauwahusu watoto wao. Kumekuwa na mazoea na dhana kwamba mali tutawapa watoto, hii ni kinyume na sheria. Zipo kesi za Mahakama Kuu zilizopinga hili swala/mtazamo.

Mwisho kabisa, pole kwa maswahibu Mkuu, pima uzani wa unayopitia kisha tafakari vizuri kama kweli talaka ndjo suluhisho la hayo maswahibu. Ukiona ndio basi fuata utaratibu, ukikwama unaweza niuliza siku yoyote nitakupa mwanga pindi nitakapoona swali lako.

Kila la kheri.
Je, kama mume na mke akienda kwa pamoja na kusema wameamua kuachana kwa amani kwani wameona ndoa yao ina misukosuko sana?
 
Habari hizo ni nadra sana kuzisikia na ni matokeo ya wanaume wasio na akili kuoa
Mwanaume asiye na akili hatakiwi kuoa.
Kuoa kunahitaji mwanaume mwenye akili sio jinga jinga.Hayo majinga jinga ndio huua
Kwako wewe kipimo cha akili ni uwezo wa kuishi na mke, wakati vichaa tunaona wanazaa.

Akili ni kutafuta hela, Kuna mchungaji, anasema pesa, hupati kwa maombi bali, pesa hupatikana kwa jasho. Mungu huombwa kibariki jasho lako.

Nimekuonyesha pesa inavyohitaji Akili kuipata.
 
Talaka sio lazima kuandika kama ni muislam mwite majina yake matatu na umwambie kuwa kuanzia leo wew si mke wangu kisheria na Sunnah kwa mujibu wa mafunzo yenu .
 
Yaan ni muislam ndo uanzishe mpaka uzi? Wewe chana kikaratasi hata kama ni cha kufungia maandazi, andika hivi" kuanzia keo mimi na wewe basi" mpelekee

Yaan waislam mbaoana kwa ndoo moja ya maandazi, na chai ya rangi, kuachana ndo uangaike?
Nasikia hata sms moja tu mnaachana unasubiri nini?
Kwenye bibilia mahali inatakiwa ya garama gani, ili Mungu aibariki ndoa.
 
Kwema humu,

Nisiwachoshe nimeishi na mke wangu kwenye ndoa mpaka sasa ni miaka mitano ila kutokana na changamoto za ndoa nilikuwa nahitaji tuachane kwa amani na mke wangu pasi kugombana, kwahiyo nilikuwa nahitaji kumpa talaka.

Msaada wenu taratibu za kuandika talaka upoje?
Kabla ya kuleta vitu humu uwe na utaratibu wa kuomba ushauri si kila linalo kukwaza unaleta humu. Sasa subiri upewe unacho hitaji.
 
Inaonekana kama unataka kususa ndoa kutokana na maudhi flani. Vaa uanaume mdogo wangu mnyooshe huyo kiumbe we ndio kichwa
 
[emoji777] Kwa Sheria ya ndoa ya Tanzania , hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuandika Wala kutoa talaka tofauti na Mahakama baada ya kupitia taratibu zote na kubaini kuwa ndoa imevunjika vipande vipanda Haina spea na Wala haitawezekana tena kwa wanandoa hao kuishi pamoja.

[emoji736] Utaratibu, unasnzia kwa Baraza la usuluishi la Kata, pale ambapo mmoja wa wandoa ataoeleka malalamiko, basi Baraza litawaita na kuwasikiliza kwa lengo sii la kuvunja ndoa Bali kuwasuluisha maana kwa mujibu wa kifungu Cha 9 Cha Sheria ya ndoa na kesi ya Hyde vs Hyde lengo la ndoa ni wanandoa waishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe. Baraza likishindwa kusuluisha litaandika certificate kwa mahakama kuwa usuluishi umeshindikana. Hivyo hakuna kesi yoyote ya maombi ya talaka yatapikelewa mahakamani kabla ya kupitia kwenye Baraza la usuluishi linambulika kisheria. Mtu mwenye dini Fulani ambapo ndoa imefungwa kwa misingi hiyo na wanayo mabaraza ya usuluishi, mabaraza hayo yanaweza kutbulika kama mbadala wa mabaraza ya Kata.

