Utata kifo cha MC Pilipili: Wauaji hawajajulikana. Polisi wasema alishambuliwa, uchunguzi unaendelea

Utata kifo cha MC Pilipili: Wauaji hawajajulikana. Polisi wasema alishambuliwa, uchunguzi unaendelea

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma likithibitisha kushambuliwa kabla ya kifo cha aliyekuwa mchekeshaji na mshereheshaji, Emmanuel Mathias maarufu MC Pilipili, suala la kuwatambua waliomshambulia, limebaki kuwa giza nene.

MC Pilipili aliyekuwa mkazi wa Swaswa Jijini Dodoma, alifariki dunia Novemba 16, 2025 majira ya Saa 9:00 alasiri katika Hospitali ya Ilazo, Dodoma wakati akipatiwa matibabu kabla ya mwili wake kuhamishiwa Hospitali ya General jijini humo.

Akizungumza na wanahabari leo Novemba 19, 2025, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) William Abel Mwamafupa amesema kabla ya marehemu kufikwa na mauti, majira ya saa 8:00 mchana, msaidizi wake, Hassan Ismail, alipigiwa simu na mtu asiyejulikana aliyemuomba wakutane.

Amesema msaidizi huyo alikutana na watu watatu wasiomfahamu waliokuwa na MC Pilipili ndani ya gari jeupe. Watu hao walimkabidhi akiwa katika hali mbaya na kisha kuondoka.

Taarifa hiyo ya Polisi imeeleza, uchunguzi wa awali umebaini kuwa MC Pilipili alifariki kutokana na shambulio lililosababisha majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake, huku watu waliohusika na tukio hilo wakiwa bado hawajafahamika.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali
Taarifa zaidi zinasema Pilipili aliwasili Dodoma Jumamosi kwa usafiri wa Treni ya SGR akitokea Dar es Salaam, ambapo alipokelewa na watu ambao bado hawajajulikana.

Mmoja wa watu wa karibu wa familia hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amedai kuwa, watu hao waliondoka naye na ndio waliokuwa naye hadi kesho yake wakati anakabidhiwa kwa msaidizi wake.

Amedai kuwa msaidizi wake huyo ambaye pia ni DJ alipigiwa simu na watu ambao hakuwajua wakimwita afike kwenye eneo walilokuwepo.

“DJ alipofika eneo aliloelekezwa akakuta watu watatu kwenye gari, wakamkabidhi simu za Pilipili na kumwambia aondoke naye… Pilipili akapiga hatua tano baada ya kushuka kwenye hiyo gari (hawakuipiga picha) akashindwa kuendelea, lile gari likaondoka na kumuacha na DJ wake,” amedai ndugu huyo.

Ameendelea kueleza kuwa, msaidizi wake huyo alichukua Bajaji akampeleka Pilipili zahanati, ambapo daktari aliyemhudumia alipompima, alielekeza apelekwe hospitali ya mkoa (General).

“Walipofika huko ndipo ikabainika ameshafariki,” amesema.

Kuhusu majeraha mwili, ndugu huyo amesema, marehemu alikutwa na majeraha mengi eneo la mgongo, “inaonekana alichomwa na pasi ya moto (imekutwa alama), amekutwa na majeraha kichwani, inaonekana alipigizwa ukutani mara kadhaa.

“Shingoni amekutwa na machirizi ya kamba kama vile alifungwa na kuvutwa, pia kwenye mabega pande zote amekutwa na vidonda ni kama alichomwa na vitu vyenye ncha kali. Wale waliompokea na kumtesa familia haijajua ni kina nani ila inaonekana ni kama walitumwa kufanya hivyo,” amedai.

TAARIFA KUTOKA MTANDAO WA X
Taarifa Zaidi kutoka mtandao wa X (zamani Twitter) zinadai kuwa, Novemba 16, Pilipili akiwa jijini Dodoma, alikwenda Royal Village Hotel kwa ajili ya maandalizi ya shughuli iliyompeleka huko.

Inadaiwa kuwa, wakati anatoka na gari kuna gari mbili zikaanza kumfuata nyuma, watu hao walimkimbiza mpaka maeneo ya karibia na Swaswa Dodoma mjini ambapo walifanikiwa kulizuia gari lake.

