Utata kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa na mwalimu

Utata kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa na mwalimu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Utata umeibuka kufuatia kifo cha mwanafunzi wa shule ya sekondari Sabasaba, baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kutoa taarifa iliyoonyesha kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kilitokana na ugonjwa saratani ya damu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 22, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma kidato cha tati alifariki dunia akiwa katika hospitali ya rufaa ya Ligula alipokuwa akiendelea na matibabu.

Amesema kuwa baada ya kifo chake mwili wake ulifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kubaini kuwa chanzo cha kifo chake kilisababishwa na kuvuja damu nyingi isiyoganda iliyokuwa ikitokea kwenye ufizi wa mdomo wake.

“Kitendo cha kutoka damu hiyo kilisababisha kupoteza damu nyingi na mwisho kifo chake na kwa mujibu wa daktari, ugonjwa huo husababishwa na saratani ya damu.

“Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake ili waweze kuuhifadhiwa na hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo,” amesema Katembo

Kwa mujibu wa Kamanda Katembo Desemba 20 majira ya saa 12 jioni baba wa marehemu, Ally Said alifika na kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi akisema kuwa, binti yake alikuwa anaumwa sana na kwamba ugonjwa wake ulisababishwa kipigo kutoka kwa mwalimu wake wa Kiingereza aliyewaadhibu kwa viboko Oktoba 20, 2022.

Alipoulizwa na Mwananchi, baba huyo ameendelea kusisitiza kuwa mwanaye alishindwa kujibu maswali akaadhibiwa.

“Mtoto aliambiwa ajibu swali akashindwa, ndipo mwalimu alimpiga mpaka akadongoka, kisha alikimbizwa polisi ambako walimu na polisi walisema arudi aje tuelewae nyumbani.

“Mama yake alimpeleka kwenye zahanati na alipopimwa walisema kuwa amepungukiwa damu na kuwa na presha ya kushuka,” amedai Said.

Naye mama wa binti huyo, Amina Manyari amesema kuwa mtoto huyo alipona mwalimu anampiga sana aliomba asiendelee kupigwa kwa kuwa hajisikii vizuri.

“Mtoto alisema hajisikii vizuri lakini mwalimu hakuelewa akaendelea kumpiga kwenye paja mgongoni na akatumia makofi na ngumi ambapo mtoto alifukuzwa darasani wakati anatoka alidondoka shuleni, nilipopewa taarifa nikaenda haraka shuleni nikakuta wamelaza kwenye dogoro ofisini ambapo nilimchukua,” amesema Manyari

MWANANCHI
 
Mimi ningefungua Bucha, huwezi nipigia mtoto wangu dizaini hiyo.
 
Sijui waalimu wa Tz wanatumia Nini hawana tofauti na Vichaa , Mtu hujalala nae ,sio mwano , sio ndugu yako ...lakini unaamua kumpa mijeredi mikali Hadi anapoteza Fahamu kifo ulemavu * nk*
Na idara zote huwa unazisema vibaya hivi au una visa na walimu?
 
Kwa vyovyote vile mwalimu hana kosa hata kama kwa sehemu ya kifo cha marehem atakuwa kahusika.

Kwanini nasema hivyo?

Kwasababu Daktari,tena wa serikali ameshathibitisha kwamba mwanafunzi hajafa kwasababu za kupigwa bali kwa ugonjwa na ni ugonjwa ambao hausababishwi kwa kipigo.

Lakini pia kisheria mwalimu anonekana hana hatia kwasababu ya muda uliopita tangu mwanafunzi apigwe na mpaka umauti ulipomkuta na hasa kwasababu wazazi wamekuja kulalamika baada ya kifo cha mwanafunzi kitu ambacho inaonesha wanataftia pa kuangushia lawama.
 
Tupinge adhabu zisizofaa kwa mwanafunzi lakini pia tusipuuze report za wataalamu wa afya
 
Sijui waalimu wa Tz wanatumia Nini hawana tofauti na Vichaa , Mtu hujalala nae ,sio mwano , sio ndugu yako ...lakini unaamua kumpa mijeredi mikali Hadi anapoteza Fahamu kifo ulemavu * nk*
MkuunTuamini ripoti ya polisi na madaktari au tuamini haya maneno yako yaliyojaa chuki dhidi ya walimu?
 
Back
Top Bottom