Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

2. Anayeamua mpaka uwe wapi sio mtu au nchi fulani yenyewe bali mikataba ya kimataifa ya kihistoria au kisiasa inayokubalika kiulimwengu (UN). Na hiyo ndio inatambua wazi na kutamka bayana kuwa mpaka wa Ziwa Nyasa upo pwani ya ziwa upande wa Tanzania na sio katikati ya ziwa. Mipaka karibu yote hapa Africa tumerithi kutoka kwa ukoloni, sehemu chache tumeiboresha na sehemu zingine tumeitengeneza upya kwa vita na migogoro.
Hapaja tokea kiongozi yeyote, na sidhani kuna siku moja atatokea kiongozi atakaye kubali kugawa sehemu ya nchi hii kwa nchi nyingine eti "sheria" ambayo hatukushirikishwa kuitunga, inasema hiyo sehemu ya nchi yetu.
Siku hiii ya leo hatuwezi kuendelea kulazimishwa na hao wakoloni tufuate matakwa yao hata katika mambo ambayo yapo wazi kama hili la mpaka unao tenganisha nchi hizi mbili.

Kama unataka kufuata "sheria" za kijinga jinga kama ile ya Misri kuhodhi matumizi ya maji, ambayo hayazalishwi kwao, hilo wengine walisha likataa siku nyingi.

Kamwe, haiwezekani kwa watu wetu waishio pembezoni mwa ziwa, kila wanapo taka kufanya shughuli zao za maisha wakatafute ruhusa toka nchi nyingine; hili hata siku moja halitawezekana, na hakuna sheria itakalo lazimisha hilo.

Hizi sheria unazo zipa umuhimu wewe hapa; za hao wakoloni; hebu kawaulize matatizo waliyo wasababishia wapalestina na sheria zao hizo!
 
Mkuu 'Zanzibar ASP', hii historia wewe ulijifunzia wapi; kwamba kuna Ziwa Malawi? Umejifunzia nchi gani historia hiyo na lini?
Kwani nchi ya Malawi imekuwa Malawi lini, kabla yako kuzaliwa?
Ziwa Tanganyika lipo hapo, na lenyewe tulidai kuwa ni Ziwa Tanzania, mali ya Tanzania; au siy; kwa mujibu wa haya uliyo eleza hapa.
Hapana, ziwa kuitwa Nyasa au Malawi siyo sababu ya ziwa kuwa sehemu ya nchi yenye jina hilo.
Unasema Msumbiji walipewa? sehemu ya ziwa na Malawi...; kwa makubaliano gani? Tanzania haina sababu ya kuomba kugawiwa sehemu ya ziwa; kwa sababu sehemu hiyo kimaumbile; ndiyo kimaumbile mbali ya hizo sheria unazo zitanguliza hapa, ni eneo tambulika enzi na enzi kuwa ni sehemu ya wakazi waliokuwepo kwenye eneo hilo hata kabla Tanganyika haijakuwepo.
Hakuna sheria inayo izidi sheria ya kimaumbile kama hiyo.
Historia chafu, ya ujanja ujanja na uongo nilijifunza darasani hapa hapa Tanzania tangu darasa la tatu mpaka kidato cha nne, baada ya hapo historia halisi nimejifunza darasani Ulaya, mitandaoni, machapisho, majarida ya kimataifa na kupitia wageni mbali mbali kutoka nje.

Jina rasmi la ziwa Nyasa kwenye umoja wa mataifa na kielimu ulimwenguni ni Ziwa Malawi, ziwa Nyasa ni jina la kale ambalo wamiliki wake walilifuta, Tanzania pekee tukagoma kulifuta.

Mozambique walipata sehemu ya umiliki wa ziwa Nyasa kupitia mkataba baina ya Waingereza (wakoloni wa Malawi) na Wareno (wakoloni wa Mozambique) kwa kubadilishana na visiwa viwili vilivyopo Mozambique. Hili lipo wazi kwa msome yoyote wa historia ya ukoloni hapa Afrika.
 
