Utaratibu wa wafiwa kuwalisha waombolezaji wengine umerasimishwa Tanzania?

Utaratibu wa wafiwa kuwalisha waombolezaji wengine umerasimishwa Tanzania?

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Habari za leo wanajamvi? bila shaka mapambano yanaendelea kama kawaida!
Tuendelee kupambana sana na kusaka michuzi kwa udi na uvumba kana kwamba hatufi, na tuendelee kumuomba na kumwabudu Mungu kana kwamba tunakufa kesho!

Kwanza kabisa napenda kutoa masikitiko yangu kama mwananzengo kwa sintofahamu ambayo imeendelea kuikumba jamii ya kitanzania kwa sehemu kubwa kama si yote.

UMUGHAKA nimekuwa nikijiuliza huu utaratibu wa kipumbavu ni nani/akina nani waliyo urasimisha? Kumekuwa na kasumba ambayo sidhani kama nikiita ni upumbavu/ushenzi kama nitakuwa nakosea.

Misiba mingi kama si yote niliyowahi kuhudhuria, nimekua nikiona utaratibu wa wale waliofikwa na msiba ndiyo ambao wanahaha kuwalisha watu ambao wamekuja msibani kutoa pole/kufariji.

Na lazima niwe mkweli ya kwamba,hata sisi kwetu pia tumepata misiba mingi tu ya ndugu zangu na utaratibu huwa ni huo huo!,hili suala limekaaje wapendwa? Yaani unakuta waliofikwa na msiba ndiyo wanaumiza vichwa namna ya kuwalisha wanaokuja kuwafariji badala ya waliokuja kuwafariji wenye matatizo wao ndiyo ilipaswa wakae wakusanyane wananzengo ili kuwalisha waliofikwa na msiba!

Huu utaratibu ni mbovu sana na siungi mkono kabisa! Ni kwanini tusiwe na utaratibu tunapoenda misibani kuwafariji wafiwa kusiwe na utaratibu wa kuwalisha wafiwa pamoja na watakao hudhuria msibani? Yaani unakutwa watu wengi wanaoenda misibani ni kupiga soga tu na kusubiri kunawishwa wakati wa kula huku wanafurahia maisha kana kwamba ni sherehe.

Watu wengi wanaenda misibani si kufariji bali kupiga soga na kula!,huu ndiyo ukweli ukubali au ukatae!

Yaani mtu amefiwa na mpendwa wake halafu bado aumize na kichwa namna ya kuwalisha wananzengo!,hii kitu iko sawa kweli?,hivi hizi nguvu unadhani atakuwa nazo?,hii imepelekea hasa watu wenye kipato cha chini wanabaki kusimangwa na wananzengo hata bila aibu!,unakuta kabisa majirani wanaongea " Msiba wenyewe hata vyakula hauna,naona watu wamechungulia tu wamesusa",kabisa?

Lakini misiba ya watu wenye uwezo utasikia "Jamaa wanapika vyakula vizuri asikwambie mtu,unakula mpaka unasaza".

Hata kama mfiwa anao uwezo,ndiyo alishe wananzengo badala ya wananzengo kumlisha yeye?.

JE,huu utaratibu ni nani aliyeuanzisha?

Je,makabila yote ya Tanzania hufanya hivi?

Wenzetu mliotembea tembea huko ughaibuni,je hali huwa iko hivi kama huku kwetu.

Unakuta "Mijitu" inaenda misibani kwa ajili ya kula tu,ikishakula hiyoooooo inalala mbele!,hata aibu haioni!,unakuta jitu badala liende hata ndani kusalimia wafiwa lenyewe linakomea getini linapiga msosi halafu linalala mbele!!

HUU UTARATIBU HAUKUBALIKI

#USIPOBADILIKATUTAKUBADILISHA
#TIGHABHATEMWE
 
Binadamu tumeumbiwa shida ambazo inabidi tukabiliane nazo, na msiba nao ni sherehe ambayo inaambatana na majonzi ndani yake.
Je ni jukumu la nani kulisha wanaouzulia msiba ?
Kumbuka wafiwa wanapewa rambi rambi, pia watu hufika na vyakula mbali mbali , sukari, chumvi, mafuta , blanket na vingine vingi tu kwa ajili ya wafiwa ,
Je wageni utawatoa na njaa, wachimbaji utawatoa na njaa, unajikuta uwezi watoa na njaa inabidi uwapikie baada ya kukufanyia shughuli mbali mbali hapo kwako.
Na siku izi ugali hatutaki tunataka wali.
Ukiona unawachukia wanao kula msibani ujue wewe ni mnyimi
 
