chuwaalbert
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 3,598
- 2,118
Ni ukweli mchungu, na hili Mwalimu Nyerere alijua kuwa ni ukweli mchungu.
Nilikuwa na maana halisi ya kuanzisha mada hii
Asante sana mkuu wangu kwakuleta mambo mpya yenye kuibua mjadala zaidi,..ni RISK kubwa sana ku-host makundi yenye silaha.
..kwanza, Tz tulikuwa tunakaribisha mashambulizi toka kwa wareno na makaburu.
..pili, kulikuwa na hatari ya kutokea vurugu na mapigano baina ya hawa wapigania uhuru wenyewe kwa wenyewe ndani ya ardhi yetu. Zanu na Zapu toka Zimbabwe walishapata kupigana kwenye makambi yao yaliyokuwa Tanzania.
..tatu, kulikuwa na hatari ya hawa wapigania uhuru kufanya vurugu au maasi dhidi ya serikali ya Tanzania. Kuna taarifa za kihistoria za wapiganaji wa ANC kuamriwa kuondoka Tanzania kutokana na sababu za kiusalama. Rejea historia ya makao makuu ya ANC kuhama toka Tanzania kwenda Zambia. Pia rejea historia ya Yasser Arafat na PLO kuhamishwa toka Jordan kwenda Tunisia.
..Samora Machel alitwaa madaraka ya Frelimo kwasababu yeye ndiye alikuwa mkuu wa majeshi. Askari wa Frelimo walikuwa nyuma yake, na hivyo kumwezesha "kumpindua" Uria Simango ambaye alikuwa na background ya Uchungaji wa Kanisa.
..Pia kwenye bandiko lako umemuelezea Samora Machel kama "mfunga vidonda" ktk majeshi ya Frelimo. Yes, Samora Machel aliwahi kuwa muuguzi, lakini baada ya kujiunga na Frelimo alipata mafunzo ya kijeshi kwa hivyo ni askari aliyekamilika.
..Vilevile sijui kama umewahi kumuona Samora Machel au kumsikiliza. Huyu bwana alikuwa na karama ya kuzungumza na kuhamasisha. Kuna kipindi alikuja Tanzania na kuhutubia zaidi ya masaa manne na wananchi wa Dsm walitulia na kumsikiliza.
..Frelimo ilihitaji kiongozi aina ya Samora kumrithi muasisi wao, Eduardo Mondlane, ambaye aliuwawa.
Sioni ni kwa vipi amekurupuka ikiwa ameweka wazi kuwa kifo chake kina utata.Tatizo la huyu kijana mara nyingi ni ukurupukaji. Hapa ni sawa na kusema kifo cha Com. Josiah Tongogara kilipangwa na Robert Mugabe. Sina uhakika kama Yericko ana habari za Casimiro Monteiro.
Tanzania na Afrika ina tatizo kubwa la watu wake kufikiri kwa nyuzi zote 360, msamehe ndugu yetu huyoSioni ni kwa vipi amekurupuka ikiwa ameweka wazi kuwa kifo chake kina utata.
Mnajifariji gizani.Sioni ni kwa vipi amekurupuka ikiwa ameweka wazi kuwa kifo chake kina utata.
Unakusudia faraja ipi hapa kwenye jukwaa la historia?Mnajifariji gizani.
Umevuta?Unakusudia faraja ipi hapa kwenye jukwaa la historia?
I'm sorry for misplacing messageMkuu unachangia mada ipi hapa? Au umekosea kupost?
Yericko na wanajukwaa naomba tusaidiane , "Kuna uhusiano gani wa kifalsafa na utendaji kati ya CCM na FLERIMO ya sasa?" Pia izingatiwe kwamba mwaka 1976 vikosi vya Tanzania vilikuwa vimeambaa katika viunga vya Maputo na hadi mwishoni mwa 1978 ilibidi askari wa Msumbiji waje kusaidia Tanzania kupigana na Uganda kwa kile Samora alichokita kwamba anawamini askari wa Tz kulikop wa kwake ambao alitoa kikosi cha askari mia sita kusaidia vita Kagera na wengi wao walifia vitani huku.