[emoji736] Kesi ikifika mahakamani, baada ya kuwasikiliza itsona kama kweli haiwezekani wanandoa Hawa kuendelea kuishi pamoja na kabla haijatoa talaka lazima itoe muda wa kisheria wa wanandoa kujitafakari hii order ni separation ambayo ni decree nisi.

[emoji736] Baada ya muda wa separation kuisha mahakama itawasikilizs tena kama bado mambo ni magumu basi itatoa talaka na amri za matunzo ya watoto ( kama wapo) na mgawanjo wa Mali walizochuma pamoja .

[emoji777] Hivyo, kwa Sheria zetu, makatatasi wanaojiandikia watu kwa kusema mara ni talaka tatu, mara talaka rejea kimsingi Yale sii talaka na hayana effect ya kuvunja ndoa, mmoja wao akienda mahakamani kesi inasikilizwa upya kwa mujibu wa Sheria na haki inatolewa. CHOMBO CHENYE MAMLAKA YA KUVUNJA NDOA KISHERIA TANZANIA NI MAHAKAMA TUU
Tatizo lako umeshindwa kuelewa hiyo sheria inasimamia ndoa za kiserekali zinazo fungwa bomani.

Nifunge ndoa ya kidini, au kimila, hata bila kuarifu derikali leo, tunataka kuachana idhini mpaka waitoa wao. ndoa za kidini na kimila taratibu za kuacha zipo ndani ya dini na mila husika. Ndiyo maana hakuna alieshitskiwa kuachana na mkewe bila kupitia mahakamani.
 
Tatizo lako umeshindwa kuelewa hiyo sheria inasimamia ndoa za kiserekali zinazo fungwa bomani.

Nifunge ndoa ya kidini, au kimila, hata bila kuarifu derikali leo, tunataka kuachana idhini mpaka waitoa wao. ndoa za kidini na kimila taratibu za kuacha zipo ndani ya dini na mila husika. Ndiyo maana hakuna alieshitskiwa kuachana na mkewe bila kupitia mahakamani.
Ila mila,bomani,dini hati hutoka serikalini kama kuhalalisha uwepo wenu kama mume na mke. Ili mmoja akizingua haswa upande wa mali serikalini husimamia mgawanyo wa mali. Tanzania haina dini ila raia wake wanaruhusiwa kuwa na imani zao tofauti tofauti.
 
Kwema humu,

Nisiwachoshe nimeishi na mke wangu kwenye ndoa mpaka sasa ni miaka mitano ila kutokana na changamoto za ndoa nilikuwa nahitaji tuachane kwa amani na mke wangu pasi kugombana, kwahiyo nilikuwa nahitaji kumpa talaka.

Msaada wenu taratibu za kuandika talaka upoje?
Talaka ukitamka tu tayari hiyo,kuandika ni kumpa ushahidi kwamba kaachika,we andika tarehe na dhumuni,Ila utaratibu eda inabidi akae kwako na umuhudumie bila kummmttombba,isipokua Kama ulimkamata akifanya uchafu
 
Humu ndani watu wamedakia na kuanza kutoa ushauri wa aanzie wapi kutoa talaka? Wanamjua huyo wanayemshauri aanzie wapi process za talaka kama ana akili timamu?

Swali la kwanza alitakiwa kuulizwa ninje una akili timamu mleta mada?

Mimi nimeanzia kumchambua huyo mtaka kutoa talaka kuwa akili hana
Akili ni nini!?
 
Kwenye bibilia mahali inatakiwa ya garama gani, ili Mungu aibariki ndoa.
NDUGU WEWE OA KWA MKEKA MAHALI ELFU 20 NDOO YA MAANDAZI NDOO YA CHAI.

ILA MKIJA KUACHANA MSITUCHOSHE KUTOA USHAURI, MTU UNAOA GHARAMA JUMLA LAKI MOJA NA ELFU MBILI, SASA HIYO NAYO NI YA KUKUTESA.KUVUNJA NDOA? UNA MAUMIVU GANI? ULITUMIA GARAMA GANI?

HII NDO SABABU MNAACHANAGA KWA SMS YA 50
 
Back
Top Bottom