Hapaja tokea kiongozi yeyote, na sidhani kuna siku moja atatokea kiongozi atakaye kubali kugawa sehemu ya nchi hii kwa nchi nyingine eti "sheria" ambayo hatukushirikishwa kuitunga, inasema hiyo sehemu ya nchi yetu.2. Anayeamua mpaka uwe wapi sio mtu au nchi fulani yenyewe bali mikataba ya kimataifa ya kihistoria au kisiasa inayokubalika kiulimwengu (UN). Na hiyo ndio inatambua wazi na kutamka bayana kuwa mpaka wa Ziwa Nyasa upo pwani ya ziwa upande wa Tanzania na sio katikati ya ziwa. Mipaka karibu yote hapa Africa tumerithi kutoka kwa ukoloni, sehemu chache tumeiboresha na sehemu zingine tumeitengeneza upya kwa vita na migogoro.
Siku hiii ya leo hatuwezi kuendelea kulazimishwa na hao wakoloni tufuate matakwa yao hata katika mambo ambayo yapo wazi kama hili la mpaka unao tenganisha nchi hizi mbili.
Kama unataka kufuata "sheria" za kijinga jinga kama ile ya Misri kuhodhi matumizi ya maji, ambayo hayazalishwi kwao, hilo wengine walisha likataa siku nyingi.
Kamwe, haiwezekani kwa watu wetu waishio pembezoni mwa ziwa, kila wanapo taka kufanya shughuli zao za maisha wakatafute ruhusa toka nchi nyingine; hili hata siku moja halitawezekana, na hakuna sheria itakalo lazimisha hilo.
Hizi sheria unazo zipa umuhimu wewe hapa; za hao wakoloni; hebu kawaulize matatizo waliyo wasababishia wapalestina na sheria zao hizo!