Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama


Wakuuu Kama Jason hatajitokeza hadi Ijumaaa.....tuanze kuwa na mashaka kuwa huyu ndie Mpiganaji Peter Tyenyi.........
katika hali ya kawaida huyu jamaa Angesha update ziara ya Rais Singapore inayoanza Kesho......

Naomba wote tuendelee kumfuatilia isije Ikawa tumepoteza member.....

Still.....searching .......>>>>>>>>>>>

Wenye taarifa Zaidi waziwekee.....ili Kama yupo ajitokeze...

What a coincidence jamaa alipotea na kufa Muda unaoendana na wa huyu jamaa kuonekana hapa..????
Imeishia wapi? Huyu Jason Bourne mlimpata au ndo ntoleee
 
Ni Mtu MJINGA tu ndiye anaweza kuua kwa njia hiyo halafu akajindanganya ameficha ushahidi. Kujua hilo kwa kufanya post motern ni rahisi sana hata kwa MD 4.

Mtu aliyekufa kwa kutumbukia kwenye maji ukimfanyia post moterm mapafu yake yanakuwa yamejaa maji.

Mtu aliyeuawa (akiwa hayuko majini) halafu akatumbukizwa majini (kisima) baada ya kuuawa mapafu yake yanakuwa hayana maji.
Na hii ni sababu tu Marehemu hawezi kuvuta hewa tena umenikumbusha mbali sana kwenye forensic pathology 🙏
 
Kwa waliomkosa kosa lisu naamini watakuwa wameuwawa kwa kulinda Siri na Kama wameuwawa basi innallilah waainailah rjiuun kwakuwa shamba ni la bwana heri na
kwakuwa mbuzi ni wa bwana heri
basi mambo yote ni heri
Sitaki kuamini ile Albadir iliyosomwa Tanga imewaacha hai hadi leo najua watakuwa wametangulia mbele za haki wakiugua kuanzia unyayo hadi unywele wa mwisho utosini.
 
Unaweza kuhisi kuwa akina Ighondu wamemu-Ighondu afisa mwenzao. Kwa jinsi wanavyoshutumiwa kwa utesaji na hizi skandali za afisa mwenzao kufa kiutatanishi hii idara inahitaji mabadiliko makubwa. Sidhani kama watu watashawishika kufanya kazi huko, labda kwa sababu ya njaa tu
Hivi ighondu ndio huyu mbunge.mpya?
 
HIVI NDIVYO AFISA USALAMA WA TAIFA ALIVYOUWAWA KIKATILI NA KUZAMISHWA NDANI YA KISIMA CHA MAJI HUKO KIJITONYAMA...!!



Tuesday, June 4, 2013 | 12:18 PM







AFISA Usalama wa Taifa, Peter Patrick Tyenyi ,53, ambaye maiti yake ilikutwa Mei 27, mwaka huu katika kisima cha maji masafi kilichopo maeneo ya ofisini kwao, Kijitonyama Makumbusho jijini Dar, kifo chake kimetajwa kuwa ni cha kimafia.

Chanzo chetu makini ndani ya familia ya marehemu kimedai kuwa wao wanaamini kuwa ndugu yao hakufa kifo cha kawaida isipokuwa kuna mkono wa mtu.
Wanafamilia hao wanadai kuwa kifo hicho ni cha kimafia kwa sababu kisima kilichokutwa mwili huwa siyo rahisi mtu kuingia bila kuonekana.
Habari zinasema siku hiyo ya kutoweka kwake, asubuhi afisa huyo alitoka nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama akiwa na afya njema.


umafia.jpg


Kiliendelea kusema kwamba mara baada ya afisa huyo kufika ofisini, walikaa kikao cha kazini na mara baada ya kumalizika hakuonekana tena.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ofisa huyo alitafutwa kwa njia ya simu baada ya kutoonekana ofisini kwa saa kadhaa lakini zote zikawa hazipatikani.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyakazi wenzake waliingiwa na hofu kwa vile haikuwa kawaida yake kuondoka ofisini bila kuaga na hakuwa na tabia ya kuzima simu zake zote.
Habari zaidi zinaeleza kuwa kutoonekana kwa marehemu kwa saa kadhaa, kuliwafanya ndugu zake wapigiwe simu na maofisa wa idara ya usalama wa taifa kuulizwa na ikabidi wafike ofisini kwake ili kupata taarifa kamili.


UMAFIA3.jpg




Inasemekana kuwa mara baada ya ndugu hao kupewa taarifa hizo waliingiwa hofu, hali iliyowafanya waanze kutembelea baadhi ya hospitali za hapa Dar lakini hawakufanikiwa kupata taarifa zozote kuhusu ndugu yao huyo.
Wakati ndugu zake wanaendelea kumtafuta kwa siku za Jumanne na Jumatano, zikapatikana taarifa kuwa kuna mwili umeonekana katika kisima cha maji masafi kilichopo maeneo ya ofisini kwake.
Imedaiwa kuwa siku ya Alhamisi ambayo mwili ulionekana, maji yalikuwa yamekatika na mmoja wa wafanyakazi wa idara hiyo alikwenda kwenye kisima hicho ndipo alipouona mwili na kutoa taarifa kwa uongozi.


