Sawa nusu ni letuNusu yake ni sehemu ya Tanzania na nusu ni sehemu ya Malawi.
Wamalawi waliingia mitini waliikacha kesi mahakamani. Mpaka ni katikati ya Ziwa, hizi habari nyingine zichukulie kuwa ni za uzushi.Mipaka ya Kiafrika haikugawanywa kwa kutumia sense. Kama ingekuwa hivyo, kusingekuwepo Wamasai pande za Tz na Kenya.
Kwa kutumia sense, Wahaya wangekuwa sehemu ya Uganda maana lugha yao inasikilizana na Kiganda na Kinyankole kuliko Kiha au Kisukuma lugha za jirani kwa huku Tanzania.
Tukipeleka sense mahakama ya kimataifa Malawi wakapeleka mikataba na wakaita wakoloni walioisaini then hapo tutaambulia sifuri. Tutaambiwa Tanganyika tulipata uhuru mwaka 1961, aliyekabidhi uhuru alikabidhi ziwa likiwa Malawi.
Kama tunabisha basi na kwanini mfano Karagwe isiwe sehemu ya Rwanda na wao wakiamua kutumia sense ya kwamba Wanyambo na Rwandese wanasikilizana.
Ni suluhisho.Kuzichapa sio suluhisho
Malawi ilishindwa sababu ni banana republic, siku wakipata serikali inayoeleweka hii kesi wanashinda na tunalazimika kuingia makubaliano mapya na compromise.Upo sawa kabisa na kwa sababu OAU iliridhia kuiheshimu mipaka ya mkoloni ni sawa. Lakini pia kama kesi ingekuwa rahisi pasipo kuangalia factors nyingine, malawi ingeshinda hiyo kesi asubuhi Ila kwa sababu kuna factors zingine. Sio rahisi hilo kutimia
Mfano Tanzania ikikubali hilo, watawezaje kudefine mipaka ya ziwa na pwani na vipi kuhusu watanzania wanaoishi maeneo ya karibu. Watakuwa na rights gani dhidi ya ziwa
Na vipi Tanzania ikikubali na kuamua kutengeneza ziwa la kutengeneza kwa kuidirect mito yote inayofeed ziwa nyasa . Je uhai wake itakuwaje
Kiuhalisia sioni Tanzania ikikubali hilo, kwa sababu sheria ya ugawaji wa maeneo haikuzingatiwa toka mwanzo lakini pia sheria ya umoja wa mataifa kwa mipaka sidhani kama itazingatiwa lakini kikubwa zaidi ni welfare ya wanyasa wenyewe
Mwalimu Nyerere na mzee Banda waliikuta mikataba ambayo hadi leo ipo, hakuna haja ya kuwafufua.Wakamfufue Mwalimu Julius Nyerere na Kamuzu Banda kama mashahidi mahususi waliochukua nchi zetu kutoka kwa wakoloni ili kesi iishe,porojo porojo za google map hazitusaidii chochote zaidi ya magomvi.
Mkuu tunaweza kupata hiyo makala ya MH Hamza JohariFatuma Karume alikuja na upotoshaji sawa na huu wa kwako mwaka ule wa 2013. Hamza Johari akaandika makala kwenye gazeti moja la kingereza na ikampa umaarufu miongoni mwa jamii ya wanasheria wa Tanzania.
Ukawa ni mwanzo wa kuwa karibu na utendaji wa kiserikali akiwa ni mshauri wa ikulu kwenye masuala mengi.
Akahusishwa katika shughuli nzima ya kisheria ya kuuhakikisha mpaka unarudi katikati ya maji ya ziwa Nyasa, Hamza na wasaidizi wake walikwenda mpaka Ujerumani kwenye kavazi za kihistoria.
Ilikuwa ni vita kubwa ya kisheria na mwisho wa yote wanasheria wa Malawi waliingia mitini na kesi haikufika mwisho hivyo serikali inayo haki ya kusambaza hilo tangazo kwa wanafunzi wa miaka hii ya sasa na kuendelea.
Hicho unachojua umeambiwa na nani?Sisi tunachojua mpaka uko kati kati ya ziwa hizo porojo zako za Google maps wapelekee wachambawima wenzako
😆😆😆😆😆Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Mazungumzo baina ya Tanzania na Malawi yafanyike. Au status quo ibaki hivihivi tunatumia bila shida wala ugomvi.Wewe Kwa akili yako mpaka sasa hivi unaonaje kiongozi,Kuhusu hili swala la ziwa Nyasa lifike mpaka kwenye ardhi yetu afu tusiwe na hata chembe ya umiliki alafu ukiuangalia vyanzo vingine vya maji vinavyo husisha nchi zaidi ya moja mpaka wa nchi hizo huwa unasoma ndani ya maji ya chanzo husika Cha maji.?
Hata kama tukikubari mipaka ya kikoloni ndio itumike lakini Kunasehemu lazima tutumie uelewa wetu kutatua migogoro mfano hasa kwenye ishu Kam hii ya maziwa na vyanzo vingine vya maji vilivyo mipakani.( Mimi naona itakuwa jambo la ajabu ziwa liguse sehemu tatu zijulikanazo kama nchi afu nchi moja ijipe umiliki waziwa lote
Usikute mjerumani alikubali ziwa liwe kwaupande wa Lawi tu kwasababu ya mapatano Yao yakipindi hicho Cha ukoloni kwamba Kila mzungu apate(hawakuwa na hasara sana maana wao wamekuja kutafuta Mali na Kila mtu apate Ili tu wapunguze migogori huko kwao ulaya.)
Ramani yako inaonyesha hivyo hivyo hata kwa ziwa TanganyikaWamalawi si wajinga kama tunalitaka hilo Ziwa tulinunue sasa..ramani ya mjerumani ambaye ndio alionganisha makabila yote akaitengeneza Tanganyika inaonyesha ziwa Nyasa halipo kwetu, kuna agenda gani nyuma ya hili ?
View attachment 3183845
Hakuna nchi inayojimilikisha. Nani alikupa mipaka ya Tanganyika unayotumia leo, nani alikupa 51% ya ziwa Victoria na akawapa Kenya 6%?Hilo ziwa haiwezekani nchi moja kujimilikisha lote ilihali na raia wetu wanalitumia kwa sababu za kiuchumi na kimaisha...eti kisa mkataba wa mkoloni....
We huoni pia Burundi na Rwanda ni sehemu ya TanganyikaWamalawi si wajinga kama tunalitaka hilo Ziwa tulinunue sasa..ramani ya mjerumani ambaye ndio alionganisha makabila yote akaitengeneza Tanganyika inaonyesha ziwa Nyasa halipo kwetu, kuna agenda gani nyuma ya hili ?
View attachment 3183845
Asa nawe jamaa una akili gani, watu wanakimbia Congo sababu ya machafuko afu unataka na kambi za wakimbizi ziwepo hapo Congo, kwann Kambi za wakimbizi wa Syria zilikuwepo kusini mwa TurkiyeUnadhani kwanini makambi ya wakimbizi ya Congo yapo Tanzania?
We mkimbizi rudini kwenu NYASA mmezamia ZanzibarSerikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Wapumbavu hawa wameanza kujisahauDuh!! Mmeanza kuingilia internal affairs za Tanganyika??!!!
Mada ni kubwa kuliko mtoa mada, ni wa kumpuuza.Umeshiba makande wewe. Kama kuna siku niliwahi kumuelewa Mzee Jakaya ni siku alipoelezea historia ya huu mgogoro. Lazima tuwafundishe watoto wetu, kwani sababu mzito za kihistoria na za kisasa zipo kwanini mpaka uwe katikati. Yaani Google map ikisema Mt.Kilimanjaro ipo Kenya na sisi tuufyate siyo?