Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Hali ya usalama inazidi kuwa tete huko Tehran, Iran baada ya serikali ya nchi hiyo kuanza uchunguzi wa maafisa wake wa usalama kuhusu kuhusika kutoa usaidizi kwa Israel katika njama za mauaji ya kiongozi mkuu wa Hamas wiki hii.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya uhakika inaonyesha namna gani mauaji hayo yaliweza kutekelezwa ipasavyo katika ardhi ya Iran, maeneo yenye usalama wa hali ya juu mnoo ambapo kiongozi mkuu wa Hamas alikuwepo.
Hali ya kutokuaminiana baina ya maafisa usalama ndani ya Iran inazidi kuongezeka huku ikidhaniwa kuwa maafisa wa kitengo cha kijasusi wa Israel (Mosad) huenda walishajipenyeza ndani ya mamlaka za usalama za Iran tangu kitambo.
Wachambuzi wengi wanaamini huenda mpango wa mauaji ulisukwa kikamilifu na Marekani kuliko Israel na sababu zikielezwa kuwa ni mpango wa muda mrefu wa Marekani kuisambaratisha Iran kwa kutengeneza na kuzusha migogoro ya ndani kwa ndani ya Iran huku ikiichonganisha Iran na mataifa mbalimbali.