Utaratibu wa timu kuanzia round ya awali halafu zingine zinasubiri round ya pili ni wa hovyoo sana

Utaratibu wa timu kuanzia round ya awali halafu zingine zinasubiri round ya pili ni wa hovyoo sana

Kwenye uzi wa mleta mada kuna sehemu yeyote kasema kuwa ni ushamba CAF kutumia ubora wa miaka 7 nyuma kupima timu kwa wakati wa sasa?
Kama hajasema huoni kama mdau kawasilisha hoja yake mpya ya kwamba CAF ipo kizamani kwa kufanya ranking ya miaka 7?
Duh!
 
Ndio maana nilikwambia hauna hoja, umeishia kusoma content tu ya mleta uzi. Mwenzio nimesoma heading na content vyote kwa pamoja ndipo nikatoa majibu kutoka hoja zake mbili. Moja ilikuwa kwenye heading ( timu kuanzia raundi ya pili) na ya pili ni hilo la kuanzia nyumbani au ugenini. Usitake kulazimisha kudharauriwa na kila mtu. Sasa rudi usome heading ya mleta uzi kisha njoo useme ni takwimu gani haihusiana na kinachoongelewa.
Aisee una moyo... unapoteza muda wako kwa mpumbavu 😂😂😂
 
Favour inatokana na kufanya vizuri kwa vilabu vyao katika mashindano ya CAF ngazi ya vilabu. Mfano halisi ni Tanzania ni miongoni mwa mwanachama wa CAF, tulikuwa tunapata nafasi ya timu moja tu klabu bingwa lakini baada ya Simba kufanya vizuri kwa misimu kadhaa Tanzania ikaingia kwenye top 12.

Hivyo kwenye ranking ya CAF zipo rank za aina mbili, kuna club ranking halafu kuna association ranking. Hii association ranking huchukua jumla ya point zilizokusanywa na vilabu katika nchi husika na ndio huchukua vilabu 12 bora, nafasi ya kuingiza timu nne (mbili klabu bingwa na mbili shirikisho) Kwa Tanzania ina jumla ya point 71 hizi point 71 zimepatikana kutoka kwa vilabu vitatu
1) Simba point 39
2) Yanga point 31
3) Namungo point 1
Hivyo hizo point 71 imeifanya Tanzania kuwa ya 6 kwenye association ranking ya CAF.
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri
 
Jana nimeangalia za kina JKU, DISCIPLES, ORLANDO PIRATES, BUMAMURU, VITAL'O itajua mexhi za awali ni muhimu.

Lazima hizi mechi ziwepo ilo kutoa vibonde, zibaki timu ambazo ni serious pekee.

Timu kama Disciples vs Orlando pirates zilikuwa zinacheza ujinga kabisa.

Pyramids inacheza na upuuzi tu wa JKU, ujinga mtupu.

Unaona kabisa gap liliopo kati ya Yanga, Pyramids na hivi vitimu vya Zanzibar, Djbouti, Botwasana, Burunei
Mimi nilivyoona Orlando Pirates wanauwasha kwenye pre season nikajua watakuwa wa moto sana safari hii kwenye klabu bingwa kumbe wanajitafuta bado.
Kingine timu za Zanzibar hazijawahi kuwa serious kwenye mpira wa miguu
 
Nadhani CAF inatakiwa kufanya review katika baadhi ya mambo yake . Hii ni taswira ya kibaguzi. Pia na suala la timu kubwa kuanzia ugenini nao huu ni utaratibu wa hovyoo sana.
Lakini pia timu zitajijenga zaidi, mnanikumbusha kuhusu ubaya ubwera
 
Mimi nilivyoona Orlando Pirates wanauwasha kwenye pre season nikajua watakuwa wa moto sana safari hii kwenye klabu bingwa kumbe wanajitafuta bado.
Kingine timu za Zanzibar hazijawahi kuwa serious kwenye mpira wa miguu
Usajili serious wa Orlando ni Gilberto ambaye ni mpenda bata kinoma.
 
CAF wana mambo mengi mno ya kizamani, kama hayo kila siku timu fulani kuanzia ugenenini ni ushamba, Away goal ni ushamba, mambo ya huyu anaanza hatua ya awali huyu ya mbele ni ushamba na ushamba ukubwa zaidi wa kutumia ubora wa miaka 7 nyuma kupima timu kwa wakati wa sasa, kwa mambo haya ndio maana ni ndoto kwa africa kubeba Wedi Cap
Ubora unapimwa kwa point ulizokusanya. Hakuna short cut. Kaza mwiko huo ukusanye points.
 
Nadhani CAF inatakiwa kufanya review katika baadhi ya mambo yake . Hii ni taswira ya kibaguzi. Pia na suala la timu kubwa kuanzia ugenini nao huu ni utaratibu wa hovyoo sana.
Mashabiki wa vyura bwana!!
 
CAF wana mambo mengi mno ya kizamani, kama hayo kila siku timu fulani kuanzia ugenenini ni ushamba, Away goal ni ushamba, mambo ya huyu anaanza hatua ya awali huyu ya mbele ni ushamba na ushamba ukubwa zaidi wa kutumia ubora wa miaka 7 nyuma kupima timu kwa wakati wa sasa, kwa mambo haya ndio maana ni ndoto kwa africa kubeba Wedi Cap
Huko unakoona wana uwezo wa kubwba wedi kapu pia kuna timu zinaanzia hatua za awali na nyingine makundi, hivi unajua kuwa uefa cl ishaanza?
 
Nadhani CAF inatakiwa kufanya review katika baadhi ya mambo yake . Hii ni taswira ya kibaguzi. Pia na suala la timu kubwa kuanzia ugenini nao huu ni utaratibu wa hovyoo sana.
Unakwama wapi aseee.... Saizi EUFACL, EUFAEL na EUFACF vinaendelea kwa hatua za awali kama ilivyo mashindano ya CAFCL na CAFCC nayo yapo hatua za awali.

Na siyo ubaguzi unafanyika, bali ni ubora wa timu ndo unaamua uanzie kwenye hatua ipi.

Na ubora wa timu unatakiwa uwe wa kipindi kisicho pungua muda fulani mfano ndani ya misimu mitano iliyopita umejikusanyia point ngapi.

HAKUNA UBAGUZI HAPO MSIPENDE KULIALIA TIMU HAZIJATENGEZA UBORA KWA MSIMU MMOJA AU MIWILI ENDELENI KUPAMBANA MTAFIKA WALIPO WALE MNAOWAONEA WIVU.
 
Hahah. Natumaini hii post yako ni joke unamkejeli mleta mada. Sitaki kuamini upo siriasi
huo ndio ukweli jamaa kaandika,
humu ndani inaonekana watu kumbe hawaelewi jinsi mashindano ya vilabu duniani yanavyoendeshwa?

hata UEFA kuna timu zinaanzia round za chini na zingine unazikuta makundi
 
CAF wana mambo mengi mno ya kizamani, kama hayo kila siku timu fulani kuanzia ugenenini ni ushamba, Away goal ni ushamba, mambo ya huyu anaanza hatua ya awali huyu ya mbele ni ushamba na ushamba ukubwa zaidi wa kutumia ubora wa miaka 7 nyuma kupima timu kwa wakati wa sasa, kwa mambo haya ndio maana ni ndoto kwa africa kubeba Wedi Cap
Mbona hata Europe ni hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom