Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Kifo cha Sokoine hakina utata wowote; ilikuwa ni ajali kawaida ya gari huko Morogoro. Nilikuwa nafanya kazi kama fundi umeme kwenye kiwanda kimojawapo hapo Mororogo, na usiku wa kuamkia ajali hiyo nilikuwa nimefanya night shift. Kwa hiyo wakati taarifa zinaingia mjini na mwili wa Sokoine kuletwa pale hospitali ya mkoa, nilikuwa niko mitaani. Magari yote mawili yaliyohusika na ajali ile yalisombwa na kuhifahdiwa pale Polisi Dar es Salaam road kwa zaidi ya miaka miwili. Watu wote watatu waliokuwa kwenye gari ile waliumia vibaya sana, ila ni Sokoine tu ndiye aliyekufa wakati dereva akivunjika miguu yote wiwili, na mlinzi (ADC) naye akiwa na majeraha makubwa sana kifuani na usoni.Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati Sokoine kwa vile alipofariki nilikua bado sijazaliwa, nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;
1. Ajali iliyosababisha kifo cha Sokoine ilikuwa ya aina gani? Kupinduka kwa gari, kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?
2. Katika hiyo ajali hayati Sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?
3. Kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?
4. Kama wako hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?
4. Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?
5. Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?
6. Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?
7. KWANINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?
Kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.
Chinga 1.
Conspiracy theories zote zilizozuka baada ya kifo hicho kuwa aliuwawa kwa njama ni uwongo mtupu; alikimbizwa hospitali ya mkoa Mororgoro pale karibu na kanisa katoliki kujaribu kuokoa maisha yake ikashindikana. Dereva wa gari ya ANC aliyesababisha ajali ile akiitwa Dumisani Dube alikuwa akiendesha gari huku amelewa, kwa hiyo alipokutana na msafara hakusimama, na polisi walipojaribu kuingilia kumsimamisha kwa nguvu ndipo akagonga gari ya Sokine head on. Tanzania hatukuwa na sheria dhidi ya drinking and driving (DUI) kwa hiyo ulevi wa Dube wakati wa ajali ile haukuzungumzwa sana





