Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Hana chembe hata moja ya uzalendo,Wala wawezi kuwa mzalendo,huyu ni Adui kwa asilimia 100..Huyu ni Public enemy.
 
Usiandike utoto kwenye mambo yenye maslahi mapana ya nchi...who do you want to impress.
Hakuna maslahi ya nchi kwenye kunyang'anya maeneo ya watu...tuna mapori mengi sana hatujaendeleza...ziwa Victoria tumeshindwa kuliendeleza uvuvi haramu umemaliza samaki sasa wameamua kuuzia wachina maeneo wanafuga samaki broilers...Embu kama nchi tuwe na priorities... Hata tupewe dunia nzima kwa hii tutaendelea kuwa maskini tu
 
Fatuma Karume alikuja na upotoshaji sawa na huu wa kwako mwaka ule wa 2013. Hamza Johari akaandika makala kwenye gazeti moja la kingereza na ikampa umaarufu miongoni mwa jamii ya wanasheria wa Tanzania.

Ukawa ni mwanzo wa kuwa karibu na utendaji wa kiserikali akiwa ni mshauri wa ikulu kwenye masuala mengi.

Akahusishwa katika shughuli nzima ya kisheria ya kuuhakikisha mpaka unarudi katikati ya maji ya ziwa Nyasa, Hamza na wasaidizi wake walikwenda mpaka Ujerumani kwenye kavazi za kihistoria.

Ilikuwa ni vita kubwa ya kisheria na mwisho wa yote wanasheria wa Malawi waliingia mitini na kesi haikufika mwisho hivyo serikali inayo haki ya kusambaza hilo tangazo kwa wanafunzi wa miaka hii ya sasa na kuendelea.
 
Njooni mlichukue!
 
Upo sahihi.
Ila nafikiri maridhiano ya mipaka yalifanyika kati ya serikali ya wakoloni wa kiingereza (Malawi) na kireno (Msumbiji).

Wakati wanaelekea kutaka kuridhiana kati ya Uingereza (Malawi) na Germany (Tanganyika), WWI ikawa imetokea na baadaye Malawi na Tanganyika zote zikawa chini ya UK, huku mpaka wa mwanzo uliotambulika na Heligolqnd treaty ukiwa haujabadilika. Ni mpaka huo ndio uliendelea kurithishwa kwenye mataifa huru na ndio unaofuatwa na google.

Ni ukweli unaouma.

Kimantiki kila mtu anatamani mpaka uwe katikati.
 
Ukweli usemwe na sio kupotoshwa.
Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kisheria, Tanzania mpaka leo tunaendelea kudai haki ya kudhurumiwa kupata sehemu ya ziwa. Hicho ndio google map wamefanya.

Nimejaribu kukufuatilia katika andiko hili kuhusu mpaka wa ziwa Nyasa. Lkn cha kushangaza hata hutaji kifungu (kipi) cha sheria (ipi) ya mwaka (gani) na ya (wapi). Naona tu unataja kuwa Malawi ni wamiliki kisheria lkini huoneshi kama nilivyokuuliza hapo juu.
Ikumbukwe kwamba JF imejaa wanatasnia mbalimbali hivyo unavyoleta jambo yafaa uwe umejitosheleza kihoja.
Asante kwa kutoa hoja, licha ya kuwa sikubaliani na hoja yako.
 
Pumzika Kwa Amani Laigwanan Edward Ngoyai Lowassa.
Hayati Lowassa aliingilia hili suala likiwa limeshasogea alitaka kupata umaarufu wa kisiasa.

Ni suala la Membe na Hamza Johari akiwa mwanasheria alipambana sana katika hii vita ya kurudisha mpaka wa Ziwa Nyasa na tunaweza kusema tulishinda kwani Malawi walipotea mazima.

Yule Mama Rais wao alifanya maamuzi ya kijinga kutangaza Malawi ni mmiliki wa Ziwa lote, Inashangaza kuona vibaraka wa mataifa mengine kama huyu mleta mada wakishadidia suala lenye kuonyesha ukosefu wao wa uzalendo.
 
