Utawala Bora hauletwi na Sheria zinazotungwa, utawala bora unaletwa na kiongozi aliyeko madarakani

Utawala Bora hauletwi na Sheria zinazotungwa, utawala bora unaletwa na kiongozi aliyeko madarakani

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Unaweza ukaona kuwa solution ni sheria ama kubadilishwe na katiba,lakini kwa ukweli hasa katiba inaweza kubadilishwa lakini bado mambo yakawa yale yale tu.

Hapa tanzania kuna watu wanalalamika kuna jambo hili limefanyika ni kinyume na sheria mara jambo lile ni kinyume na sheriaa..

Hii maana yake ni kuwa sheria imeweka utaratabu mzuri wa hilo jambo lakini sheria inakeukwa na hakuna mtu anachoweza kufanya dhidi ya huyo aliyekeuka.

Hii maana yake mtawala anaweza kuamua atakaalo maadamu tu dola iko chini yake hakuna cha kumzuia.

Ukiona kiongozi anafuata sheria ujue kuwa anafuata kwa sababu roho yake ni laini kufuata lakini akiamua anaweza asifuate.

Mwalim nyerere aliwahi kusema kuwa katiba ya tanzania inamruhusu kuwa dikteta,lakini kwa nini hakukuwa na udikteta huo wakati wa nyerere tukilinganisha na sasa hivi japo kuwa katiba iliruhusu hayo?

Ni kwa sababu kiongozi amwenyewe aliamua asiwe dikteta wa namna ambayo leo inasemwa.

Mzee kikwete alitawala miaka kumi kwa katiba ile ile ambayo utawala huu inatawala,lakini kwa nini sasa hivi kuna watu wanalalamika zaidi kuliko mwanzo na katiba ni ile ile ?

Kwa sababu kiongozi ndo ana mamlaka yote na wala sio sheria au katiba.

Kudai sheria irekebishwe wakati ambao sheria hizo hizo zilizokuepo unaona kuwa zinakeukwa na h!una uwezo wa kuwafanya lolote wakeukaji maana yake ni kuwa hata hizo ambazo unadai zitungwe zingine ama zirekebishwe zitavunjwa pia na hautakuwa nanpengine pa kwenda kushtaki.

Solution ni tuwatengeneze watu ambao watakuwa na moyo wa hiyari wa kufuata sheria,sio unatengeneza sheria alafu unawaacha watu,watu hawa wataendelea kuvunja sheria nzuuuri mulizozitengeneza wenyewe.

Kwa hiyo mtu akishakuwa na dola,mamlaka yote chini yake hauna la kumfanya lolote lile akishaamua jambo.

Hata kuwe na sheria nzuri kiasi gani zinaweza kukeukwa hadharani na bado wewe usiwe na la kufanya na kiongozi akasema potelea mbali nafanya hivi na wananchi acha wajue nani atakayesema nyoko ?

Wakuu utawala ni jambo nyeti sana,ukiona kuwa mumesikilizwa migomo yenu basi mjue kiongozi kaamua kuwa na roho nzuri tu na sio ati ni nguvu ya ummah.

Kwa mtawala hakuna nguvu ya ummah,akiamua umma unaweza ukatokomea gizani.


Njia nzuri ni kumshauri kiongozi wa aina hiyo ya kukeuka sheria na kanuni ni kwa upendo na ustaarabu na wala sio kwa mihemko na ushindani kwa sababu moto huzimwa kwa maji.

Naomba niishie hapa.
 
Back
Top Bottom