Utawajengea wakwe zako nyumba?

Utawajengea wakwe zako nyumba?

Jenga uchumi wa familia yako,
Kujjipendekeza kujenga kwenye familia ya watu wengine ni upuuzi,
Unajenga kwa wazazi wako, halafu wew unakufa na nyumba tatu na watoto wanne,

Si bora ujengee watoto wako ili future iwe nzuri, hao wakwe unaowajengea in most cases hawana more than 20 years za kuishi
 
Nitajenga kwenye uwanja wangu nawahamishia hapo, siku yakiisha nao wameisha kila mtu akale alikopeleka mboga. Maisha yenyewe sasa hivi tunaishi kimachale machale tu hakuna kufumba macho yote.
Haipaswi kuwa hivyo mkuu.
 
Jenga uchumi wa familia yako,
Kujjipendekeza kujenga kwenye familia ya watu wengine ni upuuzi,
Unajenga kwa wazazi wako, halafu wew unakufa na nyumba tatu na watoto wanne,

Si bora ujengee watoto wako ili future iwe nzuri, hao wakwe unaowajengea in most cases hawana more than 20 years za kuishi
Mkuu, huo ni mtizamo wa kibinafsi. Wewe si kwa ajili ya manufaa yako binafsi. Mafanikio yako yanapaswa kuwagusa na wengine, hata wasiokuwa na undugu nawe.

Kama utakuwa na mpango wa "kuwanufaisha" hata wasiokuwa damu moja nawe, wazazi na wakwe zako wanapaswa kuwa wa kwanza kwenye hiyo orodha.
 
Kama mtoto wao tunakaa nae kwa amani na upendo nitawajengea ila kama kuna vurugu sitawajengea ili kuepuka hasara ya kujenga ukweni. Na pia nitaangalia kama wakwe zangu wananiheshimu. Unakuta masela mmea nyumba moja lakini kuna wenzako wengine wanapewa heshima kutokana na kipato chao huku we kapuku ukidharaulika ukweni hata kuku huchiwi wanachiwa wenzako. Ukweni kuna dharau sana kama huna kitu ukilinganishwa na watozi wenzako. Labda uwe peke yako ndio umeoa huko hakuna kenge mwingine wa kulinganishwa nawe
 
Anhaa akija mwamba mwingine anachinjiwa kuku ila wewe ukienda ni mwendo wa soda ya fanta na ugali samaki hizo ni dharau kweli kweli

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom