Na kama unakumbuka vizuri mkuu swala zima la Chama kuyumba lilianza pale kinana wa Chama kwa wakati huo (mzee masilingi akiwa na kijana wa goli la maradona) walipokuja na agenda ya kujivua gamba.
Hii issue ilita mzozo sana na kuna habari kuwa ndani ya mkutano flani wa chama pale chimwaga wakati mkutano unaendelea Morani kwa ujasiri wa kimotoni alisimama na kutoa japo kidogo tu ya moyoni pale alipomuuliza mkwere kwamba inakuaje anakubali vijana wadogo (vijana toka mtam, akina December etc) wamchafue kwamba yeye ni fisadi tena fisadi mkubwa kwenye skandali ya richimondi wakati hakuna chochote alichokifanya asichokijua mkwere kwenye ile issue.
Matokeo yake mkwere aliwapiga biti madogo ambao ndio walikuwa vinara wa kuvua watu na magamba pamoja na mzee masilingi kwamba hataki kuskia tena issue ya magamba
From there ndio maana hata akina joka la makengeza wakaanza kujitapa hadharani kwamba magamba yamevuliwa yakaishia kiunoni.
Baada ya kuona mambo si mambo mkwere ikabidi amtafute mkulima kutoka Iringa arudi kusaidia kuokoa jahazi la chama na pia akapanga kikosi upya kinana akaletwa kuchukua nafasi ya masilingi alafu masilingi kutulizwa akatupwa zake kwa Trump kama balozi wetu huko.
Akina December wakatolewa kwenye kazi za chama wakapewa shavu serikalini yaani hii movie acha kwanza niweke pause.