Utawajengea wakwe zako nyumba?

Kuna mkaka ninamfaham yupo vizuri sana kiuchumi lakini kumpa mkewe japo elf 50 ya matumizi binafsi hampi sembuse kujengea wakwe nyumba...kuna watu ni wabinafsi sana.
 
Kuna mkaka ninamfaham yupo vizuri sana kiuchumi lakini kumpa mkewe japo elf 50 ya matumizi binafsi hampi sembuse kujengea wakwe nyumba...kuna watu ni wabinafsi sana.
Aisee!

Ila watu kama hao wapo. Kuna mmoja nilisikia yeye alikuwa akirudi nyumbani kutoka kazini, anakagua sukari mpaka vyombo vya chakula kama kuna iliyopungua. Kwake alikuwa haendi mgeni, hata mama yake mzazi sembuse ndugu wa mke.
 
Shida yote hapa ni umasikn tu. Hakuna kingine. Sasa kama Hela ipo Kuna shida Gani?
 
Mkuu, huko unakoenda siyo!

Tuheshimiane tu hata kama tuko nyuma ya keyboard. Huwezi jua kesho na keshokutwaπŸ™
Siyo kisa nipo nyuma ya keyboard mzee, Wewe umeelewaje jibu langu? Umezungumzia uchoyo kama kitu kibaya nimekujibu hivyo kwa maana ya kuonesha uchoyo una uzuri wake.
 
Ni jambo la kawaida sana, sasa Kama mkeo unampenda unashindwaje kufanya jambo kwa ajili ya wazazi wake Kama uwezo upo? Inakuletea heshima zaidi
 
Anhaa akija mwamba mwingine anachinjiwa kuku ila wewe ukienda ni mwendo wa soda ya fanta na ugali samaki hizo ni dharau kweli kweli

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Hiyo sio dharau, kila mtu anakuwa treated kulingana na level yake. Wewe kama huna uwezo, kuku kwako unanunua sikukuu tu wakati mkwe mwenzio kununua kuku kwake ni sawa na mchicha usitake muwe treated sawa.
Kama mkwe mwenzio wakilia shida ugonjwa au msiba anajitoa mara moja laki kadhaa hizo, wewe unatoa pole na maombi hamuwezi kuwa sawasawa kwenye mapokezi. Dunia iko hivyo ukijua kujipima unaounguza expectations
 
Mnaweza mkawa mwili mmoja lakini kia mmoja ana Hela zake na bajeti zake!hiyo dhana ya mwili mmoja inatoka wapi mkuu!!?

Wengi wanaoana lakini uchumi hauoani!!!

Sasa kama uchumi hauoani unawezaje kujenga kwa wakwe wakati mmeoana nusu yaani via vya uzazi pekee!!?
 
Uwatendee kama wazazi wako
Wao wana watoto wao wawahudumie wazazi wao, na mimi nina wazazi wangu nitawahudumia wazazi wangu. Familia nyingi za kiafrika ni masiki kwa sababu ya kuendekeza upuuzi unaoitwa undugu. yaani mtu hun ahata vinasaba nae unasema ni mzazi wako? tuache kufanya mambo mepesi yaonekane magumu. Mimi nimemuoa mtoto wao isiwe kigezo cha kutaka mimi nihudumia family tatu
 
Maisha ni mapana sana kuliko unavyohisi mkuu
 
Ni jambo la kawaida sana, sasa Kama mkeo unampenda unashindwaje kufanya jambo kwa ajili ya wazazi wake Kama uwezo upo? Inakuletea heshima zaidi
βœ…πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ™
 
Aisee!

Kwamba hakuna kitu kinachoitwa usawa kwenye hii dunia?
 
Shida yote hapa ni umasikn tu. Hakuna kingine. Sasa kama Hela ipo Kuna shida Gani?
Kwa wengine ni kama mwiko. Na mwenye mtazamo huo hawezi kuwajengea hata kama angepewa utajiri wote wa Elon Musk.
 
Wewe kama kichwa cha famili, unaweza kuweka mambo sawa, halafu:
1. Hela ya mke wako inakuwa ya kwako

2. Hela yako inakuwa ya kwenu.

Na, wakati muafaka ukifika, mtawajengea wazazi wenu wote nyumba, ukianza na wa kwako wa kukuzaa, kisha wakwe zako.
 
Wewe kama kichwa cha famili, unaweza kuweka mambo sawa, halafu:
1. Hela ya mke wako inakuwa ya kwako

2. Hela yako inakuwa ya kwenu.

Na, wakati muafaka ukifika, mtawajengea wazazi wenu wote nyumba, ukianza na wa kwako wa kukuzaa, kisha wakwe zako.
Ngumu sana mkuu!Kuna watu tulisomesha hadi mashemeji lakini Bado hatukuaminika!!Hadi unatuma Hela za matumizi Kwa wakwe lakini hamna kitu!

Tukaamua tuishi tu na kukubali wake zetu ni wabinafsi Dana mkuu!

Hiyo achana nayo !we fanya nafsi inavyokutuma!!
 
Hyo hela kafanye mambo muhimu mengine , kwani kazaliwa kwao pekee??? Au nduguze wanafanya kazi gani ??
Mwisho mambo ya wakwe sio jukumu lako , jua linatuwakia sote sawia, kujjibebesha mzigo isyokuhusu ni utoto.
Kajenge ghorofa , waachie wanao kama inheritance , wakwe malizana nao kwa mahari na kusaidia kidogokidogo
 
Ni kweli, ni ngumu, hasa kama haikuwa umeiweka huo msingi tokea mwanzoni. Lakini siyo kwamba haiwezekani.

Ila pole sana mkuu ikiwa ni wewe ndiye uliyeipitia hiyo changamoto.
 

Kama wanakaa nyumba duni na wewe unauwezo kwa nini usiwajengee?
Kama unaweza kuwasaidia watu ambao hata huna uhusiano nao kwa nini iwe tatizo kuwasaidia wakwe zako?
Wewe wajengee tena Nyumba nzuri tu kulingana na uwezo wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…