Tetesi: Utata mkubwa ripoti ya CAG , kuna uhariri umefanyika

Kama ni wewe ungekosoa kipindi meko akiwa hai? hulka za meko tunazijua
 
Yuko kwenye mioyo ya wapumbavu kama wewe, watu wasiojulikana waliibuka kwenye utawala wake, uhuru wa kuongea ulipotea chini yake, kufukuzwa kazi kinyume cha katiba ilikua chini yake bado tu mtu huyo unamtetea pumbavuuu
 
Hebu na wewe tumia akili yako vizuri. Kwani hata bila kusoma ripoti ya CAG unaiona ATCL ikiendeshwa kwa faida?

Wasafiri wa mara kwa mara tunaona mengi. Kama Bomnaedier ya Dar -Mwanza inaweza kuruka na abiria 40 badala ya 60 ujuwe kuna shida!!
 
Wewe uliyeandika kumtetea Hayati Magu inaonekana umekasirishwa sana na ripoti ya CAG iliyojaa ukweli mtupu.Dikteta yoyote duniani hakosi wafuasi yaani Die hard supporters.Wewe mmojawapo.Mfano stendi ya mabasi Mbezi(Magufuli Stand),ilijengwa kuingiza mabasi 254 lakini Magu akaingilia kati akataka majengo makubwa ili jina lake lionekana,matokeo yake mabasi yanayoweza kuingia sasa ni 152 tu.Vurugu tupu.Mengine utajijibu mwenyewe.Mwache Madam President afanye kazi zake.Sasa tunaandika kwa uhuru,akina Mbowe,Zitto na wengine angalau wapo huru wanasikika.Kwa muda mfupi tu nchi inaelekea kama nchi yenye Uhuru kamili.#KAZI ZINAENDELEA.Salaam za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Awamu ya 6.
 
Lakini inawezekana hii ndio taarifa iliyotayarishwa lakini ilikuwa inasubiri kuwa edited kulingana na kile walichodhani ni matakwa ya Mwendazake. Rais mpya aliposema anataka isiokuwa edited basi wakaitoa original.

Inachonisikitisha ni kuanza kumwaga sumu dhidi ya Rais mpya ambae ni wa chama chenu bado. Huyo Kafulila tangu lini amekuwa upinzani?

Amandla...
 

SAFI SANA NA NZURI SANA.HIYO PARAGRAPH YA MWISHO INA UKWELI ASILIMIA MIA MOJA. HUKU MTAANI WANANCHI WANAWATAZAMA TU LAKINI HAMYAJUI YALIYOMO MOYONI MWAO.KUMBUKENI FITNA HUZAA FITNA.
 
Riport Ina ukakasi hii in reality kuna fix watu Wana cheza


Any way inakuwaje Mimi nanunua uwanja najenga ukumbi wa bishara yani na hotel ILA kabla sijafungua iyo hotel tayari niwe Nisha pata hasara wakati bishara na mradi haujaanza kufanya kazi
 
Huku mitaani mambo aliyo yafanya Magu ndio hakimu wa hizo tuhumazao.
Wananchi wanaona, ngoja tuendelee kuupa muda nafasi ya kuamua tutaona wao wanafanya nini kizuri zaidi.
 
Unaambiwa juu ya SGR, yaani unatajiwa SGR imesababisha hasara zaidi ya 3b hatuambiwi imeingiza faida kiasi gani , mashaka matupu, nilitegemea atuambie na upande wa pili imeingizia faida kiasi gani.[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Hapo juu hapana UMEPOTOKA.. Huo mradi uko bado hatua ya ujenzi utazungumziaje faida? Pili hasara inayoongelewa hapa ni kwa mkandarasi kushindwa kulipwa kwa wakati as per contract na hili tatizo liko kwa wakandarasi karibia wote..
Hasara ya fidia kutokana na kutotii makubaliano kwenye mikataba
 
Penye faida hakuna hasara na penye hasara hakuna faida.Faida na hasara haviwezi kukaa kapu moja !!
 
Penye faida hakuna hasara na penye hasara hakuna faida.Faida na hasara haviwezi kukaa kapu moja !!
Hapana! Ukihesabu mapato tu bila kujali mtaji na matumizi utaona unapata faida kubwa sana
 
CAG hawezi kuongea bila ushahidi nyie acheni siasa za kutaka kumtetea dikteta wenu. Huyu hakufaa kabisa kuwa rais labda unyapara wa barabara ulikuwa unamfaa zaidi.
 
Mtahaha sana wallah... Yaani CAG alishwe matango pori halafu baadaye aliyemlisha atokee hadharani kuja kusema risiti zipo..!!!! Huoni kwamba kama alilishwa matango pori, huyo mlishaji ana kosa la kutoa taarifa za uwongo wakati anahojiwa? Hivi ukimdanganya CAG huoni kwamba unajipalia makaa ya moto?
 
 
Tatizo siyo risiti, tatizo ni MALIPO BILA MKATABA ULIO SAINIWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…