upendodaima
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 4,078
- 4,504
Ilikuwa ni Pegeout 501 alitoka nayo Vitani Uganda akakataa kuilipia Kodi na Ushuru mpakani kwenye idara ya Forodha akijinasibu yeye ni DG wa Tiss.
Habari zilipofika kwa Nyerere akatimuliwa kazi!
Sio Uganda mkuu,soma sehemu ya mahojianao yake na Raia mwema hapo kuhusu hilo sakata la gari..
Raia Mwema: Tueleze kuhusu Seychelles
Dk. Kitine: Huko nimekwenda na nchi nyingine nyingi Afrika. Mimi ni mpigania uhuru. Nimekwenda Comoro, Madagascar, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini kote huko.
Raia Mwema: Inasemekana ulipata gari aina ya benz kule Seychelles, uliletewa hapa ndani ya ndege.
Dk. Kitine: Si kweli. Hakuna kitu kama hicho. Sijawahi kuwa na benz. Ni uzushi. Nilinunua gari mimi kule Peugeot, 405, na nilinunua ile gari kwa dola hata 1,000 hazikufika. Sijui 500 au 600, na hiyo pesa niliyotumia alinipa Hassan Ngwilizi.
Halafu yeye alikuwa na mjomba wake hapa (nchini), alikuwa anajenga nyumba yake kule Lushoto akaniambia tafadhali kampe mjomba wangu hiyo, ilikuwa sawa na shilingi laki sita au saba.
Alinunua ile gari kwa niaba yangu, baadaye akafanya utaratibu wa kuileta huku, sasa alitumia hela yake hata dola 1,000 haikufika. Akaniambia tafadhali najenga nyumba kule kampe mjomba wangu.
Nimefika hapa nikampa hiyo pesa. Gari yenyewe nimenunua ya zamani ilikuwa ya hela ndogo, akanipa niilete. Lakini watu wakapiga kelele. Nimenunua gari, Mwalimu (Rais Nyerere) amenifukuza kazi.