Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umesoma vizuri maelezo yake yote? Hiyo remotely guided missile umesoma?Uchunguzi rasm umeenda kinyume na maelezo yako!View attachment 3060549
Kuna mtu huko amewashtukia IranHali ya usalama inazidi kuwa tete huko Tehran, Iran baada ya serikali ya nchi hiyo kuanza uchunguzi wa maafisa wake wa usalama kuhusu kuhusika kutoa usaidizi kwa Israel katika njama za mauaji ya kiongozi mkuu wa Hamas wiki hii.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya uhakika inaonyesha namna gani mauaji hayo yaliweza kutekelezwa ipasavyo katika ardhi ya Iran, maeneo yenye usalama wa hali ya juu mnoo ambapo kiongozi mkuu wa Hamas alikuwepo.
Hali ya kutokuaminiana baina ya maafisa usalama ndani ya Iran inazidi kuongezeka huku ikidhaniwa kuwa maafisa wa kitengo cha kijasusi wa Israel (Mosad) huenda walishajipenyeza ndani ya mamlaka za usalama za Iran tangu kitambo.
Wachambuzi wengi wanaamini huenda mpango wa mauaji ulisukwa kikamilifu na Marekani kuliko Israel na sababu zikielezwa kuwa ni mpango wa muda mrefu wa Marekani kuisambaratisha Iran kwa kutengeneza na kuzusha migogoro ya ndani kwa ndani ya Iran huku ikiichonganisha Iran na mataifa mbalimbali.
Israel imeleta maumivu makali kwa walamba viatu vya Ayatollah nawaza vile watauwana kiasi chakuisambaratisha serikali yenyewe namuonea huruma Rais wa Taifa Hilo ambaye alikuwa na sera ya mapatano japo imegeuka shubiri. Nidhahiri shahiri Iran uwenda ikasambaratika Russian wakiona mwisho wataifa lao huku kiduku akichungulia kaburi ktk umri mdogo. Nadhani kwa sasa Putin anaona uwezo wakijasusi wa Marekani ni wa level yahatari kuwahi kifikiwa. Putin hakujuwa kile kitatokea. Siku chache baada yakukutana na kiduku hali yake imekuwa mbaya zaidi kiasi anajuta kukutana na kiduku gari alilotoa kama Zawadi tayari linashukiwa kuwa na sumu yaani nihatari huku Mchina akimuonya kidugu akae mbali na Putin back channel akapuuza. 😭Kazi ya kumuua Haniyeh haiihusu Marekani, ni kazi ya Israel. Suala la Israeel kupenya kwenye idara za usalama za Iran sio geni na ni endelevu ingawa adhabu yake ni kali sana.
Hata hivyo ni kawaida ya Israel kuwachonganisha maafisa wa Iran ili kuwakwamisha kwenye kazi zao. Unakuta mtu ambaye hausiki kabisa anatengenezewa mazingira ya kuhusika, mwshowe ufanisi unashuka au anahukumiwa mtu kwa visingizio. Au mtu anatiliwa wasiwasi hata vyeo hapandi tena na kazi muhimu hapewi.
Jambo lililo wazi ni kwamba Haniyeh kauwawa na mlipuko kwenye nyumba aliyofikia. Ushahidi wa picha za satellite unaonyesha blast damage ndogo kwenye floor ya kwanza ya nyumba ile kuashiria mlipuko kutoka ndani. Nadharia ni mbili, ni bomu la kutegwa ndani, au ni version ya guided missile maana nyumba iko almost 2km kutoka kwenye vilima ambapo mtu anaweza jificha aka-guide wired au radio controlled missile.
Nadharia ya kwanza ndio more likely na ndio vyanzo ndani ya Israel vinataja. Hivyo walioingiza bomu ndani ni Iranians kwa maelekezo ya Mossad, ni kina nani hapo ndio pagumu. Na Israel ilijuaje atakuwa nyumba ile napo sio suala la watumishi wa ile nyumba, kwanza unakuta walipanda bomu likiwa kwenye mfumo wa friji hapo upambane na watu wa logistics na procurement. Na nyumba kama hizo watumishi wake ni level za chini za usalama wanaambiwa andaa mazingira kuna ugeni hawajui mgeni ni nani mpaka afike. Kule juu wanaopanga mipango mgeni afike ndio wanajua atafika wapi na ukute sio nyumba moja tu angeweza fikia. Sasa mkanganyiko unasababisha wakamatwe watu wengi humo wasiohusika.