Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

My apologies if this just so happens to be an incorrect prejudice, ila username yako inasadifu uzi wako. Ama ni kutokujua sheria za kimataifa za mipaka? Ikitokea nchi zinapakana kwenye chanzo cha maji (isipokuwa bahari), mpaka ni nusu ya chanzo hicho. Hivyo ndivyo nijuavyo. Nadhani mambo ya Tanganyika ungetuachia waTanganyika tu kiongozi.
 
Mipaka ya Kiafrika haikugawanywa kwa kutumia sense. Kama ingekuwa hivyo, kusingekuwepo Wamasai pande za Tz na Kenya.

Kwa kutumia sense, Wahaya wangekuwa sehemu ya Uganda maana lugha yao inasikilizana na Kiganda na Kinyankole kuliko Kiha au Kisukuma lugha za jirani kwa huku Tanzania.

Tukipeleka sense mahakama ya kimataifa Malawi wakapeleka mikataba na wakaita wakoloni walioisaini then hapo tutaambulia sifuri. Tutaambiwa Tanganyika tulipata uhuru mwaka 1961, aliyekabidhi uhuru alikabidhi ziwa likiwa Malawi.
Kama tunabisha basi na kwanini mfano Karagwe isiwe sehemu ya Rwanda na wao wakiamua kutumia sense ya kwamba Wanyambo na Rwandese wanasikilizana.
Wamalawi waliingia mitini waliikacha kesi mahakamani. Mpaka ni katikati ya Ziwa, hizi habari nyingine zichukulie kuwa ni za uzushi.
 
Mtoa Mada naona unawathamini sana Wakoloni na kuona maamuzi yao ndio sahihi.

Kama ni hivyo warudishie Waarabu kisiwa chao cha Zanzibar na muendelee kuwa Watumwa kama walivyo amua Waarabu.
Wewe bado una fikra ya kuwa Mtumwa.

Wanyasa wa Tanganyika walikuwa wanalitumia Ziwa Nyasa kama raslimali yao halari ya asili bila bugdha yoyote ile kabla hata ya kuja huyo Mkoloni wako, na Kabla ya kuja kwa yule anaye kujaza ujinga mwingi kichwani na kukabwa na kupigwa kule Pangoni na Ibirisi.
 
Upo sawa kabisa na kwa sababu OAU iliridhia kuiheshimu mipaka ya mkoloni ni sawa. Lakini pia kama kesi ingekuwa rahisi pasipo kuangalia factors nyingine, malawi ingeshinda hiyo kesi asubuhi Ila kwa sababu kuna factors zingine. Sio rahisi hilo kutimia

Mfano Tanzania ikikubali hilo, watawezaje kudefine mipaka ya ziwa na pwani na vipi kuhusu watanzania wanaoishi maeneo ya karibu. Watakuwa na rights gani dhidi ya ziwa

Na vipi Tanzania ikikubali na kuamua kutengeneza ziwa la kutengeneza kwa kuidirect mito yote inayofeed ziwa nyasa . Je uhai wake itakuwaje

Kiuhalisia sioni Tanzania ikikubali hilo, kwa sababu sheria ya ugawaji wa maeneo haikuzingatiwa toka mwanzo lakini pia sheria ya umoja wa mataifa kwa mipaka sidhani kama itazingatiwa lakini kikubwa zaidi ni welfare ya wanyasa wenyewe
Malawi ilishindwa sababu ni banana republic, siku wakipata serikali inayoeleweka hii kesi wanashinda na tunalazimika kuingia makubaliano mapya na compromise.

Status itabaki hivi endapo Nyasa hamna gesi au mafuta, siku zimetokea malighafi humo tutabishana. Ikitokea ni maji tu basi wanaweza ruhusu tutumie au tuvue samaki.

Na kisheria za kimataifa, ni marufuku kuzuia chanzo cha asili cha maji kisielekee nchi nyingine. That's an act of war.

Nigeria kwenye Niger Delta wana mabwawa ya umeme kama Kainji ambayo maji yake yanatokea nchini Niger. Nigeria ililazimika kuipa umeme Niger ili nayo isijenge bwawa kwake ambalo litazuia maji. Kwenye HEP station angalau mtazozana, sasa kwenye hamna eti Tz tuzuie maji yasiende Nyasa sijui yakalete mafuriko wapi lazima kimataifa tuonekane na makosa makubwa.
 
Wakamfufue Mwalimu Julius Nyerere na Kamuzu Banda kama mashahidi mahususi waliochukua nchi zetu kutoka kwa wakoloni ili kesi iishe,porojo porojo za google map hazitusaidii chochote zaidi ya magomvi.
Mwalimu Nyerere na mzee Banda waliikuta mikataba ambayo hadi leo ipo, hakuna haja ya kuwafufua.

Iddi Amin alikuwa na sababu hafifu za kuidai Kagera salient, mipaka ya nchi kitaratibu inagawanywa kwenye natural obstacle. Na pale obstacle ni mto Kagera, na sehemu ile inaingiliana na Uganda zaidi kuliko Tanzania. Ila kimkataba wa kikoloni wao walichora mstari kwa rula. Basi iko hivyo anayebisha analeta ugomvi.

Ni makosa yalifanyika na wakoloni, na founding fathers wa OAU waliyajua makosa hayo ila wakaona muda utakaotumika kupigana na kubishana hauna manufaa. Kila nchi ina claim, na zipo nchi zaidi ya 50.
 
Fatuma Karume alikuja na upotoshaji sawa na huu wa kwako mwaka ule wa 2013. Hamza Johari akaandika makala kwenye gazeti moja la kingereza na ikampa umaarufu miongoni mwa jamii ya wanasheria wa Tanzania.