Ni dhahiri kabisa, badala ya elimu hiyo kukusaidia kupanua uwezo wako wa kutambua mambo; badala yake ikakugeuza kuwa mtu wa kuimba kama santuri vile, na nyimbo zenyewe wakizitunga hao hao walio kufundisha.

Maana ya "elimu" umeigeuza kabisa, na kuwa kujazwa ujinga ili uendelee kuamini kila kitu unacho kisikia toka kwa hao hao uliotakiwa kujifunza kutumia akili yako mwenyewe badala ya kutegemea uliyo jazwa kichwani.

Nasikitika sana kwa kuyasema haya, kwa mtu kama wewe, ambaye siku zote nimekuwa nikidhani ana upeo wa kutosha kujisimamia mwenyewe.
 
Ila kwenye mzozo wa mashariki yakati pia Huwa na sikia unatumika ushahidi wakale mno enzi za akina edomu(Esau) na Yakobo yani hapo kabla hata Israel haijaitwa Israeli.
 
Jina rasmi la ziwa Nyasa kwenye umoja wa mataifa na kielimu ulimwenguni ni Ziwa Malawi, ziwa Nyasa ni jina la kale ambalo wamiliki wake walilifuta, Tanzania pekee tukagoma kulifuta
Hakuna kitu kama "mmiliki" wa ziwa. Hili ziwa halipo Malawi pekee; kwa nini wawe wamiliki?
 
Ni dhahiri kabisa, badala ya elimu hiyo kukusaidia kupanua uwezo wako wa kutambua mambo; badala yake ikakugeuza kuwa mtu wa kuimba kama santuri vile, na nyimbo zenyewe wakizitunga hao hao walio kufundisha.

Maana ya "elimu" umeigeuza kabisa, na kuwa kujazwa ujinga ili uendelee kuamini kila kitu unacho kisikia toka kwa hao hao uliotakiwa kujifunza kutumia akili yako mwenyewe badala ya kutegemea uliyo jazwa kichwani.

Nasikitika sana kwa kuyasema haya, kwa mtu kama wewe, ambaye siku zote nimekuwa nikidhani ana upeo wa kutosha kujisimamia mwenyewe.
Asante kwa kunishtumu mimi binafsi.
Pole kwa kushindwa kujibu hoja za hii mada.
 
Umeshiba makande wewe. Kama kuna siku niliwahi kumuelewa Mzee Jakaya ni siku alipoelezea historia ya huu mgogoro. Lazima tuwafundishe watoto wetu, kwani sababu mzito za kihistoria na za kisasa zipo kwanini mpaka uwe katikati. Yaani Google map ikisema Mt.Kilimanjaro ipo Kenya na sisi tuufyate siyo?
Amekosa uzalendo, duniani bila akili unakosa hata kipande kidogo Cha aridhi
 
UN wanatambua Anglo-Germany treaty kama ndio msingi wa kuelezea mpaka wa Ziwa Malawi (Nyasa). Nimeona hiyo Anglo-Germany treaty, na inasema wazi Malawi ndio wamiliki wa ziwa lote la Nyasa. Tanzania tumekuwa tukiupinga huo mkataba wa Heligoland treaty kutumika kama msingi wa kujua mpaka wa Ziwa Nyasa kwa hoja kuwa haukutenda haki, una kasoro na umekosa uhalisia (jambo ambalo hata mimi naliunga mkono kwa 100%), lakini mpaka leo hii UN haijawahi kuukataa huo mkataba wa Heligoland kutumika katika kuelezea mpaka wa ziwa Nyasa. Na hukujawahi kuwepo tena mkataba mpya wa kutambua mpaka katika ziwa hilo baina ya Malawi na Tanzania.

