..ni RISK kubwa sana ku-host makundi yenye silaha.
..kwanza, Tz tulikuwa tunakaribisha mashambulizi toka kwa wareno na makaburu.
..pili, kulikuwa na hatari ya kutokea vurugu na mapigano baina ya hawa wapigania uhuru wenyewe kwa wenyewe ndani ya ardhi yetu. Zanu na Zapu toka Zimbabwe walishapata kupigana kwenye makambi yao yaliyokuwa Tanzania.
..tatu, kulikuwa na hatari ya hawa wapigania uhuru kufanya vurugu au maasi dhidi ya serikali ya Tanzania. Kuna taarifa za kihistoria za wapiganaji wa ANC kuamriwa kuondoka Tanzania kutokana na sababu za kiusalama. Rejea historia ya makao makuu ya ANC kuhama toka Tanzania kwenda Zambia. Pia rejea historia ya Yasser Arafat na PLO kuhamishwa toka Jordan kwenda Tunisia.
..Samora Machel alitwaa madaraka ya Frelimo kwasababu yeye ndiye alikuwa mkuu wa majeshi. Askari wa Frelimo walikuwa nyuma yake, na hivyo kumwezesha "kumpindua" Uria Simango ambaye alikuwa na background ya Uchungaji wa Kanisa.
..Pia kwenye bandiko lako umemuelezea Samora Machel kama "mfunga vidonda" ktk majeshi ya Frelimo. Yes, Samora Machel aliwahi kuwa muuguzi, lakini baada ya kujiunga na Frelimo alipata mafunzo ya kijeshi kwa hivyo ni askari aliyekamilika.
..Vilevile sijui kama umewahi kumuona Samora Machel au kumsikiliza. Huyu bwana alikuwa na karama ya kuzungumza na kuhamasisha. Kuna kipindi alikuja Tanzania na kuhutubia zaidi ya masaa manne na wananchi wa Dsm walitulia na kumsikiliza.
..Frelimo ilihitaji kiongozi aina ya Samora kumrithi muasisi wao, Eduardo Mondlane, ambaye aliuwawa.