linkoln1888
Member
- Jul 9, 2021
- 21
- 15
Sekretariate ya ajira katika Utumishi wa umma inatangaza kazi kwa niaba ya taasisi/shirika la umma kuhitajika mtu mwenye elimu ya kidato cha Nne na cheti cha taaluma fulani tu, halafu kwenye usaili wanaweka mtu mwenye elimu ya Degree na ziada ya ngazi ya cheti alichokipata baada ya kuhitimu degree, naye akafanya usaili pamoja na wenye elimu za kidato cha Nne na Vyeti vya taaluma husika, na baada ya usaili, yule mwenye degree na ziada ya elimu ngazi ya cheti ndiye akapangiwa kazi kuwa ndiye aliyefaulu.
Swali langu
1. Je, walifanya haki kuweka mwenye elimu yake ya juu Degree kwa kazi iliyokuwa mahsusi kwa mtu wa ngazi ya cheti?
2. Je, walijua au mwombaji alificha taarifa za elimu zake wakati wa kuomba kazi?
3. Kama ni kosa la mwombaji, anawajibikaje?
4. Je, linaleta picha gani kwenye uwazi na haki kwa waombaji kazi?
5. Je, mtumishi huyo atakuwa na ufanisi kufanya kazi ya mwenye elimu ngazi ya cheti, ili hali yeye ana degree?
6. Kwa wataalamu wa Uchumi rasilimali watu, hali hii inaleta tija