Utaratibu wa tozo za maegesho ya gari

Utaratibu wa tozo za maegesho ya gari

Scaramanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2020
Posts
490
Reaction score
704
Utaratibu huu mpya hasa jiji la Dar es salaam kuhusu tozo za maegesho ya gari wahusika wautizame upya.Sipingi kuhusu toz hii bali utaratibu siyo mzuri na unaleta urasimu au usumbufu kwa watumiaji wa magari pale wanapoegesha.

Sasa hivi ukiegesha gari waliopewa jukumu kusimamia wana scan na kukupa risiti ambayo unatakiwa ulipie kwa njia ya simu au uende kwa kwa wakal ukalipe.

Kweli mia 500 mtu uanze tafuta wakala na siyo kila mtu anaweka pesa mpesa au tigopesa. Kwanini wasingefanya utaratibu kama kuwepo na kadi maalum unajaza humo kifurushi chako ukifika wakati wa kulipia mtozaji anakuwa na mashine unaweka kadi yako na password biashara inakwisha .

Fikiria wazee ambao hata mpesa hawajui yaani kweli kubudi njia rahisi ya kuondoa usumbufu. Mbona airport au mlimani city hamna tatizo kuna vibanda unaenda lipia tu.

Sasa karisiti kakipotea imekula kwako maana utakutana na adhabu ambazo hazikuwa na msingi wowote kama njia ya ulipaji ingekuwa ni rahisi na rafiki kuliko ilivyo sasa.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Wabongo hamnaga jema. Mmerahisishiwa malipo bado mnalalama.
 
Bladfaken, sitapaki gari yangu kwenye hayo maeneo yao......hizo parking zenyewe hazijajengwa rasmi kama maeneo ya parking ni mwendo wa kutafuta tozo kila pahala.
 
Tozo ya parking ni wizi mtupu kwann tulipie parking hali Hakuna unachonufaika nacho Hakuna cha ulinzi wa kuoshewa gari.
Wizi mtupu.Nini lengo la parking
 
Utaratibu huu mpya hasa jiji la Dar es salaam kuhusu tozo za maegesho ya gari wahusika wautizame upya.Sipingi kuhusu toz hii bali utaratibu siyo mzuri na unaleta urasimu au usumbufu kwa watumiaji wa magari pale wanapoegesha.Sasa hivi ukiegesha gari waliopewa jukumu kusimamia wana scan na kukupa risiti ambayo unatakiwa ulipie kwa njia ya simu au uende kwa kwa wakal ukalipe. Kweli mia 500 mtu uanze tafuta wakala na siyo kila mtu anaweka pesa mpesa au tigopesa. Kwanini wasingefanya utaratibu kama kuwepo na kadi maalum unajaza humo kifurushi chako ukifika wakati wa kulipia mtozaji anakuwa na mashine unaweka kadi yako na password biashara inakwisha .Fikiria wazee ambao hata mpesa hawajui yaani kweli kubudi njia rahisi ya kuondoa usumbufu. Mbona airport au mlimani city hamna tatizo kuna vibanda unaenda lipia tu.Sasa karisiti kakipotea imekula kwako maana utakutana na adhabu ambazo hazikuwa na msingi wowote kama njia ya ulipaji ingekuwa ni rahisi na rafiki kuliko ilivyo sasa.
Utaratibu mbovu mno na hasa kwa hiyo njia walio ichagua ya malipo kwa njia ya simu, mfumo ambao umeleta makasiriko na machukizo kwa watumiaji almost wote. Bill ya 500 mwenye malipo unalipa 500+200 =700 huu ni upuuzi wa kiwango cha lami.
 
Na sijui hata unavyofanya kazi, kwamba usipolipa baada ya siku 7, faini inakuaje? Na kama sikupewa risiti, mimi sio wa kupaki maeneo ya hivyo hata miezi miwili, nianze kufunga safari kumtafuta mwenye mashine anichekie kama gari inadaiwa?
 
Sawa kulipia parking ....

Ila serikali,halmashauri wangeweka sehemu zote alama kuonyesha kuwa ni parking ya kulipia
Lakini kwa style hii kidogo inaleta sintofahamu

Ova
 
Utajikuta umekamatwa na trafiki unadaiwa faini ya parking 300,000/-
 
Sawa kulipia parking ....

Ila serikali,halmashauri wangeweka sehemu zote alama kuonyesha kuwa ni parking ya kulipia
Lakini kwa style hii kidogo inaleta sintofahamu

Ova
tena hapa ndiyo changamoto ingine unakuta unaingia kanisani unatoka unakuta risiti na ukiangalia hamna kibao chocote cha kuonyesha kuwa eneo hilo ni parking au siyo parking na kama ni parking unatakiwa lipia. kanisani kwetu hapa sinza KKKT kila juammosi na jumapili wanakuja watoza parking tena ni njia ya vumbi tunapaki nje kwa shida sana lakini tunatozwa
 
Utajikuta umekamatwa na trafiki unadaiwa faini ya parking 300,000/-
Ikitokea hala kama hii mwenye chombo cha moto ni wapi anaweza peleka malalamiko yake au shauri lake kupinga hiyo fine ?
 
Sawa kulipia parking ....

Ila serikali,halmashauri wangeweka sehemu zote alama kuonyesha kuwa ni parking ya kulipia
Lakini kwa style hii kidogo inaleta sintofahamu

Ova
Wanapenda kuvuna wasichopanda.
Kweli kabisa waweke sehemu zote alama ioneshe ,ili mtu ajue parking ya kulipia

Ova
 
tena hapa ndiyo changamoto ingine unakuta unaingia kanisani unatoka unakuta risiti na ukiangalia hamna kibao chocote cha kuonyesha kuwa eneo hilo ni parking au siyo parking na kama ni parking unatakiwa lipia. kanisani kwetu hapa sinza KKKT kila juammosi na jumapili wanakuja watoza parking tena ni njia ya vumbi tunapaki nje kwa shida sana lakini tunatozwa
Huu ni sawa na uhuni mkuu
Kuna wakati walikuwa wanakuja mpaka
Masokoni wakiona watu wameegesha
Magari wanawabandikia risiti
Hakuna sign wala nini

Ova
 
Utajikuta umekamatwa na trafiki unadaiwa faini ya parking 300,000/-
Na naingia kwenye mtandao kama walivyoelekeza, tangu asubuhi mpaka sasa nasubiri meseji ya kujibiwa!
 
Back
Top Bottom