Utaratibu wa Waziri wa Ardhi wa kudhalilisha wawekezaji umepitwa na wakati. Akumbuke hii awamu ya 6

Utaratibu wa Waziri wa Ardhi wa kudhalilisha wawekezaji umepitwa na wakati. Akumbuke hii awamu ya 6

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Leo Waziri Wa Ardhi alimwita mwekezaji Bagamoyo na kumdhalalisha mbele ya Wananchi.Inawezekana huyu mwekezaji ni mkosaji lakini utaratibu huu umekufa katika awamu hii ya 6.

Utaratibu huu ni kutaka kuzijolea sifa tu,kwani angewaeleza wananchi kuwa suala la mwekezaji na watendaji wake analishughulikia na watapata majibu yao hata siku ya 2,kungetokea nini?Kwa taarifa waziri ajue Watanzania ni wavumilivu,wapenda amani,wastaarabu sana sana.Shida zao sio kudhalilisha binadamu wenzetu bali kupata haki zao.

Inaelekea waziri huyu wa Ardhi ana jazba zake.Utawala wa awamu ya 6 ni kuvutia wawekezaji kwa wingi ili maisha ya wananchi hasa masikini yaboreke.

Huku ni kuwafukuza wawekezaji.Kama wana makosa kama huyu wa bagamoyo,aitwe ,wakae naye na maofisa wa wizara yake kama kuna uamuzi wachukue kwa manufaa ya wananchi.Ustaarabu ni utamaduni wa watanzania.Hii awamu ya 6 inaheshimu haki za wananchi wote masikini na matajiri,wawekezaji na wananchi wa kawaida.

Pia awamu ya 6 inaheshimu mihimili 3, yaani serikali, bunge na mahakama. Kwa ninavyojua mimi huyu mwekezaji akienda mahakamani kwa kudhalilishwa kipi kitatokea?

Wananchi wanataka na wanapenda sana kupata haki zao kwa ustaarabu ndio maana awamu ya 6 inapenda sana kuwasikiliza kwa upendo sio kwa kitendo cha waziri huyu.Kinatotuangusha watanzania ni hawa mawaziri kutakabsifa kwa wananchi kwa staili aliyoitumia waziri wa ardhi.

Kwani muda wote wananchi wananyanyasika alikuwa wapi? Hafai huyu.
 
Back
Top Bottom