Na lazima niwe mkweli ya kwamba,hata sisi kwetu pia tumepata misiba mingi tu ya ndugu zangu na utaratibu huwa ni huo huo!,hili suala limekaaje wapendwa?,yaani unakuta waliofikwa na msiba ndiyo wanaumiza vichwa namna ya kuwalisha wanaokuja kuwafariji badala ya waliokuja kuwafariji wenye matatizo wao ndiyo ilipaswa wakae wakusanyane wananzengo ili kuwalisha waliofikwa na msiba!.
Dah nimecheka utadhani mazuri, yaani mnakua hamlali. Mnachangishana Hadi kukopa kisa kuwalisha Watu wanaokuja kuwafariji! Si heri ukodi Watu wa kukufariji ujue Moja, msiba ukiisha unalipa invoice maisha yanaendelea
 
Binadamu tumeumbiwa shida ambazo inabidi tukabiliane nazo, na msiba nao ni sherehe ambayo inaambatana na majonzi ndani yake.
Je ni jukumu la nani kulisha wanaouzulia msiba ?
Kumbuka wafiwa wanapewa rambi rambi, pia watu hufika na vyakula mbali mbali , sukari, chumvi, mafuta , blanket na vingine vingi tu kwa ajili ya wafiwa ,
Je wageni utawatoa na njaa, wachimbaji utawatoa na njaa, unajikuta uwezi watoa na njaa inabidi uwapikie baada ya kukufanyia shughuli mbali mbali hapo kwako.
Na siku izi ugali hatutaki tunataka wali.
Ukiona unawachukia wanao kula msibani ujue wewe ni mnyimi
Mkuu siyo kwamba ni mnyimi,ishu hapo ni wao kuleta vyakula au kutoa michango itakayonunua hivyo vyakula,kumbuka siwezi kufiwa na bado nilishe lundo la wananzengo wakati huohuo bajeti ya msiba ikiwa juu ya wafiwa!

Tubadilike
 
Asikwambie mtu mkuu,misiba inawaacha wafiwa na madeni makubwa mno kisa kuwalisha waliopaswa kuwalisha wafiwa!!
 
Mkuu siyo kwamba ni mnyimi,ishu hapo ni wao kuleta vyakula au kutoa michango itakayonunua hivyo vyakula,kumbuka siwezi kufiwa na bado nilishe lundo la wananzengo wakati huohuo bajeti ya msiba ikiwa juu ya wafiwa!

Tubadilike
Ndo Mana tunapitisha mchango
 
Mkuu michango huwa kuna muda haitoshi kwasababu watu walisha jiaminisha ya kwamba anayepaswa kuwalisha ni aliyefikwa na msiba
Usipowalisha ndio utajua wamekuja zika au kula. Yaani ni lawama Kila sehemu. Jamaa alifanya kusudi akawalisha wali Chinese na ana uwezo mkubwa wa kupika nyama, hawakumchelewesha walimfuata na kumpaka pale pale kabla ya maziko, ilibidi wengine tuangue kicheko huku pembeni wanalalamika siku nyingine akitulisha majani kama mbuzi hatuji tena
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]wananzengo jau sana
 
Utakuta mtu anakuja msibani na rambirambi ya buku lakina anataka buffet ya kuku na mazagazaga mengine.
Misiba inatumika kama sehemu ya kubadilisha diet.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Binadamu tumeumbiwa shida ambazo inabidi tukabiliane nazo, na msiba nao ni sherehe ambayo inaambatana na majonzi ndani yake.
Je ni jukumu la nani kulisha wanaouzulia msiba ?
Kumbuka wafiwa wanapewa rambi rambi, pia watu hufika na vyakula mbali mbali , sukari, chumvi, mafuta , blanket na vingine vingi tu kwa ajili ya wafiwa ,
Je wageni utawatoa na njaa, wachimbaji utawatoa na njaa, unajikuta uwezi watoa na njaa inabidi uwapikie baada ya kukufanyia shughuli mbali mbali hapo kwako.
Na siku izi ugali hatutaki tunataka wali.
Ukiona unawachukia wanao kula msibani ujue wewe ni mnyimi
Mjomba nimekupa like [emoji23]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom