Recategorization ni kwa wale waliojiendeleza ndani ya utumishi kwenye fani tofauti na aliyoajiriwa nayo. Kinachoongelewa hapa ni suala la mtu mwenye degree na ziada ya certificate kutumia elimu ngazi ya cheti alichokipata baada ya kumaliza degree ili kuomba kazi inayotaka mtu mwenye Elimu ya Kidato cha NNE na cheti cha astashahada.
Mfano, mm nilimaliza degree mwaka 2016 kisha mwaka 2017 nikasoma kakozi fulani kwa ngazi ya astashahada, baada ya hapo nikaona kazi inayotaka mwenye Kidato cha NNE na Ngazi ya cheti kwenye fani fulani, basi nikafuta taarifa zangu za elimu ya Degree na kuacha tu ile ya Certificate na Kidato cha NNE, kisha kwa njia hiyo nikawashinda wale wa certificate kwenye usaili nikapata kazi, Je, nikipeleka cheti changu cha Degree nikiripoti kazini, cheti hicho cha degree kitachukuliwa kama matokeo ya kujiendeleza kieleimu kwenye utumishi au kitachukuliwaje?