Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 3, 2021 jijini Dodoma, Job Ndugai amesema katika hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni hakukuwa na jambo la kukashifu wala kudharau juhudi za Serikali ila alikuwa anasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.
Bwana Ndugai amesema mwishoni mwa mwaka uliopita alikuwa mgonjwa sana hivyo hakuweza kuwa katika nafasi ya kujitetea kwa kile kilichokuwa kinasambaa mtandaoni.
"Hali yangu ya kiafya ilikuwa si nzuri mpaka sasa mnashuhudia sauti yangu ila nataka kuweka sawa kuwa tarehe 26, mwezi Desemba nilialikwa na kikundi kimoja cha watu wa dodoma, wanaoangazia maisha ya wenyeji, kikundi hicho lengo ni ushikamano na kujenga makumbusho ya utamaduni wa watu.
Na hakukuwa kukashifu, Hapakuwa na lolote la kukashifu au kudharau juhudi zozote za serikali, katika mazungumzo yetu zaidi nilisisitiza umuhimu wa tozo na kodi."
Aliongeza kusema kuwa kama kuna mtu angeona video nzima ya kile alichozungumza, hakuna migongano ambayo ingeweza kutokea;
"Katika mazungumzo yale, baadhi ya watu wakakatakata clip ya video, wakawasilisha ujumbe nusu, ujumbe nusu ule umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, ambao mjadala umesababisha usumbufu wa hapa na pale" amesema Ndugai na kuongeza
"Hapakuwa na lolote la kukashifu wala kudharau juhudi zozote za Serikali, tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono.
Katika mazunguzo hayo ambayo yalienda na video hiyo fupi, ninakiri kuwa mitandao ina nguvu sana na ina uwezo wa kutengeneza agenda.
Binafsi nimeumia sana kwa kauli yangu kuonekana kuwa ninapinga mkopo, mimi binafsi nina ushuhuda wa fedha hizo kutumika kujenga shule nzuri ya kiwango katika jimbo langu.
Je, Ndugai na Samia walisema nini?
Ifahamike chanzo cha mjadala huu ni mkopo uliopokewa na serikali kutoka Shirika la Fedha Duniani (IFM) wa shilingi trilioni 1.3 ambazo zimeelekezwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, vituo vya afya na huduma nyinginezo.
Akizungumza katika Mkutano wa pili wa wana kikundi cha Mikalile Ye Wanyausi wa jamii ya Wagogo jijini Dodoma, Desemba 27, 2021, Job Ndugai alimlenga moja kwa moja Rais Samia kwa kusema, "Juzi mama ameenda kukopa shilingi trilioni 1.3.
Hivi ipi bora, sisi Watanzania kwa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa tuwe na madeni au tubanane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe na kwa namna gani?
Tutembeze bakuli ndio heshima? Tukishakopa tunapiga makofi, sisi wa kukopa kila siku? Tukasema pitisha tozo anayetaka asiyetaka, pitisha tozo lazima tuanze kujenga wenyewe, nani atatufanyia,yuko wapi huyo mjomba, tukapitisha.
Sasa 2025 mtaamua mkitoa waliopo sawa, waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa, endapo hiyo nayo ni namna ya kuongoza nchi, hivi sasa deni letu ni Trilioni 70. Hivi ninyi wasomi hiyo ni afya kwa taifa? Kuna siku nchi itapigwa mnada hii,"
Rais Samia alijibu mapigo wakati wa hafla ya utiaji sahihi mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu cha Makutupora (Manyoni mkoani Singida) hadi Tabora kwa kusisitiza serikali itakopa kugharamia miradi ya maendeleo. Hafla hiyo iliofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 28, 2021.
"Kwa njia yoyote, kwa vyovyote tutakopa. Tutaangalia njia rahisi, njia zitakazotufaa kukopa na fedha hizi hatutazitoa kwenye kodi tunazokusanya ndani, ni lazima tutakopa.
Kama walidhani kutakuwa kuna kusimamishwa miradi ili wapate la kusema, halipo. Kuna jitihada za kutuvunja moyo kwenye mkopo, hakuna nchi isiyokopa, tutakopa tumalize miradi ya maendeleo ili tuendelee kwa sababu ukikopa unajenga sasa kwa haraka na kuharakisha maendeleo na mikopo hii ni ya miaka 20 kwahiyo tutakopa na tutalipa taratibu," alisema Rais Samia