Mzozo uliozuka mwaka 2012 ulitokana na Malawi kutaka kuanza kuchimba mafuta katika ziwa Nyasa upande ambao Tz tunadai ni mali yetu, na Tz kutishia kuingia vitani dhidi ya Malawi, na hiyo ikapelekea Malawi kutaka kushtaki kwa kuzuiwa kutumia rasimali inazozimiliki.
Huo mkataba nani aliusaini. Je chief mkwawa , au chief merere wanajua?
 
Historia chafu, ya ujanja ujanja na uongo nilijifunza darasani hapa hapa Tanzania tangu darasa la tatu mpaka kidato cha nne, baada ya hapo historia halisi nimejifunza darasani Ulaya, mitandaoni, machapisho, majarida ya kimataifa na kupitia wageni mbali mbali kutoka nje.
Hili hapa ni wazi lina kudhalilisha mwenyewe, ukilifikiria kwa makini. Siyo swala la kujivunia hata kidogo kuonyesha kuwa umesoma na kuelimika.
Mozambique walipata sehemu ya umiliki wa ziwa Nyasa kupitia mkataba baina ya Waingereza (wakoloni wa Malawi) na Wareno (wakoloni wa Mozambique) kwa kubadilishana na visiwa viwili vilivyopo Mozambique. Hili lipo wazi kwa msome yoyote wa historia ya ukoloni hapa Afrika.
Na hili hapa chini, linakuonyesha kuwa hao wakoloni unao dhani wao walikuwa na akili nzuri; kwani inaonyesha jinsi walivyo kuwa watupu sana kichwani walipo kuwa wakigawa hizi sehemu.
Ujuha wao ni kutojuwa kwamba mstari katikati ya ziwa toka juu hadi chini ndiyo ilikuwa njia sahihi ya mpaka katika ziwa hilo.
Sasa hadi karne hii unapoona ujinga ulio fanyika na bado ukashindwa kutambua kilicho sahihi; hiyo elimu unayo dai kuipata itakuwa ni ya manufaa gani!

Nikukumbushe tu, ujinga wa hao watu wako hadi leo ndio unao wasumbua wapalestina; ujinga huo huo, ndio unao tuhimiza tusitumie maji yanayo tiririka kwenga Misri; na kwa bahati mbaya sana, hiyo elimu waliyo kujaza wewe akilini inakulazimisha ukubaliane na ujinga huu!
 
Pole kwa kushindwa kujibu hoja za hii mada.
Sioni popote nilipo shindwa kujibu hoja hata moja. Unayo tetea wewe ni mambo batili bayana.

Imenididi nikuseme wewe binafsi, kwa sababu umejiweka katika utetezi kwa elimu uliyo pewa na hao walio kupotosha.
Historia ya jina "Malawi" ni ya jiuzi juzi tu, lakini hata yenyewe unaichukulia kuwa nzito ya kuisoma kimataifa , kana kwamba nchi ya Malawi imekuwa na umuhimu wa kipekee sana!
 
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zime
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Mawimbi ya hilo ziwa yanapiga nchi gani? au tuwachaji buku kwa kila wimbi linalotua kwetu
 
Hakuna kitu kama "mmiliki" wa ziwa. Hili ziwa halipo Malawi pekee; kwa nini wawe wamiliki?
Malawi walimilikishwa ziwa na wenye ziwa (wakoloni wa uingereza) kama ilivyo Tanzania tulivyomilikishwa nchi kubwa na wenye nchi yao (wakoloni wa uingereza). Hivyo ni kawaida kabisa.
 
Na bado unafikiri Malawi na Tanganyika ni mali zao, au siyo?
Walipo fanya makosa ya wazi, kuwanyima haki waTanganyika kutumia ziwa walilo zoea siku zote kuwa ni sehemu yao ya matumizi tokea eneo hilo liumbwe, sasa waendelee kuheshimu ujinga huo?
Maana ya kuwa na elimu ni nini, kama haiwezi kutumika kujuwa mambo kama haya.
 
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Unaiamini Google Map kweli, mpaka wetu na Malawi ni kati kati ya Ziwa Nyasa na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom