Licha ya kuwa Kuna baadhi ya walimu wanakosea, watu wengi Wana chuki binafsi na walimu
Kuna matukio mengi makubwa yanaendelea kwa madaktari, wanasiasa, mapolisi nk ila kesi ikiwa kwa walimu ndio huwa inakuwa multiplied mara 100
Kuna watu humu kuwalea watoto wao tu wanashindwa, then assume unakuwa na watoto 200 walioshindikana kwa wazazi wao
Wakati huo huo mkumbuke, Kuna mikakati ya kiwilaya na kimkoa inataka shule zifanye vizuri, zisipofanya vizuri huwa walimu au shule inawajibishwa
Yaani hapo ukiwa serious utakutana na matukio kama haya, ukiwa free utakuja kusemwa na wazazi, walimu na wanafunzi hawana Nidhamu, wanafelisha, yaani hakuna la afadhali
Kuna mwalimu alikuwa na slogan yake " BORA SHULE IFELI KULIKO MAMBO YANGU YAFELI"
Ni muda Sasa wa walimu kubadilika, hakuna haja ya kujichosha, fundisha kibosi, mwanafunzi asipoelewa achana naye ataelewa kwenye chumba Cha mtihani, fika shuleni mawazo yako yawe kwenye miradi yako
Wanafunzi wakifeli, hasara sio yako, wakifaulu faida ni yake na wazazi wake, hamna haja ya kujitesa na kuingia kwenye risk