Ukawa ni mwanzo wa kuwa karibu na utendaji wa kiserikali akiwa ni mshauri wa ikulu kwenye masuala mengi.

Akahusishwa katika shughuli nzima ya kisheria ya kuuhakikisha mpaka unarudi katikati ya maji ya ziwa Nyasa, Hamza na wasaidizi wake walikwenda mpaka Ujerumani kwenye kavazi za kihistoria.

Ilikuwa ni vita kubwa ya kisheria na mwisho wa yote wanasheria wa Malawi waliingia mitini na kesi haikufika mwisho hivyo serikali inayo haki ya kusambaza hilo tangazo kwa wanafunzi wa miaka hii ya sasa na kuendelea.
Mkuu tunaweza kupata hiyo makala ya MH Hamza Johari
 
Sisi tunachojua mpaka uko kati kati ya ziwa hizo porojo zako za Google maps wapelekee wachambawima wenzako
Hicho unachojua umeambiwa na nani?
Kama uliambiwa na serikali ya CCM kupitia matamko yao au shuleni ulipokuwa ukisoma, basi piga piga kifua chako kwa kujiamini huku ukijisemea mwenyewe wewe ni mjinga kabisa!

Google map ni sehemu tu ya kupata taarifa za kiramani, na taarifa zao wanazitafuta kutoka vyanzo rasmi mbali mbali vyenye kueleweka na kukubalika na mamlaka za kiulimwengu.
 
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
😆😆😆😆😆
 
Wewe Kwa akili yako mpaka sasa hivi unaonaje kiongozi,Kuhusu hili swala la ziwa Nyasa lifike mpaka kwenye ardhi yetu afu tusiwe na hata chembe ya umiliki alafu ukiuangalia vyanzo vingine vya maji vinavyo husisha nchi zaidi ya moja mpaka wa nchi hizo huwa unasoma ndani ya maji ya chanzo husika Cha maji.?

Hata kama tukikubari mipaka ya kikoloni ndio itumike lakini Kunasehemu lazima tutumie uelewa wetu kutatua migogoro mfano hasa kwenye ishu Kam hii ya maziwa na vyanzo vingine vya maji vilivyo mipakani.( Mimi naona itakuwa jambo la ajabu ziwa liguse sehemu tatu zijulikanazo kama nchi afu nchi moja ijipe umiliki waziwa lote

Usikute mjerumani alikubali ziwa liwe kwaupande wa Lawi tu kwasababu ya mapatano Yao yakipindi hicho Cha ukoloni kwamba Kila mzungu apate(hawakuwa na hasara sana maana wao wamekuja kutafuta Mali na Kila mtu apate Ili tu wapunguze migogori huko kwao ulaya.)
Mazungumzo baina ya Tanzania na Malawi yafanyike. Au status quo ibaki hivihivi tunatumia bila shida wala ugomvi.

Ila Tanzania kulazimisha au kujiaminisha ziwa nusu liwe lake kisheria haiko na back up. Maana Malawi wala Tanganyika sio zilizogawa mipaka. Hata Kenya wangependa kuwa na eneo kubwa la ziwa Victoria ila waliambulia kaeneo kadogo 6%, Uganda 43% wakati Tanzania ina nusu nzima 51%.

Sasa Kenya waje hapa walazimishe ziwa ligawanywe kwa 33% kwa nchi tatu itakuwaje?

Ziwa Tanganyika 45% Congo, 41% Tanzania, 8% Burundi na 6% Zambia. Zambia na Burundi nazo zilalamike zitake mgawo sawa?

Tanzania kuna sehemu nyingi imependelewa kuliko kupunjwa. Thats life huwezi pata kila kitu.
 
Hilo ziwa haiwezekani nchi moja kujimilikisha lote ilihali na raia wetu wanalitumia kwa sababu za kiuchumi na kimaisha...eti kisa mkataba wa mkoloni....
Hakuna nchi inayojimilikisha. Nani alikupa mipaka ya Tanganyika unayotumia leo, nani alikupa 51% ya ziwa Victoria na akawapa Kenya 6%?
Huyohuyo ndio aliipa Malawi ziwa lote.

Ukisema wanajimilikisha basi na Kenya iseme tunajimilikisha mlima Kilimanjaro na Uganda iseme tunajimilikisha bandari nyingi wakati yenyewe haina.
 
Unadhani kwanini makambi ya wakimbizi ya Congo yapo Tanzania?
Asa nawe jamaa una akili gani, watu wanakimbia Congo sababu ya machafuko afu unataka na kambi za wakimbizi ziwepo hapo Congo, kwann Kambi za wakimbizi wa Syria zilikuwepo kusini mwa Turkiye

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Dunia imechangamka currently,Mara ukraine,Mara Palestina,Mara congo,Sudan, Syria n.k
Na sisi kupitia lake nyasa dispute "tuwachangamshe" wamalawi.
 
We mkim
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
We mkimbizi rudini kwenu NYASA mmezamia Zanzibar
 
Umeshiba makande wewe. Kama kuna siku niliwahi kumuelewa Mzee Jakaya ni siku alipoelezea historia ya huu mgogoro. Lazima tuwafundishe watoto wetu, kwani sababu mzito za kihistoria na za kisasa zipo kwanini mpaka uwe katikati. Yaani Google map ikisema Mt.Kilimanjaro ipo Kenya na sisi tuufyate siyo?
Mada ni kubwa kuliko mtoa mada, ni wa kumpuuza.
 
Back
Top Bottom