Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Sawa mkuu ila hii tathmini imefanyika upande wetu sisi watanzania sio wao .Mkuu hizo faida serikali inawezaje kuzitarajia na kujivunia nazo hadharani wakati huo huo inasema hata majadiliano na DP world bado hayajafanyika?
Hizo faida hata DP world hawajazisema popote, serikali ya Tanzania inapata wapi huo ujasiri na uhakika wa kuzipata?
Pia tunatakiwa kama ni kweli pawe na ufuatiliaji wa je hizo tathmini kweli zitafikiwa ?
Ndo maana hata muwekezaji akipewa tenda ya kujenga barabara katika ubora fulani ,wanafuatilia kujua je ni kweli kama makubalini na kama unakumbuka Magufuli alikuwa anavunja kabisa na nyundo kuangalia ubora.
Ishu katika nchi zetu ni ufuatilia wa "performance of contract" je muwekezaji anaweza kutimiza yale aliyoahidi maana sisi kama watanzania kwa makubaliano tushafanya tathmini yetu na kujua tutapata asilimia fulani kama ongezeko.
Kumbuka kagame alitaka bandari na alifanya tathmini na kuahidi kiasi fulani kama faida ambacho ni kikubwa zaidi ya tulichokuwa tunapata.