Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Hapaja tokea kiongozi yeyote, na sidhani kuna siku moja atatokea kiongozi atakaye kubali kugawa sehemu ya nchi hii kwa nchi nyingine eti "sheria" ambayo hatukushirikishwa kuitunga, inasema hiyo sehemu ya nchi yetu.
Siku hiii ya leo hatuwezi kuendelea kulazimishwa na hao wakoloni tufuate matakwa yao hata katika mambo ambayo yapo wazi kama hili la mpaka unao tenganisha nchi hizi mbili.

Kama unataka kufuata "sheria" za kijinga jinga kama ile ya Misri kuhodhi matumizi ya maji, ambayo hayazalishwi kwao, hilo wengine walisha likataa siku nyingi.

Kamwe, haiwezekani kwa watu wetu waishio pembezoni mwa ziwa, kila wanapo taka kufanya shughuli zao za maisha wakatafute ruhusa toka nchi nyingine; hili hata siku moja halitawezekana, na hakuna sheria itakalo lazimisha hilo.

Hizi sheria unazo zipa umuhimu wewe hapa; za hao wakoloni; hebu kawaulize matatizo waliyo wasababishia wapalestina na sheria zao hizo!
 
Historia chafu, ya ujanja ujanja na uongo nilijifunza darasani hapa hapa Tanzania tangu darasa la tatu mpaka kidato cha nne, baada ya hapo historia halisi nimejifunza darasani Ulaya, mitandaoni, machapisho, majarida ya kimataifa na kupitia wageni mbali mbali kutoka nje.

Jina rasmi la ziwa Nyasa kwenye umoja wa mataifa na kielimu ulimwenguni ni Ziwa Malawi, ziwa Nyasa ni jina la kale ambalo wamiliki wake walilifuta, Tanzania pekee tukagoma kulifuta.

Mozambique walipata sehemu ya umiliki wa ziwa Nyasa kupitia mkataba baina ya Waingereza (wakoloni wa Malawi) na Wareno (wakoloni wa Mozambique) kwa kubadilishana na visiwa viwili vilivyopo Mozambique. Hili lipo wazi kwa msome yoyote wa historia ya ukoloni hapa Afrika.
 
Ni dhahiri kabisa, badala ya elimu hiyo kukusaidia kupanua uwezo wako wa kutambua mambo; badala yake ikakugeuza kuwa mtu wa kuimba kama santuri vile, na nyimbo zenyewe wakizitunga hao hao walio kufundisha.

Maana ya "elimu" umeigeuza kabisa, na kuwa kujazwa ujinga ili uendelee kuamini kila kitu unacho kisikia toka kwa hao hao uliotakiwa kujifunza kutumia akili yako mwenyewe badala ya kutegemea uliyo jazwa kichwani.

Nasikitika sana kwa kuyasema haya, kwa mtu kama wewe, ambaye siku zote nimekuwa nikidhani ana upeo wa kutosha kujisimamia mwenyewe.
 

Jina rasmi la ziwa Nyasa kwenye umoja wa mataifa na kielimu ulimwenguni ni Ziwa Malawi, ziwa Nyasa ni jina la kale ambalo wamiliki wake walilifuta, Tanzania pekee tukagoma kulifuta.
Ila kwenye mzozo wa mashariki yakati pia Huwa na sikia unatumika ushahidi wakale mno enzi za akina edomu(Esau) na Yakobo yani hapo kabla hata Israel haijaitwa Israeli.
 
Jina rasmi la ziwa Nyasa kwenye umoja wa mataifa na kielimu ulimwenguni ni Ziwa Malawi, ziwa Nyasa ni jina la kale ambalo wamiliki wake walilifuta, Tanzania pekee tukagoma kulifuta
Hakuna kitu kama "mmiliki" wa ziwa. Hili ziwa halipo Malawi pekee; kwa nini wawe wamiliki?
 
Asante kwa kunishtumu mimi binafsi.
Pole kwa kushindwa kujibu hoja za hii mada.
 
Amekosa uzalendo, duniani bila akili unakosa hata kipande kidogo Cha aridhi
 
Huo mkataba nani aliusaini. Je chief mkwawa , au chief merere wanajua?
 
Hili hapa ni wazi lina kudhalilisha mwenyewe, ukilifikiria kwa makini. Siyo swala la kujivunia hata kidogo kuonyesha kuwa umesoma na kuelimika. Na hili hapa chini, linakuonyesha kuwa hao wakoloni unao dhani wao walikuwa na akili nzuri; kwani inaonyesha jinsi walivyo kuwa watupu sana kichwani walipo kuwa wakigawa hizi sehemu.
Ujuha wao ni kutojuwa kwamba mstari katikati ya ziwa toka juu hadi chini ndiyo ilikuwa njia sahihi ya mpaka katika ziwa hilo.
Sasa hadi karne hii unapoona ujinga ulio fanyika na bado ukashindwa kutambua kilicho sahihi; hiyo elimu unayo dai kuipata itakuwa ni ya manufaa gani!

Nikukumbushe tu, ujinga wa hao watu wako hadi leo ndio unao wasumbua wapalestina; ujinga huo huo, ndio unao tuhimiza tusitumie maji yanayo tiririka kwenga Misri; na kwa bahati mbaya sana, hiyo elimu waliyo kujaza wewe akilini inakulazimisha ukubaliane na ujinga huu!
 
Pole kwa kushindwa kujibu hoja za hii mada.
Sioni popote nilipo shindwa kujibu hoja hata moja. Unayo tetea wewe ni mambo batili bayana.

Imenididi nikuseme wewe binafsi, kwa sababu umejiweka katika utetezi kwa elimu uliyo pewa na hao walio kupotosha.
Historia ya jina "Malawi" ni ya jiuzi juzi tu, lakini hata yenyewe unaichukulia kuwa nzito ya kuisoma kimataifa , kana kwamba nchi ya Malawi imekuwa na umuhimu wa kipekee sana!
 
 
Hakuna kitu kama "mmiliki" wa ziwa. Hili ziwa halipo Malawi pekee; kwa nini wawe wamiliki?
Malawi walimilikishwa ziwa na wenye ziwa (wakoloni wa uingereza) kama ilivyo Tanzania tulivyomilikishwa nchi kubwa na wenye nchi yao (wakoloni wa uingereza). Hivyo ni kawaida kabisa.
 
Malawi walimilikishwa ziwa na wenye ziwa (wakoloni wa uingereza) kama ilivyo Tanzania tulivyomilikishwa nchi kubwa na wenye nchi yao (wakoloni wa uingereza). Hivyo ni kawaida kabisa.
Na bado unafikiri Malawi na Tanganyika ni mali zao, au siyo?
Walipo fanya makosa ya wazi, kuwanyima haki waTanganyika kutumia ziwa walilo zoea siku zote kuwa ni sehemu yao ya matumizi tokea eneo hilo liumbwe, sasa waendelee kuheshimu ujinga huo?
Maana ya kuwa na elimu ni nini, kama haiwezi kutumika kujuwa mambo kama haya.
 
Unaiamini Google Map kweli, mpaka wetu na Malawi ni kati kati ya Ziwa Nyasa na si vinginevyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…