Utata wa kanisa la Arise and Shine. Je, linatumia usajili wa Calvary Assemblies of God(CAG)?

Utata wa kanisa la Arise and Shine. Je, linatumia usajili wa Calvary Assemblies of God(CAG)?

Mi mwenyewe nimeona kuna utata hapo! Kivipi? Wakati wa uzinduzi juzi kati Maboya alikuwa anatambulishwa kama askofu mkuu. Inafahamika kuwa Maboya ni Kiongozi mkuu wa kanisa la Calvary Assemblies of God. Lini Mwamposa alijinasibisha kuwa ni mshirika wa CAG? Mwamposa tangu yupo Moshi alijishughulisha na Inuka na Uangaze (Arise and Shine) na yeye ndiye kiongozi wake na si Maboya wa CAG. Je Arise and Shine inatumia usajili wa CAG? Maana kwenye uzinduzi ilikuwa inatamkwa ARISE AND SHINE CALVARY ASSEMBLIES OF GOD. Nijuavyo hayo ni makanisa mawili tofauti na kila kanisa lina kiongozi wake. Sasa hapa mbona wanatuchanganya, kiongozi ni Maboya au Mwamposa? na je hilo ni kanisa moja au mawili?
Mwamposa ni muumini mwaminifu wa C.A.G tangu zamani na ministry yake Iko chini ya Maboya
 
Tulia nikujuze

TAG ilipopata Changamoto Askofu Moses Kulola aliondoka na kuanzisha EAGT na Kwahiyo Vijana walokole wa wakati ule akina Kakobe, Lusekelo, Mitimingi, Gamanywa, Maboya, Gwajima na wengine wengine wengine wakaondoka TAG ya Lazaro na Mwenesongole na kumfuata baba yao wa Kiroho Moses Kulola

Kulola akafungua mlango kwa hawa Vijana wake kuanzisha ministry zao chini ya Mwamvuli wa EAGT

Hawa Vijana walipokomaa nao sasa wameruhusu hawa New Generation kuanzisha ministry Chini yao ndio hawa unawaona akina Mwamposa, Kulaya, Msungu, Musa nk

Karibu sana 😄🙏
 
Back
Top Bottom