Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Huenda labda ni kuchanganyikiwa au kutokujipanga kwa viongozi wa Tanzania katika kutetea mkataba wa uwekezaji wa bandari baina ya DP world na Tanzania. Kumekuwa na kauli za kukinzana na kuvuruga kutoka kwa viongozi watetezi wa sakata hili ili kujibu shutuma za Bandari yetu kutolewa bure na milele kwenda kwa muarabu wa Dubai. Watetezi wanasema kilichopitishwa bungeni sio mkataba bali ni makubaliano tu ya ushirikiano baina ya Tanzania na Dubai, yanayotengeneza msingi wa mamlaka ya bandari Tanzania kukaa chini na kujadiliana na Dp world na mwisho kutengeneza mkataba wa uwekezaji wa bandari. Maajabu ni kuwa serikali imekuwa ikijivunia faida za kitakwimu tutakazopata Tanzania kupitia uwekezaji wa Dp world hapa Tanzania wakati huo huo viongozi hao hao wanasema kuwa majadiliano bado na mkataba bado!
Maswali.
1. Wamejuaje hizo faida kabla ya majadiliano au kuwepo mkataba?
2. Hizo faida zimeandikwa wapi na zinasimamia misingi ipi ikiwa majadiliano bado na mkataba bado?
3. Nini mantiki ya kwenda kwenye majadiliano au kutengeneza mkataba tena wakati kila kitu chenye faida kwetu kipo tayari kwa kuwa serikali yetu na DP wameshapatana, kukubaliana na kupitisha bungeni?