Utata wa maamuzi: Nimeona elfu mbili nje barabarani na mimi niko kwenye hiace

Utata wa maamuzi: Nimeona elfu mbili nje barabarani na mimi niko kwenye hiace

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Nilikuwa ndani ya hiace, tukawa tumesimama kwenye mataa round about, nilikuwa seat ya mwisho dirishani, ghafla kutazama mbele kidogo pembezoni mwa barabara, kulikuwa na elf 2, ndani ya hice watu wamejaa sana, nimeshindwa kumwambia mtu yeyote mpaka tukaondoka.

Je, ungekuwa wewe ungefanyaje na home au getho una elf 1 tu ya tahadhari?
 
simpo ungetokea dirishani ukapanda gari jingine, net profit ingekua 2000-400=1600 kubwa sana hiyo mkuu vyuma vimekaza
 
simpo ungetokea dirishani ukapanda gari jingine, net profit ingekua 2000-400=1600 kubwa sana hiyo mkuu vyuma vimekaza
Hiyo ingeweza kuwa tofauti.... Ile anashuka tu na gari ina ondoka, ile unaanza kuikaribia ghafla imeokotwa hapo ndo utajua chocho zote za kufika unapo kwenda...
 
Mimi iliwahi kunitokea ila pembeni kulikua na jamaa muuza maji nikampigia mruzi nikamuonyeshea chini akaikota akatupia jicho kwenye gari akanionyeshea dole gumba na mimi nikamuonyeshea dole gumba tukatabasamu ile nashusha tu mkono chini gari zikaruhusiwa.Hakika nilisikia faraja sana moyoni,nilikua na stress lakini zote ziliisha ghafla na mwili wangu ukawa mwepesi kana kwamba nilibeba mzigo mzito sana halafu nikautua.Jambo hili ni moja katika wema nilioufanya duniani ambao nitaukumbuka katika maisha yangu.Hii ilitokoea mataa ya magomeni upande wa magomeni mikumi usawa wa ile Hotel
 
Hiyo ingeweza kuwa tofauti.... Ile anashuka tu na gari ina ondoka, ile unaanza kuikaribia ghafla imeokotwa hapo ndo utajua chocho zote za kufika unapo kwenda...
hahahaha
 
Ningeruka.

Kuna siku nilimpa konda mia tano akasahau kunipa mia yangu nikashuka gari ikaondoka.
Nilivyokumbuka nikakamata boda fasta kuikimbiz gari.
Boda boda nikampa buku jero konda akanipa mia yangu.
Badae nilijiona mjjinga sana
[emoji23][emoji28][emoji23]
 
Nilikuwa ndani ya hice, tukawa tumesimama kwenye mataa round about, nilikuwa seat ya mwisho dirishani, ghafla kutazama mbele kidogo pembezoni mwa barabara, kulikuwa na elf 2, ndani ya hice watu wamejaa sana, nimeshindwa kumwambia mtu yeyote mpaka tukaondoka.

Je, ungekuwa wewe ungefanyaje na home au getho una elf 1 tu ya tahadhari?
kwenye mataa round about!!! [emoji20]
 
Ningeruka.

Kuna siku nilimpa konda mia tano akasahau kunipa mia yangu nikashuka gari ikaondoka.
Nilivyokumbuka nikakamata boda fasta kuikimbiz gari.
Boda boda nikampa buku jero konda akanipa mia yangu.
Badae nilijiona mjjinga sana
Duuuuhhh heshima yako
 
Hela hizi!!, zinasababisha tuamue maamuzi ya ajabu!
Nilikuwa nakojoa kwenye choo cha umma, nauli ikadondoka kutoka kwenye mfuko wa shati, kwa sababu hela ilikuwa ni hiyohiyo tu, nikaingiza mkono kwenye mfereji wa mkojo kuitafuta, mkono wa kushoto nikaona unanichelewesha, nikaingiza mkono wa kulia kuanzia mwanzo wa mfereji hadi mwisho wa mfereji, sikuiona.
Siku hiyo nilitembea kwa miguu kutoka Posta mpaka Kiwalani!
 
Ilikuwa jero nini?
 
Back
Top Bottom