“Baadaye wakashuka watu wanne… kisha wakaenda kwenye gari la MC Pilipili wakawa wakibishana kwa dakika kadhaa. Baadaye watu hao wakamshusha MC Pilipili kwenye gari yake kwa nguvu na kuanza kumpiga. Kisha walimwingiza kwenye moja ya gari zao kisha wakaondoka naye.”

Siku hiyo inaelezwa kuwa familia yake ilipigiwa simu ikajulishwa kwamba mwili wa MC Pilipili umeokotwa kando ya barabara na tayari umefikishwa General Hospital Dodoma.

“Ndugu walifika hospitali kwa ajili ya kuthibitisha kama kweli ni ndugu yao, baada ya kumkagua wakakagua mwili huo ulikuwa na jeraha la risasi, majeraha ya mijeledi maeneo ya mgongoni na kwenye bega alikuwa ameunguzwa na kitu kama pasi,” zimedai taarifa hizo.

Soma pia
 
Napata doubt moja..ujue ma MC Huwa wanakua wanapendwa na WANAWAKE..

Kwa kinywa chake mc pilipili aliwai kusema akiwa secondary wanawake/ mabinti wengi walikuaga Wana mzimia na kupenda anavyo ongea... wanawake hao walikua wanapenda ucheshi wake..

NB. ISIJE KUA PENGINE KISASI ALICHUKUA MWANAMKE / MKE WA MTU (KIBOPA) NDIO IKAPELEKEA KUTEKWA NYARA NA KUTESWA MPAKA KUPELEKEA MAUTI YA NDUGU MC PILIPILI & VICE VERSA IS TRUE.
 
Utata uko kwenye kumrudisha baada ya kumpiga tena wakapiga simu aje kuchukuliwa. Walitaka kumtesa tu ndiyo maana wakamrudisha ili apelekwe hospital? Wangekuwa na lengo la kumuua wangejihangaisha na kuchukuwa risk ya kumrudisha?
 
This is bullshit
mara kafa na presha mara kauwawa mara sijui nini?

which is which..

9dec tukutane tu FOCUS KWENYE TARGET.
 
Utata uko kwenye kumrudisha baada ya kumpiga tena wakapiga simu aje kuchukuliwa. Walitaka kumtesa tu ndiyo maana wakamrudisha ili apelekwe hospital? Wangekuwa na lengo la kumuua wangejihangaisha na kuchukuwa risk ya kumrudisha?
According to maelezo ya ndugu yake alishushwa ashakufa ht dr alisema alifika kashakufa

Km wangekuwa na nia vya kumtesa wasingempiga kichwani
 
Utata uko kwenye kumrudisha baada ya kumpiga tena wakapiga simu aje kuchukuliwa. Walitaka kumtesa tu ndiyo maana wakamrudisha ili apelekwe hospital? Wangekuwa na lengo la kumuua wangejihangaisha na kuchukuwa risk ya kumrudisha?
Aiseeee ngoja vyombo vifanye kazii ila hii saga itakua ni bifu ama KISASI...

INASEMWA MWILI WAKE ULIKUA NA JERAHA LA KUCHOMWA PASI YA MOTO NA MICHUBUKO MBALI MBALI..

Nimekumbuka miaka ya 90's kulikua na bro mmoja akiitwa Steve jamaa tukasikia kelele ya mwizi mwizii huyo bro akaja na pasi ya umeme imechemka aka mbandika mwizi mgongoni..

Bro Steve alikuaga gangster sana sijui yupo wapi Sasa...nakumbuka ile miaka mtu barabara ni kubwa ila msukuma amekariri anakufuata upande UNAO tembelea anakupigia kengele umpishe bro Steve alikua anawanyooshaga
 
Sidhani hata kama Polisi Wanahusika hapo. Au ndio ile Wahuni/Wahalifu wanafanya yao ili ijulikane ni Polisi

Haya ni mambo ya Bifu tu, lbd alitembea na mke wa Mtu
 
Sidhani hata kama Polisi Wanahusika hapo. Au ndio ile Wahuni/Wahalifu wanafanya yao ili ijulikane ni Polisi

Haya ni mambo ya Bifu tu, lbd alitembea na mke wa Mtu
 
Back
Top Bottom