UMAFIA4.jpg




Imeelezwa kuwa baada ya uongozi kupata taarifa hizo, walienda kushuhudia na kuutambua kuwa ni wa Tyenyi.
Mwili huo ulikutwa ukiwa umeharibika na ulichukuliwa hadi Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania, Lugalo.
"Ndugu wa marehemu ilibidi wapewe taarifa ambapo walifika alipokua akifanyia kazi kisha kwenda Lugalo na kuutambua mwili," kilisema chanzo hicho.
Mwili huo ulifanyiwa uchunguzi (post mortem) na wanandugu waliruhusiwa kuuchukua tayari kwa mazishi.
Muda wote kabla mwili haujasafirishwa kwenda Musoma kwa mazishi, msiba ulikuwa kwa mdogo wake aitwaye Julius Patrick, Kigamboni.
Kwa mujibu wa familia kupitia kwa Julius, mwili ulisafirishwa kwa ndege Jumamosi asubuhi ya wiki iliyopita na kuzikwa siku hiyohiyo jioni lakini majibu ya uchunguzi hayajapatikana.


UMAFIA5.jpg


Marehemu ameacha watoto watatu na maofisa wa polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini wakasema msemaji ni mkuu wao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela.

UMAFIA6.jpg

ACP Kenyela alipopigiwa simu alithibitisha kutokea tukio hilo.
"Ni kweli mwili wa marehemu ulikutwa kwenye kisima chao lakini upelelezi bado unaendelea," alisema Kenyela.




Read more: HIVI NDIVYO AFISA USALAMA WA TAIFA ALIVYOUWAWA KIKATILI NA KUZAMISHWA NDANI YA KISIMA CHA MAJI HUKO KIJITONYAMA...!! - GUMZO LA JIJI
Lijendari uko wapi siku hizi?
 
Ni kukumbushana tu kwamba unaweza kumtolea Nape bastola kwa kutumwa na Makonda , lakini ukaja kujikuta unafia kwenye maua .
Samahani mkuu! Ila kwa ninavyofahamu wao wenyewe wanajua mwisho wao wataishia wapi... aidha wanaweza kuwa na mwisho mzuri au mbaya ila wanachokifanya ni ile kutii lolote/chochote wanachoagizwa au wanachotakiwa kukitekeleza kwa wakati husika. Si ndo sheria za mapolisi, wanajeshi na wanavyombo wengine wa ulinzi na usalama?!

Si jambo la kushangaza kwa yule bwana kumtolea silaha mheshimiwa Nape siku ile, alifanya alichoagizwa 🙂
 
Samahani mkuu! Ila kwa ninavyofahamu wao wenyewe wanajua mwisho wao wataishia wapi... aidha wanaweza kuwa na mwisho mzuri au mbaya ila wanachokifanya ni ile kutii lolote/chochote wanachoagizwa au wanachotakiwa kukitekeleza kwa wakati husika. Si ndo sheria za mapolisi, wanajeshi na wanavyombo wengine wa ulinzi na usalama?!

Si jambo la kushangaza kwa yule bwana kumtolea silaha mheshimiwa Nape siku ile, alifanya alichoagizwa [emoji846]
Intelijensia ni taaluma kama zilivyo nyingine, kama udakitari, na uhandisi, ukifika muda unastaafu vzr,Ila kuna masharti yake, mfano maofisa wa CIA, wanaostaafu, mfano akiandika kitabu kuhusu maisha yake, lazima kitabu kipitiwe na mamlaka za juu, kuona kama hakuna classified information, pili ofisa mstaafu wa CIA, FBI, hawezi, kujiamulia akaenda nchi nyingine kama Iran, au, Korea ya kaskazini, akatoa mafunzo kwa majeshi ya nchi hizo kama consultant, lakini anaweza kwenda austaria,Canada, nk,huku kwetu, uchawa mwingi,
Kila member wa security Agency, kuanzia polisi,armed forces, intelijensia, nk, ni majambazi amabayo hayajaamua kuua tu, yakipata nafasi, yanamtoa MTU robo,
Imetokea mtwara, makachero tena senior officers wa polisi, wamemuua kijana kwa sindano ya sumu, ili wamuibie milioni 30 tu! Wengine juzi wamefungwa miaka 20,kwa kosa LA kumbambikia mtu kosa.
 
Mkuu, marehemu hakwenda kuteka maji pale bali alitumbukia aidha kwa bahati mbaya kutokana na matatizo yake ya akili au alijitumbukiza. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa alishafanya majaribio kadhaa ya kujiua lakini aliweza kuokolewa.
Mkuu wanasema icho kisima kilikuwa kinalindwa.adondoke TENA.haaiingii kichwani
 
Back
Top Bottom