Utata wa kanisa la Arise and Shine. Je, linatumia usajili wa Calvary Assemblies of God(CAG)?

Utata wa kanisa la Arise and Shine. Je, linatumia usajili wa Calvary Assemblies of God(CAG)?

Mi mwenyewe nimeona kuna utata hapo! Kivipi? Wakati wa uzinduzi juzi kati Maboya alikuwa anatambulishwa kama askofu mkuu. Inafahamika kuwa Maboya ni Kiongozi mkuu wa kanisa la Calvary Assemblies of God. Lini Mwamposa alijinasibisha kuwa ni mshirika wa CAG? Mwamposa tangu yupo Moshi alijishughulisha na Inuka na Uangaze (Arise and Shine) na yeye ndiye kiongozi wake na si Maboya wa CAG. Je Arise and Shine inatumia usajili wa CAG? Maana kwenye uzinduzi ilikuwa inatamkwa ARISE AND SHINE CALVARY ASSEMBLIES OF GOD. Nijuavyo hayo ni makanisa mawili tofauti na kila kanisa lina kiongozi wake. Sasa hapa mbona wanatuchanganya, kiongozi ni Maboya au Mwamposa? na je hilo ni kanisa moja au mawili?
 
... Je Arise and Shine inatumia usajili wa CAG? Maana kwenye uzinduzi ilikuwa inatamkwa ARISE AND SHINE CALVARY ASSEMBLIES OF GOD. Nijuavyo hayo ni makanisa mawili tofauti na kila kanisa lina kiongozi wake. Sasa hapa mbona wanatuchanganya, kiongozi ni Maboya au Mwamposa? na je hilo ni kanisa moja au mawili?
na Maboya alikuwa anaongea kwa kujiamini kama vile yupo nyumbani!
 
na Maboya alikuwa anaongea kwa kujiamini kama vile yupo nyumbani!
sijawahi kumsikia wala kumsoma maboya kuwa ni kiongozi wa arise and shine tangu mwamposa yuko moshi, imekuwaje kutambulishwa kama askofu mkuu wakati yeye ni kiongozi wa calvary assemblies of god?
 
Makanisa mengi hususani ya kiroho hayana usajili binafsi ila yanajiweka chini ya mwamvuli wa usajili wa makanisa mengine.
Ukitaka kuhakiki hili jaribu kufuatilia na ukikutana na kanisa linaloitwa tawi la......elewa ni ile " under the umbrella".
 
Walifanya mipango yao kuligunga ufunuo na uzima la Gwajima ili twende au tuhamie Rise and shine la Mwamposa.

Kuanzia leo mimi nahamia lile la mchungaji mtume Askofu masihi ZUMARIDI yeye anaenda Mbinguni na kurudi kila siku.
 
Haya makanisa ya kiroho huwa yanakuwa na majina fulani kama a.k.a, mfano Mlima wa Moto la aliyekuwa Mch. G. Rwakatare lilikua chini ya uangalizi wa EAGT. Kuna makanisa mengine unakuta labda linaitwa Moria Christian Center, Horebu Christian Center, Shalom Christian Center, Mlima wa Sayuni Christian Center, Beroya Christian Center. Huu unakua ni kama utambulisho wa huduma fulani ya kiroho maalum inayotolewa na kanisa hilo.

Kwa mantiki hiyo, hata huduma ya Arise and Shine chini ya mwamvuli wa CAG, inaweza kutambuliwa zaidi kutokana na huduma inayotolewa pale kuliko jina la mwangalizi wake (CAG).

NB:
Maoni yangu sio sheria
 
Endelea kwenda kukamuliwa sadaka tu mkuu, usihoji 🙂
 
Watumishi wengi huwa hawapendi kwenda shule za theolojia na kupata vyeti vya kuwarahisishia usajili wa makanisa yao kwenye mamlaka lakini pia huwa hawapendi mlolongo wa hatua za usajili wa kanisa ambazo kimakadirio huwa inachukua miaka miwili mpaka miaka mitano ili mamlaka ijiridhishe juu ya huduma yako ndio uwe full registered na mamlaka jambo ambalo kwa watumishi wengi huwa wanashindwa kuvumilia ili kukimbizana na maokoto ndio wanajikuta wanazama kwenye mitego ya hivyo.
 
Mwaka juzi kuna mtu Arusha aliwahi kuniambia kuwa Maboya ni baba wa kiroho wa Mwamposa
 
Nadhani watu wengi wanaongea bila kujua ukweli. Kanisa la CAG la Maboya limeruhusu wachungaji wake kutumia majina ya huduma zao lakini wakiwa Chini ya CAG. Arise and Shine ni mojawapo ya makanisa yanayotumia nicknames ila lipo Chini ya CAG.
 
Back
Top Bottom