Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu


Katika Mipaka ya Holigoland treaty Rwanda na Burundi pamoja rasi ya Cabo Delgado zipo ndani ya Tanganyika. Kwa hiyo tuanze kudai hayo maeneo yetu yarudi ndani ya Tanganyika siyo?
 
Mkuu tunaweza kupata hiyo makala ya MH Hamza Johari
Duh, huu ni mtihani zaidi ya miaka 10 imeshapita. Ni ya mwaka 2013 iliandikwa baada ya Fatuma Karume kuilisha matango pori jamii ya Watanzania akisema kwamba mpaka ni pembeni ya Ziwa akimaanisha Ziwa lote ni mali ya Malawi.
 

Upo sawa kabisa, sipo aware sana na international laws lakini najua fika hizo claims za malawi kuchukua ziwa nyasa zina contradiction kuanzia kwenye mkataba wa mwanzo ambao hakufuata makubaliano ya mgawanyo wa mipaka,

The same system and laws ambazo zinatumika leo hii kutafsiri mipaka ya nchi kiasi kwamba malawi kuchukua ziwa zima itakuwa ni exceptional case ambayo imetengenezwa katika udhaifu wa makubaliano ya mwanzo yasiyojali welfare au hata cultural distinctions za wakazi husika.

Upo sawa kisheria lakini malawi akipewa Ziwa usidhani kutakuwa kuna diplomatic relations nzuri and actual war haitoepukika, unless malawi ipate akili ya kutoa ushirikiano kwenye matumizi ya Ziwa ambayo nayo ni kazi kubwa.

Kuhusu kuzuia maji kuna njia nyingi ikiwemo hiyo dam kwa sababu unajua fika bwawa la Nyerere limeleta impact gani haswa kwenye drainage system nzima. Kwa hiyo Tanzania iliyojipiga kifua kutumia maji ya Ziwa Victoria ndio hiyo hiyo itatumia maji yake itakavyoona inafaa
 
Sawa ila kunamaeneo mengine kutokana na mpaka wa ki-ardhi nadhani umefanya Tanzania kuchukua eneo kubwa kiasi kwenye maziwa

Mfano muundo wa ziwa Tanganyika na nchi zilizoizunga hilo ziwa kutokana namipaka mama ya kiardhi imefanya Zambia na Burundi kupata asilimia ndogo pia Kwa Kenya mpaka wa ardhi umenyima umiliki wakupata asilimia kubwa na hivyo hivyo Tanzania pia ingepata asilimia ndogo kwenye ziwa Nyasa kutokana na mpaka wa ardhi.

Ila tukisema tubaki hivi hivi kuwa mpaka wa ziwa Nyasa huishie pwani ya Tanzania lakini tulitumie ziwa hilo pasipo kutanabaisha mipaka hapo tunakuwa tunawasikilizia Wamalawi kuamua upepo wamatumizi ya ziwa uende vipi nahisi kama tutakuwa watumwa hivi na wanyonge kwenye maamuzi.

Mimi naona mipaka inayohusu maji tukiichukulia kuanzia kwenye mipaka ya ardhi tukafanyia makadirio ya kuiingiza kwenye ziwa au mto unagusa nchi zaidi ya moja,tunaweza tukaitatua migogoro tukandoe vinyongo.
 
Na Wangoni pia wapi pande zote za Tanzania na Malawi.
 
Tatizo ni wazungu kwenye heligoland treaty ndo walifuta huo mpk ambao walisema malawi wachukue jurisdiction ya ziwa lote ambapo mwaka 1967 ndo ugomvi ulianza wakashindwa kupatana ila ugomvi ulipamba moto 2012 malawi walivyoanza uchimbaji wa mafuta ambapo serikali ya Tanzania wakasema isitishwe mpk ugomvi uishe wangekuwa na busara wangekubaliana ila sasa ziwa lina faida sana ndo.maana ugomvi ila kwa mozambique hawana ugomvi walieka border 1954 katika mkataba wa uingereza na wareno.
Cha kuongezea ziwa likiwa malawi.linaitwa lake malawi,tanzania.lake nyasa na likiwa msumbiji linaitwa lake niassa
 
Mbona hujatoa/onyesha uthibitisho wa hoja yako? lete chanzo/support cha hoja yako na siyo maneno yako tu.
 
U Universal law inasema " mpaka wa kwenye maji ziwani ni KATIKATI ya ziwa husika.
 
Mlima Kilimanjaro ni ardhi hiyo sio maji

Ila tukisema tufumue mipaka mpaka ya ardhi mambo yatakuwa mengi na itabidi tufuate makabila yaliyo mipakani ya nayo ingia nchi zaidi ya moja ili yakae kwenye nchi moja,maana hapo tutakuwa hatuitaki kabisa mipaka ya kikoloni tutakuwa tunaitakamipaka yetu sisi wenyewe tutayoiweka.
 
Ukweli usemwe na sio kupotoshwa.
Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kisheria, Tanzania mpaka leo tunaendelea kudai haki ya kudhurumiwa kupata sehemu ya ziwa. Hicho ndio google map wamefanya.
Toa sababu za msingi za kisheria kuonyesha mpaka ulioonyeshwa na Google map ni sahihi kuliko ule ulioonyeshwa na JMT.
 
Ni kweli kabisa ila hapo mwishoni nitakupinga sasa una train navy kwa ajili ya air force??
 
Mnavyobwabwaja huku kama vile nyie ndo mmepewa mamlaka na Mungu ya kuamuliwa wazawa walikuwa wakitumia hayo maji tangu Asili
 
Wewe ni Mjinga wa mwisho Popoma mkubwa, usiyejitambua.

Sheria za kimataifa, International territorial water,b

When countries separated with water bodies, mpaka wake ni katikati.

Kwa sababu maji ni uhai!!, kama akili zako za kuvukia barabara zingetosha ungejiuliza kwanini ziwa nyasa upande wa msumbiji Wewe unafikiri KIJINGA!! wakati wa kuabudu Sheria za wakoloni zimepita!!


Unafikiri Ethiopia ni wajinga waliojenga Hydro Electric power kubwa sana, kwa maji ya mto Nile??
Angetaka kufuata Sheria za wakoloni kwa ajili ya Matumizi ya maji ya moto Nile unafikiri angejenga???

Lowasa alikuwa Mjinga alipofanya project kubwa ya maji Toka ziwa Victoria to KAHAMA??? alipokuwa waziri wa maji?

think big, acha kuabudu Sheria za mizimu ya kikoloni!
 
Hivi Nyerere alipopewa nchi na Waingereza mwaka 1961 hawakumpa documents zinazoonyesha mipaka ya nchi wanayompa? Maana Tz imepata uhuru 1961. Malawi 1964. Wakati wanatupa uhuru walitupa nchi gani? Maana kesho Zanzibar watadai km 16 za pwani ya Tz. Pengine ndiyo anachotaka ASP😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…