Mmmmmmmmmmmmmmmmmh! Akhsante kwa kutoa uhusiano wa kihistoria zaidi ya nilivyouliza kuhusu uhusiano wa KIFALSAFA na UTENDAJI...mahusiano ya Frelimo na CCM hizi za sasa ni kwamba vyote ni vyama tawala ktk nchi zao. hakuna lingine.
..pia ukumbuke kwamba wakati wa vita ya ukombozi tanu na baadaye ccm vilikuwa ni vyama dola.
..kwa maana nyingine suala la kujitolea ktk vita vya ukombozi lilikuwa ni la wa-Tanzania wote ambao leo hii wengine wapo ccm, chadema, nccr, cuf, etc etc.
..Katika vita vya Kagera marafiki Algeria, Angola, Msumbiji, na Zambia ni kati ya marafiki zetu waliotusaidia kwa hali na mali. Particularly, Msumbiji walituma askari kuja kupigana bega kwa bega na askari wetu.
..Baadaye wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi Tanzania ililazimika kupeleka askari Msumbiji kusaidia ktk vita dhidi ya magaidi wa Renamo.
..Miili ya askari wetu waliokuwa wamezikwa maeneo mbalimbali Msumbiji ilirejeshwa nchini wakati wa utawala wa Mzee Mkapa na kuzikwa kwa heshima za kijeshi ktk eneo la Naliendele Mtwara. Majuzi pia Raisi Kikwete alitoa nishani za "Operation safisha Msumbiji" kutambua mchango wa mashujaa wetu waliopigana dhidi ya magaidi wa Renamo.
Kwakuongeza kibwagizo nikuwa, Wamakonde hawa wa Msumbiji ndio waliofanikisha kuweka ulinzi wakati wa ujenzi wa Daraja la Kagera lililolipuliwa na majeshi ya Nduli. Ilikuwa ngumu sana kwa majeshi ya Tz kulijenga daraja hilo kwakuwa kila wakijaribu kulijenga walikuwa wanashambuliwa, mpaka walipofika wamakonde haw na kulipiga usingizi wa kitaalamu heshi la Uganda, lilipokuja kuamka asubuhi daraja lilikuwa limekamilika..mahusiano ya Frelimo na CCM hizi za sasa ni kwamba vyote ni vyama tawala ktk nchi zao. hakuna lingine.
..pia ukumbuke kwamba wakati wa vita ya ukombozi tanu na baadaye ccm vilikuwa ni vyama dola.
..kwa maana nyingine suala la kujitolea ktk vita vya ukombozi lilikuwa ni la wa-Tanzania wote ambao leo hii wengine wapo ccm, chadema, nccr, cuf, etc etc.
..Katika vita vya Kagera marafiki Algeria, Angola, Msumbiji, na Zambia ni kati ya marafiki zetu waliotusaidia kwa hali na mali. Particularly, Msumbiji walituma askari kuja kupigana bega kwa bega na askari wetu.
..Baadaye wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi Tanzania ililazimika kupeleka askari Msumbiji kusaidia ktk vita dhidi ya magaidi wa Renamo.
..Miili ya askari wetu waliokuwa wamezikwa maeneo mbalimbali Msumbiji ilirejeshwa nchini wakati wa utawala wa Mzee Mkapa na kuzikwa kwa heshima za kijeshi ktk eneo la Naliendele Mtwara. Majuzi pia Raisi Kikwete alitoa nishani za "Operation safisha Msumbiji" kutambua mchango wa mashujaa wetu waliopigana dhidi ya magaidi wa Renamo.
Ahajahahahaha.Kwakuongeza kibwagizo nikuwa, Wamakonde hawa wa Msumbiji ndio waliofanikisha kuweka ulinzi wakati wa ujenzi wa Daraja la Kagera lililolipuliwa na majeshi ya Nduli. Ilikuwa ngumu sana kwa majeshi ya Tz kulijenga daraja hilo kwakuwa kila wakijaribu kulijenga walikuwa wanashambuliwa, mpaka walipofika wamakonde haw na kulipiga usingizi wa kitaalamu heshi la Uganda, lilipokuja kuamka asubuhi daraja lilikuwa limekamilika