Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Nina undugu na binti wa kwanza aliyefichua unyama wa babu seya kwa mama yake baada ya kubanwa aseme kwa nini alichelewa kurudi shule. Kama ndugu tunasamehe kwa muda aliokaa jela hautoshi kulinganisha na madhala aliyosababisha. Ilikuwa hivi sitataja majina. Mtoto X(ndugu) alichelewa kurushibshule, mama mlezi alimbana amueleze kwanini kachelewa. Mtoto X alijibu alichelewa sababu walipitia kudai pesa kwa babu, mama mlezi alizidi dadisi pesa ya nini na kwa kazi gani? Mtoto X akajichangaya na asiweze jibu. Mama akahisi kuna kitu hapa, ilikumuonyesha upendo na kumtoa hofu akaamua kumkumbatia, akahisi harufu mbaya toka kwa binti, akahisi binti haogi vizuri, lakini alipokwenda deep akagundua mtoto kahalibiwa. Akatumia mbinu ya ziada ikiwa ni pamoja na kutumia ukali, binti akatoa siri. Mama mlezi aka panic akapiga simu kuomba ushauri kwa ndugu yetu mngine, being kwamba yeye ni mlezi na mtoto anatoka kwa upande mume ikaonekana kwa kiwango cha uharibifu ule, na yeye kuchelewa kugundua itaonekana hakuwa karibu na mtoto lakini ikashauliwa shauri lipelekwe Polisi Urafiki, Babu seya akakamatwa akawekwa ndani. Mpaka hapo mlalamikaji alikuwa huyo ndugu yangu na mtoto aliyepata madhala ni huyo mmoja.
BABU SEYA ALIKOROGA.
Kumbuka wakati huo bendi ya babu seya ilikuwa inapiga Polisi officers mess, Babu alikuwa karibu IGP hiyo habari zilimfikia mkuu huyo na kumuarisha Tiba kumtoa. Tiba akamtoa kwa dhamana, Babu asikae kimya, nyumba ya Babu na Mlalamikaji zilikuwa jirani, Babu alivyotoka polisi si akaanza tambo, ohoo sisi watu wakubwa wewe utafanya nini. Mlamikaji akaona amedhalilishwa, akaana mhoji mtoto wake kwa upole na huku akimuadi hata muampiga wala kumsemea kwa baba ambae wakati huovalikuwa safarini. Mtoto akafunguka kuwa hayuko peke yake, huwa wako wengi na hupitia shule na huwaombea ruksa kwa Mwalimu. Kati ya watoto wa jirani sana na Mlalamikaji ni muhaya kama ulifuatilia kesi kulikuwa na jina la Koku. Mlalamikaji akaenda kwa mama K akamuelezea mama K akawambishi kuwa K hawezi fanya hayo, na K pia akiulizwa alikataa kabisa, lakini Mama X alijua K anaogopa sababu ya kipigo kwani familia hiyo kwa kipondo sio mchezo. Mama X akamtaka mama K amuhakikishie K kuwa akikosema ukweli hatampiga, alipomuhakishia K nae akasema ukweli na zaidi ya alichosema X. Mama K alikuwa na pressure, kwa ilipanda ghafla akapoteza fahamu. Kumbuka Mama X baada ya yeye kumripoti babu Seya, kazidiwa kete sasa anataka support. Kile kitendo cha mama K kupoteza fahamu kikaleta tahaluki mtaani watu wakajaa kujua kullkoni? Ikabidi Mama X ajatibu kwa uwezo waka kuwajuza wananzengo ambao wengine ndio kwanza walijulishwa mabinti zao ni wahanga. Juhudi zilifanywa kumpepea Mama K lakini pia kupigia Baba K na wababa wengineb warudi home kukabiliana na mkasa. Wababa waliporudi na kusikia mkasa na jinsi mama X alivyojaribu kulipeleka hilo kwenye chombo husika na mtuhumiwa kuachiwa wazee wakapandwa na hasira.
TIBA ANAHUSISHWA NA KAMATA YA PILI YA BABU SEYA.
Baazi wa wababa walishaamua kuchukua sheria mkononi yaani kumuangamiza babu seya na familia yake. Baba K alikuja na wazo mbadala, kwa yeye alikuwa mtu wa Bukoba na wa karibu na mkuu wa polisi wa kanda, na pia huyu ni baba wa ubatizo wa mtoto K ambate pia ni muahanga, baba K alimpigia simu Tiba. Kwenye simu alimuambia tiba mkasa wote, na kwamba licha ya kwamba mlalamikaji alikuwa Mama X, babu Seya hakufanyia kitumbaya mtoto X pekeyake bali watoto wengi pamoja na mwanao wa ubatizo K, na sasa mazali wameshajua Baba seya ni rafiki wa IGP kama wazazi wameamua kuchukua sheria mkononi, yeye anajua kitachofuati ni yeye baba K na wenzake kusota jela hivyo ajiandae kusaidua familia akiwa kama ndugu. Tiba akaomba chonde chonde kisifanyike chochote mpaka atakapofika. Kweli muda Landrover Discovery likatinga Sinza nyumba wafanyakazi wa Kiwanda cha Sigara. Tiba akasikia yeye mwenyewe alisikia maelezo toka kwa mlalamikaji wa kwanza na aliwahoji watoto wahanga, akapiga radio call kwa mkuu wake, akimtaarifu kutii amri ya mtoa babu S kwa zamana, lakini pia maendelea ya sakata na yuko na wazazi ambao wameamua kutoa uhai wa Babu na watoto wake. Polisi mkuu akasikika akijitoa lawama kuwa kama hali niyo basi afanye awezavyo. Babu S alikamatwa tena, this time pamoja na watoto wake, sisi tulichukulia kuwa watoto wa babu wanawekwa ndani sababu ya usalama wao na hasa baada ya wananzengo kutishia maisha yao.
USHAHIDI ULIOMKANDAMIZA.
Mengine yote yakuwa maelezo na hali ya watoto waliohalibiwa lakini tisi ni siku mahakama ilivyohamia nyumbani kwa babu S. Watoto wahanga walionyesha mahakama mazingira yote ikiwa ni pamoja na mikeka na mafuta ya mgando aliyotumia. Yaani imagine mtoto mmoja anasema alikuwa anatufanyia kwenye mkeka alafu anaenda mahali ulipofichwa alafu anasema tena huu hapa, then mngine anasema alikuwa anatupakaga mafuta, mngine anachoma chumba anakuja na mafuta, watoto sio mmoja wanaitika si hayoo hapo.
Hitimisho:
Mimi ni mtu wa karibu na mhanga kama nilvyosema, nilikua na jua Babu S. anahatia lakini bado sikujua alifanya yale kwasababu gani, ni ugonjwa au ni nini? Na kwa nini afanye pamoja na watoto wake. Juzi niliposikia hukumu ya mbunge mmoja wa kongo ambaye amehukumiwa na mahaksma ya kimataifa kwa kufanya unyama wa aina hii akiwa ana wapiganaji wake kwa kufanya ushirikina nikapata jawabu kuwa huko kwa wenzetu kongo hili ni jambo la kawaida.
Mara ya mwisho nimemuona X sasa ni mdada mkubwa tuu. Amesoma anafanyakazi, lakini hayuko ok, inawezekana madhala mengine ameyapata kutokana na kushawa wa watu wa karibu, maana isiwe msiba, vikija vibibi vya kutoka mkoani vilikuwa vinakumbushia, hivi yule mtoti ni yupi? Walikuwa wanamshaa kana kwamba kajinyea.
Mwisho