Unajua kwamba OAU walikubaliana kuwa mipaka ya kikoloni ndio iendelee kutumika baada ya uhuru?
Yani unataka kusema kwamba nchi za Afrika tuna busara sana kwahiyo tuanze kuchora upya mipaka. Unazijua akili za Mwafrika kweli mkuu?
Yani turudie kuchora, Uganda wapendekeze kupata Kagera salient, Kenya wapendekeze kupata mlima Kilimanjaro pale ambapo ramani ilipindishwa ili mlima uwe Tanzania, Zanzibar wadai pwani ya bara maana kuna Sultan aliwahi sema anaimiliki na akiwapa Wajerumani sijui, Tanzania tudai sehemu ya Masai Mara ya Kenya ili Wamasai wote wawe Tanzania, Kenya wapendekeze waongezewe sehemu ya ziwa Victoria wawe nayo nyingi maana Tanzania imechukua kipande kikubwa zaidi, Burundi nao waombe sehemu kubwa zaidi ya ziwa Tanganyika. Hapo ni sisi tu, bado sehemu nyingine za Afrika.
Kiuhalisia ukisoma Helligoland treaty na mkataba mwingine, hakuna ushahidi unaoonyesha Tanzania tunamiliki nusu ya ziwa Nyasa. Hata Wajerumani waliokuwa wanatawaka Tanganyika ramani yao inaonyesha Nyasa nzima ni ya Malawi.
Sisi Tanzania tunakuwa na claim kuwa wazungu walikubaliana kama kuna chanzo cha maji mpakani basi kigawanywe kila nchi inayopakana ipate kiasi chake. But that wasn't the case kwa ziwa Nyasa. Tukienda mahakama ya usuluhishi, zikaletwa mikataba na mashahidi wakoloni Tanzania tunashindwa asubuhi na mapema kabisa.