Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Kifo cha Sokoine hakina utata wowote; ilikuwa ni ajali kawaida ya gari huko Morogoro. Nilikuwa nafanya kazi kama fundi umeme kwenye kiwanda kimojawapo hapo Mororogo, na usiku wa kuamkia ajali hiyo nilikuwa nimefanya night shift. Kwa hiyo wakati taarifa zinaingia mjini na mwili wa Sokoine kuletwa pale hospitali ya mkoa, nilikuwa niko mitaani. Magari yote mawili yaliyohusika na ajali ile yalisombwa na kuhifahdiwa pale Polisi Dar es Salaam road kwa zaidi ya miaka miwili. Watu wote watatu waliokuwa kwenye gari ile waliumia vibaya sana, ila ni Sokoine tu ndiye aliyekufa wakati dereva akivunjika miguu yote wiwili, na mlinzi (ADC) naye akiwa na majeraha makubwa sana kifuani na usoni.

Conspiracy theories zote zilizozuka baada ya kifo hicho kuwa aliuwawa kwa njama ni uwongo mtupu; alikimbizwa hospitali ya mkoa Mororgoro pale karibu na kanisa katoliki kujaribu kuokoa maisha yake ikashindikana. Dereva wa gari ya ANC aliyesababisha ajali ile akiitwa Dumisani Dube alikuwa akiendesha gari huku amelewa, kwa hiyo alipokutana na msafara hakusimama, na polisi walipojaribu kuingilia kumsimamisha kwa nguvu ndipo akagonga gari ya Sokine head on. Tanzania hatukuwa na sheria dhidi ya drinking and driving (DUI) kwa hiyo ulevi wa Dube wakati wa ajali ile haukuzungumzwa sana
 
Ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…