We JPM alikuwa ni habari nyingine, miradi mingi ilikuwa inajengwa kwa pamoja ukijumuisha miradi mikubwa Kama Sgr na Bwawa la umeme. Barabara kila wilaya, masoko ya kisasa mikoa yote, stendi mikoa yote, vituo vya afya zaidi ya 400, zahanati zaidi ya 800, hospitali za wilaya zaidi ya 70, Hospitali za kanda 3, ujenzi wa meli mpya ziwa Victoria na ziwa Nyasa. Madaraja makubwa Kama Ubungo interchange, daraja la Salender na daraja la Busisi. Miradi ya maji mfano mradi wa maji toka ziwa Victoria kwenda Tabora. Kuhamisha makao makuu ya serikali na wizara zake kwenda Dodoma ndani ya mwaka 1.
JPM alikuwa genius katika utekelezaji wa miradi, katika miaka mitano amefanya mengi kuzidi awamu yeyote ya watangulizi wake. Tumseme kwa mengine lakini siyo swala la miradi.
Sent from my itel W6004 using
JamiiForums mobile app