Mimi nashauri kila nyumba iwe na king'ora juu ya paa ambacho kitakuwa kina sense moshi,short kikiwa connected na fire detector.
King'ora kiwa na taa kubwa kama zile za bandari ili iwe rahisi kinapolia wasamalia wema na taasisi za uokoaji kufanya mchakato wa kutoa msaada.
Kingine tuhakikishe taasisi zote hasa zinazochukua watu wengi serikali iendelee kutilia mkaazo wa wakandarasi wanaofanya wiring wawe ni wale registered na wenye sifa.
Aidha inatakiwa kila anaefanyiwa wiring aombe kibali tanesco kabla ya kuanza kufanya wiring kama utaratibu wa kuomba vibali vya ujenzi.
Natambua kuwepo utaratibu wa kupeleka michoro, lakini bado inabidi serikali iongeze meno.
Aidha serikali na tanesco wakishirikiana na taasisi zingine wafanye utafiti wa kuhusu kufanya wiring kwamba wiring zote zipite ndani ya ukuta badala ya kupitisha juu ya dali tena zikiwa loose. Ambapo ni rahisi kushika moto, na matukio yote ya moto mara nyingi huanzia dalini hasa matukio yanayotokana na short-circuit za umeme.
Vile vile serikali iiepe meno tanesco kuhakikisha jengo lolote na mtu yeyote ahakikishe awe na main switch pamoja na circuit breaker ambazo zinafanya kazi kama kujizima zenyewe pale load inapozidi au short-circuit inapotokea..
Mwishi ni muhimu sasa serikali kuweka utaratibu wa kuhakikisha kila jengo mbele yake kuwe na kisima cha maji, na hili lisimamiwe na idara za maji huku ofisi ya waziri mkuu kitengo cha uokoaji kikipewa meno ya kuwang'ata hawa idara za maji kwa kutojaza maji.
Sio lazima kila jingo lakini hii itasaidia vikosi vya uokoja kutokwenda mbali kufuata majini wao inatakiwa kuja na dawa za kutosha tu.
Sent from my Infinix X650B using
JamiiForums mobile app