SoC04 Utatuzi wa Kero ya Maji

SoC04 Utatuzi wa Kero ya Maji

Tanzania Tuitakayo competition threads

Bwana kaduga

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
863
Reaction score
1,812
Asante sana JAMII FORUMS kwa kutuletea STORY OF CHANGE.

Bila shaka viongozi wamekuwa wakisikia changamoto ya maji karibia TANZANIA nzima, ama kwa hakika TANZANIA TUITAKAYO ni ile ya viongozi kuweza kupokea malalamiko ya wananchi wao na kuitatua kwa wakati.

Tunataka nchi nzima iwe na maji ya uhakika na sio maji yapatikane mijini tu na tena upatikanaji wake ni wa mgao, maji yakitoka jumamosi hadi jumanne ndio yatoke tena hiyo sio TANZANIA TUITAKAYO.

Viongozi husika wa watatue kero za wananchi kwa wakati, wawatue mizigo raia wao unakuta sehemu za vijijini maji ni tatizo kubwa wanayatoa sehemu za mbali na kupelekea kupoteza muda mwingi kwa ajiri ya foleni.

Maji ni muhimu sana kwa binadamu hivyo kupitia vyanzo tulivyo navyo vitusaidie upatikanaji rahisi wa maji kote nchini, kupitia kodi tunazo lipa serikali iwekeze nguvu nyingi katika hili.

Nihitimishe kwa kusema TANZANIA TUITAKAYO ni ile ya kumsikiliza mwananchi wa hali yoyote.
 
Upvote 1
Maji ni muhimu sana kwa binadamu hivyo kupitia vyanzo tulivyo navyo vitusaidie upatikanaji rahisi wa maji kote nchini, kupitia kodi tunazo lipa serikali iwekeze nguvu nyingi katika hili.
Jambo zuri, ni moja wa vitu tunavipa kipaumbele, maana hata ukiangalia mambo ya afya. Tukiweza kupata maji safi tunapunguza magonjwa kwa asilimia kibwa sana.

Serikali sikivu inasikia
 
Back
Top Bottom