Utata kifo cha MC Pilipili: Wauaji hawajajulikana. Polisi wasema alishambuliwa, uchunguzi unaendelea

Tungekuwa na taasisi huru na imara ya polisi, na ambayo haifungamani au kutumiwa kisiasa; hii kesi ni nyepesi sana.

Ila kwa sababu tuna taasisi ya hovyo, na ambayo inaendeshwa kisiasa; hata sitashangaa kuona imeishia kwenye uchunguzi tu, huku ikishindwa kuwatia mbaroni watuhumiwa! Huku ushahidi wote ukiwa hadharani.
 
Au wake za watu??

BTW: Emmanuel Mathias msaidizi wake ni Hassan Ismail hao mashehe wajipange!!
 
Hata padre walisema alikimbia madeni
 
Wameishia kujua gari.

1.Simu aliyopigiwa msaidizi haiwezekani kufahamika?

2.Kama Nchi ilikaa siku 6 pasipo mawasiliano ya maana,imekuwaje hiyo namba na vifaa vilivyotumika wasijulikane kwa haraka?

Wawe wanakaa kimya basi yakiwa yanatokea matukio kama hayo.Watu wajitafutie taarifa wenyewe.
 
Aisee nimesoma ujumbe wa dada mtu katuma kwa mtu na umewekwa kule insta
anasema wameambiwa wasiseme ...
Kasema kaka yake kapigwa risasi,pia alikuwa na majeraha ya kupigwa na fimbo na kuchomwa na pasi🥲🥲🥲

Mpk sshv nawaza
 
Hivi ndugu zangu wote niwaulize, kama (kwa mfano tu) tuseme kuna mtu ameajiriwa kama mkuu wa mahesabu wa kampuni au shirika na kukawa kuna upoteaji wa pesa kila mara na kila anapoulizwa pesa zimeenda wapi na ni nani anaeiba akiwa anajibu hajui, hivi mtu huyo atabaki na ajira kweli?

NImetowa mfano huo ni sawa na hawa askari wetu wa upelelezi walivyo na hii tabia ya kuwa kila mtu anapotekwa au kuuliwa tunaambiwa uhalifu huo umefanywa na watu wasiojulikana. Sasa kama hawa maafisa tumepoteza mamilioni kuwapa mafunzo ya uchunguzi na intelenjisia na hawana uwezo wa kutatua tatizo hili kuna haja gani ya kuwa nao? Kuna haja gani ya kuwaajri mijitu hii ambayo kila siku wanatupa jawabu moja tu "watu wasiojulikana". Inaonyesha mahalifu wana akili zaidi na umahiri wa juu kuliko vikosi vya upelelezi pamoja na viongozi wao, imefika wakati waanze kufukuzwa kazi kwa kushindwa kukamata wahalifu.
 
According to maelezo ya ndugu yake alishushwa ashakufa ht dr alisema alifika kashakufa

Km wangekuwa na nia vya kumtesa wasingempiga kichwani
Maelezo mengine yanasema alitembea hatua chache halafu akaanguka. Anyways, kwa nini wa-risk kumrudisha? Kwa sababu wakati wamemshusha gari yao ingeweza kuzingirwa na wao wakakamatwa.
 
NDUGU walipigiwa simu kuwa NDUGU yao ameokotwa barabarani.
Msaidizi wake anasema alipigiwa simu na watu wasiojulikana akamchukue pilipili.
Yote Kwa yote pilipili ameuliwa hakuna ubishi.
Bado polisi wanatafuta pa kuanzia?
Mimi sio polisi ila nawashauri kama kweli wanania ya kuwapata waanze na namba za SIMU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…