Hilo unalolizungumza ni matatizo ya serikali na siyo nchi...ninyi watoto wa 2000 mnajifanya mnajua mambo sana kumbe ni bure kabisa...
Hapa concern yetu ni mipaka ya nchi,umesikia tuitaja CCM ama cuf au Chadema?
Hayo unayoyaongelea yanaweza kuwa solved na Serikali,who knows labda wewe unaweza ukaja kuwa Rais na kuunda serikali Yako na kufanya maziwa,mapori na bahari viwafaidie Watanzania?
Tofautisha kati ya Serikali and Nchi..
Serikali zinakuja na kwenda,lakini nchi itabaki kuwa vilevile, nchi ni urithi wetu,usituletee uchuro wako hapa.
 
Wenye majibu ni wakoloni waliotuchorea mipaka... sisi...mipaka yetu ilikua kwisho wa wasukuma, mwisho wa wachagga, wazanaki e.t.c kuna mahakama za kimataifa kazi yao ni kusupuhisha kesi zaivi
 
Malawi waliishindwa hiyo kesi katika mahakama za kimataifa,, wanasheria wao hawakujitokeza walipohitajika.

Mpaka ni nusu ya maji ya Ziwa Nyasa, Fatuma Karume aliwaingiza chaka watanzania Hamza Johari akafanya utetezi ndio maana leo hii limetolewa tangazo hilo la Serikali.
 
Poyoyo nyingi...lete minutes na mipaka ya Berlin conference tuone ziwa nyasa mwisho wake wapi...serikali ya CCM imezoeaa uongo kwenye kila kitu...na hapa usishangae wanataka ziwa wakakopee WB under an umbrella ya kuwekeza uchumi wa bluu...my foot.
 

Upo sawa kabisa na kwa sababu OAU iliridhia kuiheshimu mipaka ya mkoloni ni sawa. Lakini pia kama kesi ingekuwa rahisi pasipo kuangalia factors nyingine, malawi ingeshinda hiyo kesi asubuhi Ila kwa sababu kuna factors zingine. Sio rahisi hilo kutimia

Mfano Tanzania ikikubali hilo, watawezaje kudefine mipaka ya ziwa na pwani na vipi kuhusu watanzania wanaoishi maeneo ya karibu. Watakuwa na rights gani dhidi ya ziwa

Na vipi Tanzania ikikubali na kuamua kutengeneza ziwa la kutengeneza kwa kuidirect mito yote inayofeed ziwa nyasa . Je uhai wake itakuwaje

Kiuhalisia sioni Tanzania ikikubali hilo, kwa sababu sheria ya ugawaji wa maeneo haikuzingatiwa toka mwanzo lakini pia sheria ya umoja wa mataifa kwa mipaka sidhani kama itazingatiwa lakini kikubwa zaidi ni welfare ya wanyasa wenyewe
 
Poyoyo nyingi...lete minutes na mipaka ya Berlin conference tuone ziwa nyasa mwisho wake wapi...serikali ya CCM imezoeaa uongo kwenye kila kitu...na hapa usishangae wanataka ziwa wakakopee WB under an umbrella ya kuwekeza uchumi wa bluu...my foot.
Minutes za Berlin zinaonyesha mpaka ni katikati ya maji ya Ziwa, wanasheria walilipigania hili suala miaka ile Membe akiwa waziri wa mambo ya nje na wanasheria wa Malawi wakaingia mitini.
 
Minutes za Berlin zinaonyesha mpaka ni katikati ya maji ya Ziwa, wanasheria walilipigania hili suala miaka ile Membe akiwa waziri wa mambo ya nje na wanasheria wa Malawi wakaingia mitini.
Weka hapa tuzijadili...usiongelee vitu vya kusadikika...wanasheria wetu hao ambao kila kesi wanapigwa huko majuu...should we trust them ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…