Kuna ndugu yangu amelipia kifurushi cha NHIF cha Tshs. 530,000 kwa mwaka.
Hapa karibuni amepata tatizo la maumivu ya jino. Kwa vile anaishi Oysterbay, akaamua kwenda kwenye hospitali binafsi iliyo karibu ili kupata matibabu.
Alivyofika hospitali, walimwambia kabla ya kupata matibabu inabidi aende Hospitali ya Wilaya wamwandikie rufaa ya kutibiwa katika hospitali yao!
Wote tunajua Hospitali za Wilaya zinavyokuwa na wagonjwa wengi zaidi ya uwezo wake. Kumwambia mgonjwa afunge safari hadi hospitali ya wilaya, ambayo kwa huyu ni Mwananyamala ni usumbufu ambao hauna sababu.
Kama NHIF wana makubaliano na hii hospitali binafsi, kwa nini wamsumbue mgonjwa kupoteza muda wake kwenda kutafuta rufaa?
Kama hawana imani na hospitali binafsi, kwa nini wasiweke wazi kuwa wagonjwa wao lazima watibiwe katika hospitali za serikali ili mteja aamue kama kuna sababu ya kujiunga na NHIF badala ya mifuko mingine ya Bima ya afya?
Ni vizuri NHIF wakatoa ufafanuzi kuhusu ulazima wa mgonjwa kufuata rufaa kutoka hospitali za Wilaya ambazo zimeelemewa na wagonjwa; na zinaweza kuwa mbali na eneo alilopo mgonjwa.